Mtoto wa Miaka 8, Martha Godfrey amejinyakulia kitita cha Tsh Milioni
Moja leo baada ya kuwabwaga wenzake watano walioingia tano bora katika
Shindano la kusoma Biblia hapa Mkoani Kagera. Shindano lililokuwa
likishindaniwa na watoto walio Chini ya Umri wa Miaka 15 ambalo
lilishirikisha Wilaya mbalimbali za hapa Mkoani Kagera. Wilaya
zilizoshiriki ni Muleba, karagwe na Misenyi na katika mashindano hayo
kumalizikia hapa Bukoba Mjini kwa Kumpata Mshindi kwenye Fainali
iliyokuwa ya kukata na shoka iliyofanyika leo katika Uwanja wa Kaitaba
Bukoba Mjini. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.
Watoto walioingia fainali na hatimae kumpata mshindi ni Neema Masembejo,
Jonathan Kasika, Enock Joel, Neema Jackson na Martha Godfrey. Fainali
hizo zilipambwa na Wasanii mahili wa Nyimbo za Injili kutoka Jijini Dar
es salaam. Rose Muhando, Bonny Mwaitege na Gaston Sapula. Ambao
walilipamba vilivyo Shindano hilo na kuhudhuriwa na Umati wa Watu wengi
wakiwemo Viongozi wa Dini na wa Siasa. Katika Shindano hilo watoto wengi
walishiriki lakini waliweza kupatikana Watoto 5 ambao waliingia hatua
ya Fainali na kupata washindi watatu na hatimae kumpata mshindi Martha
Godfrey. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.
Mashindano haya ya Kusoma Biblia ni ya Kwanza kwa Mkoa wa Kagera na
yaliandaliwa na Radio Kasibante fm 88.5 kupitia kipindi chake cha Gospal
Flava na Mdhamini Mkuu ambaye pia ndie alikuwa Mgeni rasmi Mbunge wa
Jimbo la Bukoba Mjini maarufu 'swahiba' Mh. Balozi Khamis Kagasheki.
Picha na Faustine Ruta, Bukoba.
Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini maarufu 'swahiba' Mh. Balozi
Khamis Kagasheki akitoa neno mbele ya Umati Mkubwa wa Watu
waliojitokeza kwa Wingi wakati wa Fainali za Shindano la Biblia kwa Mkoa
wa Kagera leo Jumapili.
Gaston Sapula ndie aliyeanza kufunguka!
Gaston sapula akiwaburudisha kwa nyimbo za dini Mashabiki!
Gaston Sapula na Vijana wake wakitoa Burudani
Wimbo wake wa Mbuyu ulianza kama mchicha ukishika kasi! Vijana na Bosi wao wakiendesha!!
Usipime!! Gaston Sapula na Vijana wake wakifanya yao kwenye Fainali ya kusoma Biblia Bukoba leo jumapili.
Enock Joel.
Kauli mbiu yao ikiwa inatoka Mithali 10:1 -Mwana mwenye hekima humfurahisha Babaye bali mwana mpumbavu ni mzigo kwa mamaye.
Mtoto
Martha Godfrey ambaye alishinda Sh Milioni moja kwenye Fainali ya
kusoma Biblia ambapo yeye alitoa somo lake kutoka Kumbukumbu la Torati
4:1-10
Jonathan Kasika
Neema Jackson
Neema
Masembejo, Jonathan kasika, Martha Godfrey, Enock Joel na Neema Jackson
wote walitinga hatua ya fainali hiyo na Martha mwenye umri wa miaka 8
akaibuka kidedea katika shindano hilo la kusoma biblia huku kila mmoja
akisoma somo ambalo lilikuwa halifanani na mwingine mstari wa kwanza
mpaka wa kumi. Picha na Faustine Ruta, Bukoba. Watoto hao walifanya
vyema sana katika Usomaji wa Biblia na ikiwa ni mara yao ya kwanza
katika shindano hilo.
Bonny Mwaitege aliingia kwa Mbwembwe Uwanjani na akawashika Watu kiukweli
Muimbaji
maarufu wa nyimbo za injili Boniface Mwaitege (Bony) akiimba nyimbo
kwa hisia mbele ya mashabiki wake kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba mjini
kwenye Fanali za Biblia leo Jumapili.
Henry Mwaibambe(RPC) alimtuza Ndugu yake Bony Mwaitege
Mbunge
wa Bukoba Mjini "Swahiba" Mh. Khamis kagasheki akimtuza Bony Mwaitege
Uwanjani kaitaba baada ya kuburudishwa na mwimbaji huyo nyota wa Nyimbo
za kumsifu Mungu.
Hatarii tupu!
Muimbaji maarufu wa nyimbo za injili Boniface Mwaitege akifanya yake na Madancer wake
Mratibu Joys Roboz hakupimika alipokuwa!!
Mashabiki waliingia kwa Wingi
Kwa Makini wakisikiliza na kuburudika kwa nyimbo za injili.
Mashabiki wakimtuza Bony Mwaitege.
Furaha kwa Mashabiki'
Kwa
Umahiri mkubwa wa Msanii wa Nyimbo za Injili Bony Mwaitege aliweza
kujizolea sifa kutoka kwa Mashabiki wake baada ya kuimba Wimbo wake
Mpya.
Bony Mwaitege akifungua zawadi aliyopewa na Shabiki mbele ya umati!
"Live Bila Chenga" Mwimbaji Bony Mwaitege akiendeleza zoezi la kupata senene!!
Shabiki alitoa zawadi ya Senene kwa Bony Mwaitege na ndipo mwimbji
Gaston Sapula na Bony kuzichangamkia hapo hapo "Live bila chenga"
Mashabiki Jukwaa kuu wakiangalia zoezi la kula Senene likiendelea kushika kasi wakati wa Fainali za Biblia.
Kwa swala zima la Dini hata babu alitinga uwanjani kushuhudia Vijana wakiwajibika kutoa Neno
Mambo ya Bukoba haya!!!
Aaah!! Kumbe tamueee!!
Karibu!! Gaston Sapula(kushoto) na Bony wakishikamana kwa zoezi zima la kuchangamkia zawadi waliyopewa ya Senene!
Mbunge wa Bukoba Mjini Balozi Khamis kagasheki(kulia) akiwa meza kuu ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.
Viongoz mbalimbali wa Dini walijitokeza katika fainali za Kusoma Biblia zilizofanyika kwa mara ya kwanza hapa Bukoba.
Mratibu
wa Shindano hilo Joyce Roboz akifurahia baada ya kukunwa na nyimbo
mbalimbali kutoka kwa wasanii hao wakali kutoka jijini dar es Salaam.
shindano hilo liliandaliwa na ikiwa ni Ubunifu wake mwenyewe Joyce Roboz
na kufankiwa kuchukua sura mpya hapa Bukoba na kuwafanya baadhi ya
Wananchi kutoamini jambo hilo kama linaweza kufanyika.
Diwani Mulungi nae furaha tupu!
Zungusha!!! Muimbaji maarufu wa nyimbo za injili Boniface Mwaitege akitimua vumbi!!
Brother Samwel na Mkewe walipokuwa ni furaha tupu...wakiburudishwa na Mwaitege
Muimbaji wa nyimbo za injili Boniface Mwaitege akicheza na Vijana wake.
Bony Mwaitege alimtuza mwimbaji mwenzake wa injili ose Muhando.
Rose Muhando nae aliingia kwa salamu salamu za Kiface book!!
Rose Muhando akiendelea kutoa burudani kwa Wakaazi wa Bukoba waliohudhuria Shindano hilo kwenye Uwanja wa kaitaba.
Nani zaidi???
Watatu ndani ya kaitaba!!
Rose Muhando akicheza na Shabiki wake
Rose Muhando na Vijana wake wakitawala sehemu yao!
Washindi
wakiwa wameonesha Vitita Vyao(pesa) walizojishindia leo kwenye Fainali
za Mashindano hayo. Na hapa ni kwenye picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi Mh.
Balozi Khamis Kagasheki.