Wednesday, June 24, 2015

 

 

WWW.BUKOBASPORTS.COM
 
 
UONGOZI wa Coastal Union,Wagosi wa Kaya umeingia mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja kuifundisha timu ya Coastal Union katika msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania Bara itakayoanza Mwezi Agosti mwaka huu .
Kocha huyo ambaye ni raia wa Uganda, ameingia karandasi ya kuinoa Coastal Union leo jijini Tanga mbele ya Katibu Mkuu wa timu hiyo, Kassim El Siagi na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Albert Peter. Akizungumza kwa njia ya simu baada ya kumalizika zoezi hilo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa kutokana na umahiri aliokuwa nao kocha huyo wana imani ataipa mafanikio timu yao katika ligi kuu msimu ujao.

 “Uwezo wa kocha Mayanja unatupa matumaini makubwa ya mafanikio ukizingatia ana uwezo wa kufundisha na kupata mafanikio hivyo tunaamini kuja kwake kwetu itakuwa chachu katika maendeleo”, alisema Assenga
Mayanja aliwahi kuzifundis
ha timu za soka Kiyuvu FC ya Rwanda,timu ya Mamlaka ya Mapato (URA),Vipers FC ya Bunamwaya na KCC zote za Uganda amesema kutua kwake kwenye timu Coastal Union kunampa faraja hivyo atahakikisha anatoa mchango wake kuipa mafanikio.
Pia alisema mipango yake ni kuhakikisha timu inang’ara katika michuano ya ligi kuu msimu ujao ikiwa ni pamoja na kubadili aina ya mchezo wa timu hiyo ili iweze kupata mafanikio kwa kuhirikiana na wachezaji, mashabiki na uongozi kwenye medani za kitaifa na kimataifa.



Mchezaji wa Yanga Juma Abdul (kulia0 akimtoka mchezaji wa Friends Rangers leo kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Karume

TIMU ya Yanga yenye maskani yake mtaa wa Jangwani na Twiga jana iliifunga Friends Rangers mabao 3-2 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Yanga ambayo ilikuwa inawajaribu wachezaji wake ambao wamesajiliwa msimu huu ilianza kupata bao la kwanza dakika ya 11 lililofungwa na Kpah Sherman akimalizia pasi ya Busungu
Hata hivyo Friends Rangers walisawazisha bao hilo dakika ya 25 lililofungwa na Mussa Juma lakini dakika ya 37 Yanga waliongeza bao la pili lililofungwa na Busungu baada ya kupokea pasi toka kwa Sherman bao lililodumu hadi mapumziko.

Kocha wa timu ya Taifa 'Taifa stars' Charkes Mkwasa akiongea na waandishi wa habari leo wakati alipotangaza kikosi chake cha kuivaa Uganda. Kulia ni msaidizi wake Hemed Morocco
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine leo amemtambuisha kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Charles Boniface Mkwasa mbele ya waandishi wa habari.
Akiongea na waandishi wa habari, Mwesigwa amewaomba wadau wa mpira wa miguu nchini kuwapa sapoti makocha hao wazawa wanaoanza kazi kesho kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda julai 4, 2015 jijini Kampala.
Mara baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari, Mkwasa amesema anashukuru kwa TFF kumpatia nafasi hiyo ya kuingoza Taifa Stars na msaidizi wake Hemed Morocco, na kuomba watanzania kuwapa sapoti.
Mkwasa amesema cha kwanza atakachokifanya na msaidizi wake Morocco ni kurudisha imani ya watanzania juu ya timu yao ya Taifa, kisha watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri katika michezo inayowakabili.


Mh. January Makamba na mkewe, Ramona Makamba(kulia) baada ya kuwasili mkoani hapa Kagera kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania Urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho cha CCM. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Mh. January Makamba na mkewe, Ramona(kulia) mara baada ya kushuka kwenye Ndege leo hii Jumatano asubuhi juni 24, 2015. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Mh. January Makamba akisalimiana na Katibu wa Vijana Mkoa wa Kagera
Mh. January Makamba akisalimiana na Wanafunzi wa Sekondari waliokuwa Uwanjani hapo ambao bila Shaka walikuwa wanasoma masomo ya Ndege inavyoruka na kutua na mengineyo kiujumla leo jumatano juni 24, 2015. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Mh. January Makamba akisaini kwenye kitabu cha Wageni kwenye Uwanja Ndege Bukoba.
Mh. January Makamba na mkewe, Ramona wakiteta jambo kwa furaha.
Msafara wa Bodaboda kuelekea Mjini kwenye mzunguko na kugeuka kwenye Makao makuu ya CCM Mkoa wa Kagera




Mjini Bukoba, Bodaboda wakimsindikiza Mh. Januari Makamba



Makamba akisalimia Wakazi wa Mji wa Bukoba walijitokeza kwa wingi
January Makamba ameendelea na Ziara yake ya Kusaka Wadhamini katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania na leo hii jumatano juni 24, 2015 yupo hapa Mkoani Kagera akiomba Uzamini. Mh. January Makamba amepokelewa na wakazi wengi wa Mkoa wa Kagera wakiwemo Vijana walijitokeza kwa wingi kumpokea. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Mh. Januari Makamba baada ya kusalimiana na Wakazi waliojitokeza kwenye Makao makuu ya CCM ameelekea katika Hospitali ya Mkoa kuwaona wagonjwa mbalimbali na Baada ya hapo ameelekea Wilayani Misenyi kwenda kusalimia Wakazi wa huko na Kuwaomba wamdhamini kwa kuweka saini fomu zake za kuwania Urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho cha CCM.
Mh. Januari Makamba Akitia saini Katika kitabu cha wageni Ofisi za CCM

January Akizungumza na wakazi wa Bukoba waliojitokeza kumsikiliza katika katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kagera leo

Wakazi wa Mji wa Bukoba wakimsikiliza Mh. January Makamba kwa makini leo hii jumatano.


Liverpool imefikia makubaliano ya kumsaini Roberto Firmino kwa Dau la Pauni Milioni 29 ambalo litamfanya awe Mchezaji wa Pili kununuliwa na Klabu hiyo kwa Fedha nyingi.
Firmino, mwenye Miaka 23, ni Straika wa Klabu ya Bundesliga huko Germany, Hoffenheim, na sasa yuko Nchini Chile akiichezea Brazil kwenye Fainali za Copa America.
Mkuu wa Liverpool, Ian Ayre, yupo Nchini Chile kusimamia Dili hii ambayo itampa Staa huyo Mkataba wa Miaka Mitano huku tayari inasemekana washaafikiana kuhusu maslahi yake binafsi.
Firmino ameifungia Hoffenheim Bao 49 katika Mechi 153 na Juzi aliipigia Brazil Bao la Pili wakati wanaichapa Venezuela 2-1 na kutinga Robo Fainali ya Copa America.

Mwaka 2011, Liverpool ilimsaini Straika wa Newcastle, Andy Carrol, kwa Dau la Pauni Milioni 35 ambalo ndio kubwa katika historia ya Klabu hiyo.
Hivi karibuni Liverpool ilimnunua Straika wa Burnley Danny Ings pamoja na Kipa Adam Bogdan, Beki Joe Gomez na Kiungo James Milner tayari kwa ajili ya Msimu mpya.
Lakini wapo njiani kumpoteza Staa wao mkubwa Raheem Sterling ambae amegoma kusaini Mkataba mpya na kutaka kuhama huku Manchester City wakitoa Ofa mbili ambazo zimekataliwa.
Roberto Firmino

waliotembelea blog