Saturday, June 13, 2015



Muongozaji wa video za muziki wa Afrika Kusini, Godfather ataongoza video ya wimbo mpya wa kundi la Yamond Band ‘Cheza Kimadoido’ na Diamond ndiye atakayeigharamikia. Meneja wa kundi hilo, Said Fella, amesema Yamoto Band watasafiri Jumatatu kuelekea nchini Afrika Kusini kushoot video hiyo. “Wiki ijayo tunatarajia kufanya video mpya ya Yamoto Band na Godfather atakuwa Director.



ALI KIBA NA MBWEMBWE ZAKE SASA

ALI KIBA NA ABDU KIBA WAKIWARUSHA







JE UNAWAJUA HAWA

ABDU KIBA ....ALI KIBA..NA PROMOTA "DMK GLOBAL " KABLA YA SHOW KUANZA



Winga Memphis Depay amekamilisha Uhamishi wake wa Pauni Milioni 31 kujiunga na Manchester United kutoka PSV Eindhoven ya Holland.
Depay, mwenye Miaka 21, amesaini Mkataba wa Miaka Minne ukiwa na nyongeza ya Mwaka Mmoja.
Wakiongea baada ya kusaini Mkataba, Depay alisema hii ni ndoto yake iliyotimia wakati Meneja wa Man United, Louis van Gaal, alisema Mchezaji huyo ana nafasi kubwa kuwa mmoja wa Wachezaji bora kwenye Klabu hiyo.
Mwezi uliopita, Depay alifuzu upimwaji afya yake na kusubiri kusainiwa Mkataba.
Katika Msimu ulioisha Mwezi Mei, Depay ndie aliibuka akiwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Holland, Eredivisie, alipofunga bao 22 na kuibeba PSV Eindhoven kubeba Ubingwa wao wa kwanza wa Holland tangu 2008.

Memphis Depay akiwa na Meneja Van Gaal


Bondia Floyd Mayweather Jr ndio mwanamichezo aliyeingiza pesa nyingi zaidi dunia katika kipindi cha miezi 12 iliyopita kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Mayweather ameingiza kiasi cha dola milioni 300 katika kipindi cha miezi hiyo na fedha nyingi ikiwa imepatikana kutoka na pambano lake na bondia Manny Pacquiao.
Manny ameshika nafasi ya pili katika orodha hiyo huku nyota wa kandanda Cristiano Ronaldo akiwa katika nafasi ya tatu kwa wanamichezo waliotengeneza pesa nyingi.
Orodha kamili ipitie katika tovuti ya bbcswahili.com

Ifuatayo ni orodha kamili ya wanamichezo hao
1. Floyd Mayweather, US, US$300m (£194m).
2. Manny Pacquiao, Philippines, $160m (£103.4m)
3. Cristiano Ronaldo, Portugal, $79.6m (£51.4m)
4. Lionel Messi, Argentina, $73.8m (£47.7m)
5. Roger Federer, Switzerland, $67m (£43.3m)
6. LeBron James, US, $64.8m (£41.9m)
7. Kevin Durant, US, $54.1m (£35m)
8. Phil Mickelson, US$50.8m (£32.8m)
9. Tiger Woods, US, $50.6m (£32.7m)
10. Kobe Bryant, US, = $49.5m (£32m)

waliotembelea blog