Tuesday, October 8, 2013

first interview gus poyetGus Poyet kocha mpya Sunderland
KLABU ya Sunderland imemteua Kocha wa zamani wa Brighton Gus Poyet kuwa Meneja mpya wa Klabu hiyo ya Sunderland leo Jumatano kuonoa timu kwa miaka matatu.

Sunderland, ambao wako mkiani kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na Pointi 1 katika Mechi 7, walimtimua Paolo Di Canio hapo Septemba 22 baada kudumu kwa Miezi 6 akiongoza Mechi 13 tu.


Klabu hiyo ambayo inajulikana kama "The Black Cats " inashikilia mkia katika ligi kuu ya Premier na ilimpiga kalamu Paolo Di Canio mnamo mwezi wa September baada ya kuhusika na mechi 13 tu.
Ataungana na wasaidizi wake za zamani wa Brighton Mauricio Taricco na Charlie Oatway."nina hamu ya kuwathibitishia uwezo wangu mashabiki--ninataka wawe na imani kwa sababu tunahitaji kushikamana " Poyet, mwenye umri wa miaka 45, ameiambia wavuti wa klabu hiyo.

"Nadhani msingi wa mafanikio yangu katika mechi za nyumbani Brighton ni uhusiano wangu na mashabiki, --na naweza kuona hali hiyo hiyo hapa ,"aliongeza Poyet, ambaye alipigwa kalamu na Brighton mnamo mwezi wa Juni.

"ni changamoto kubwa lakini inanipa motisha na nashukuru kwa kupata fursa hii ya kuongoza katika ligi kuu"
Poyet ambaye ni mchezaji wa zamani wa taifa wa timu ya Uruguay atakua meneja wa sita wa Sunderland katika kipindi cha miaka mitano.
Kocha msaidizi wa Sunderland Kevin Ball amekua akishikilia uongozi wa klabu hiyo tangu Di Canio afutwe kazi kutokana na malalamiko ya wachezaji.
Kocha aliyekuwa wa muda Kevin Ball pale Sunderland, pia inaaminika pamoja na kupewa kibarua hicho cha muda alikuwa analilia nafasi hiyo klabuni hapo. Wengine waliokuwa wanahusishwa ni Steve McClaren, Roberto Di Matteo na Tony Pulis.


KUHUSU POYET
July 2006 - Assistant at Swindon with Dennis Wise taking over as manager
October 2006 - Both Poyet and Wise moved to Leeds keeping the same roles
October 2007 - Becomes first team coach at Spurs under Juande Ramos
November 2009 - Takes over as boss at Brighton, winner the League One title in 2011
June 2013 - Sacked as manager of Brighton after a club inquiry
October 2013 - Appointed Sunderland manager

Sijuhi itakuwaje??
Vincent Kompany, Nahodha wa Manchester City na Mchezaji wa Belgium, atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki hadi 4 baada ya kuumia Nyonga kwenye Mechi ya Wikiendi City walipoifunga Everton Bao 3-1.
Pia, maumivu hayo yatamfanya akose Mechi muhimu za Man City ambako yeye ndio nguzo kubwa kwenye Difensi na Mechi hizo ni za Ligi dhidi ya West Ham, Chelsea na Newcastle, na ile ya UEFA CHAMPIONS Ugenini huko Urusi watakapocheza na CSKA Moscow.

Vicent Kompany chini wakati anauguza majeraha yake wikiendi iliyopita wakati wanacheza na Everton ambapo City walishinda 3-1.Kazi ipo kwa City bila Kompany.
Belgium training
Wachezaji wa Belgium wakifanya mazoezi, akiwemo mchezaji wa  Chelsea Eden Hazar.
Eden Hazard Eden Hazard akionesha mambo yake wakati wa mazoezi hivi karibuni.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah (kulia) akionyesha fomu za kujiunga na Tamasha la Mitindo kwa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini lijulikanalo kama Redd's Uni-Fashion Bash kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi Tamasha hilo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Mahusiano wa Kampuni hiyo,Edith Mushi.

Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Edith Mushi (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za Washindi mbali mbali Watakaoshiriki kwenye Tamasha la Mitindo kwa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini lijulikanalo kama Redd's Uni-Fashion Bash.Tamasha hilo limezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Fimbo Butallah











BINGWA wa dunia wa kanda wa WBF, Fransic Cheka amealikwa wialayani Muheza mkoani Tanga kwa lengo la kutoa hamasa kwa mchezo wa ngumi wilayani hapo.

Kocha wa Ngumu wa Muheza, Charles Muhiru amesema wamemualika Cheka wilayani kwao ili kutoa hamasa kwa mabondia wao ambao nao wana kiu ya kufikia mafanikio ya Cheka.
Muhiru alisema kuwa Cheka atafika Muheza siku ya sikukuu ya pili ya Idd Alhaji na kushuhudia mapambano ya ngumi ya mabondia wa wilayani humo ambayo yatafanyika kwenye Viwanja vya Jitegemee.
Kocha huyo pia aliombva kuungwa mkono na wadau wa mchezo huo kwa lengo la kutoa sapoti kubwa ili kufanikisha ziara hiyo sambamba na mchezo huo kwa ujumla ili kuwawezesha vijanja wanaoingia katika mchezo huo kupata mafanikio na kuliletea taifa sifa kama ilivyokuwa kwa Cheka.

M


TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
VODACOM PREMIER LEAGUE (VPL) 2013/2014



NO. TEAMSPWDLGFGAGDPTS



1Simba SC74301651115



2Young Africans SC7331137612



3JKT Ruvu FC740385312



4Azam FC725096311



5Kagera Sugar FC732285311



6Coastal Union FC725052311



7Mbeya City SC725086211



8Ruvu Shooting FC731375210



9Rhino Rangers FC714278-17



10Mtibwa Sugar FC714258-37



11Tanzania Prisons FC714249-57



12JKT Oljoro FC712448-45



13Mgambo Shooting FC7124211-95



14Ashanti United SC7025415-112




TOTAL491421141001000126




AS FOR: 06/10/2013







Abas Kinzasa kwa jina la usanii anaitwa 20 Percent akiwa kwenye majonzi baada ya kufiwa na Baba yake mzazi Mzee Kinzasa aliyefariki juzi siku ya Jumapili na kuzikwa siku ya Jumatatu kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Hapa ndipo alikozikwa Mzee Kinzasa baba mzazi wa 20 Percent aliyefariki siku ya jumapili na kuzikwa siku ya jumatatu kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichopo Wilaya ya Mkuranga

Msanii 20 Percent na ndugu zake wakiweka udongo kwenye kaburi la marehemu baba yake mzazi mzee Kinzasa
Abas Kinzasa kwa jina usanii anaitwa 20 percent akieleza jambo kandokando ya kaburi la  Baba yake mzazi Mzee Kinzasa aliyefariki siku ya jumapili na kuzikwa siku ya jumatatu kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichopo Wilaya ya Mkuranga

Marehemu mzee Kinzasa akiombewa dua baada ya kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele
Hii ndio nyumba aliyoicha marehemu Mzee Kinzasa iliyoko kwenye kijiji cha Kimanzichana
Baadhi ya wananchi waliofika msibani
Wazee wakiesabu kiasi cha pesa kilichopatikana kwa watu waliotoa rambirambi zao kwenye msiba wa marehemu Mzee Kinzasa
Mzee
akieleza jambo kwenye msiba wa baba yake na 20 Percent aliyefariki siku
ya Jumapili na kuzikwa nyumbani kwake kwenye kijiji cha Kimanzichana
Mwenyekiti wa mtaa wa Kimanzichana akimkabidhi mtunza pesa, pesa alizopewa na wananchi kwa ajili ya rambirambi
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye msiba wa baba yake na 20 Percent kwenye
kijiji cha Kimanzichana kilichoko wilaya ya Mkulanga mkoani Pwani hapo jana mchana
Mtunza pesa akieleza kiasi cha pesa zilizopatikana baada ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika msibani hapo  kutoa rambirambi zao.

siku-tundu-lisu-alipokutana-na-jk-ikulu-jijini-dar-es-salaam_f685e.jpg
Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu amesema hotuba ya kila mwezi ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa siku tatu zilizopita, imejaa maneno mengi ya kuambiwa hasa kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, ikiwa ni pamoja na uteuzi alioufanya wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za makao makuu wa Chadema, Lissu alisema kauli zilizotolewa na Rais za kumshutumu yeye (Lissu) kuzungumza uongo bungeni, kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba zilikuwa zakuambiwa, hazina ukweli wowote.
"Pengine rais Kikwete angesoma hotuba yangu niliyoitoa bungeni asingezungumza vile kuhusu mimi."


Katika hotuba yake, Rais Kikwete alimshutumu Lissu kwa kusema kwamba katika uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa Rais hakuheshimu mawazo ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

Rais Kikwete alisema kauli hiyo ya Lissu ni uzushi, uongo na uzandiki wa hali ya juu huku akisisitiza kuwa Lissu alitoa kauli hiyo ili kupotosha ukweli na pengine isaidie kujenga hoja yake ya kutaka Rais asiteue wajumbe 166 wa Bunge Maalum la Katiba.

Katika maelezo yake ya jana, Lissu alisema kuwa alipinga Rais kuteua wajumbe wa Bunge la Katiba kwa sababu hata wakati akiteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya kupelekewa majina na taasisi mbalimbali, alifanya uteuzi wa watu ambao hawakupendekezwa na taasisi mbalimbali, ikiwemo TEC na CCT.

Lissu ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala alisema kamati hiyo ilipokutana na wawakilishi wa TEC na CCT (majina yanahifadhiwa kwa kuwa hatukuwapata kuthibitisha hilo), wawakilishi hao walikiri wazi kuwa majina waliyoyapendekeza sio ya watu walioteuliwa na Rais.

"Sasa hapo uongo na uzandiki wangu ni nini, labda hao wawakilishi wa TEC na CCT walisema uongo, hata wawakilishi wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania nao waliieleza kamati kuwa majina waliyoyapendekeza, sio ambayo Rais aliteua" alisema Lissu.

Alisema kuwa Rais amemshutumu bila kuujua ukweli, kusisitiza kuwa kama angesoma hotuba yake aliyoisoma katika mkutano wa 12 wa Bunge, asingezungumza maneno hayo dhidi yake.

"Ndio maana katika hotuba yake rais Kikwete alikiri wazi kwa kusema, nimeambiwa, nimesikia, nimeelezwa ukweli ni kwamba wasaidizi wake wamemdanganya," alisema Lissu.
MCHEKESHAJI mkongwe nchini, Amri Athuman 'King Majuto' ametangaza nia yake ya kujitosa kwenye siasa akitaka kuwania Ubunge katika Jimbo la Tanga Mjini katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
Akihojiwa na kituo cha Clouds FM, Mzee Majuto mwenye umri zaidi ya miaka 60, alisema Mungu akimjalia atajitosa kwenye ubunge jimboni humo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), akidai kiu hiyo imechochewa na mafanikio ya wasanii waliojitosa kwenye siasa na kufanya vyema.
Mzee Majuto alisema, uzoefu alionao katika kuishi kwake mjini Tanga itamwezesha kuwatatulia kero na kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi wenzake iwapo Mungu atamjalia katika kusudio lake.
Kadhalika Muigizaji, ambaye pia ni mtayarishaji na muongozaji wa filamu nchini, Yekonia Watson 'Amani' amesema matarajio yake miaka michache ijayo ni kujitosa kwenye siasa akitaka kuwania Ubunge kabla ya kuangalia nafasi ya juu zaidi kwa maana Rais.
Akizungumza na MICHARAZO jioni, Watson alisema anaamini ana uwezo na kipawa cha uongozi hivyo anaweka mambo sawa kabla ya kujitosa jumla kwenye duru hilo, japo yeye hakuweka bayana atajitosa kupitia chama gani.
"Kwa sasa ni mapema mno, ila nitaanzia Ubunge kisha kuangalia nafasi ya juu, ila muhimu Mungu anipe uhai na umri wa kufanikisha hilo," alisema mkali huyo anayejiandaa kuachia filamu yake mpya iitwayo 'Uwanja wa Vita' aliyoigiza na wasanii kadhaa nyota akiwamo Irene Uwoya.


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewahakikishia Watanzania kuwa uchaguzi wa kupata Kamati mpya ya Utendaji ya shirikisho utafanyika Oktoba 27 mwaka huu kama ilivyopangwa.
“Wazungu wanasema ije mvua au jua, uchaguzi utafanyika. Isipokuwa tunachotaka kuhakikisha ni kuwa unakuwa uchaguzi huru na wa haki,” amesema Rais Tenga wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF leo mchana (Oktoba 7 mwaka huu).

Amesema mchakato unakwenda vizuri kilichobaki ni revision (mapitio) na rufani, masuala ambayo yako mbele ya Kamati ya Rufani ya Maadili na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi.

Rais Tenga amesema lengo la hatua hizo si kuzuia watu wasigombee kwani ni lazima mambo ya msingi ikiwemo sifa za wagombea yaangaliwe, lakini kwenye haki ni lazima kuhakikisha inatendeka hata kama ni kwa mtu mmoja.

Mchakato wa uchaguzi ulivutia waombaji 58 ambapo watatu wamekata rufani Kamati ya Rufani ya Uchaguzi kupinga kuondolewa na Kamati ya Uchaguzi wakati wengine wanane masuala yao yamepelekwa Kamati ya Rufani ya Maadili kwa njia ya mapitio (revision) ili kupata mwongozo wa utekelezaji.

waliotembelea blog