Saturday, November 29, 2014


Arsenal Jack Wilshere atakuwa nje ya Uwanja kwa Miezi Mitatu baada ya kufanyiwa operesheni ya enka yake hii Leo.
Wilshere aliumia Jumamosi iliyopita wakati Arsenal inachapwa Bao 2-1 na Manchester United Uwanjani Emirates.
Habari hizi za operesheni ya Wilshere zimethibitishwa na Arsenal na mwenyewe Wilshere aliposti Picha yake Mtandaoni akiwa Kitandani baada ya kufanyiwa hiyo operesheni.

Kukosekana kwa Wilshere ni pigo kubwa kwa Arsenal ambayo sasa imekumbwa na Majeruhi wengi baada ya pia Jumatano kupoteza Wachezaji wawili walioumia kwenye Mechi ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LIGI walipoifunga Borussia Dortmund Bao 2-0.
Wachezaji hao wawili ni Nahodha wao Mikel Arteta na Yaya Sanogo ambao watakuwa nje kwa muda abao unaweza kufikia hata Wiki 6.

Majeruhi wengine wa Arsenal ni Mesut Özil, Theo Walcott, Danny Welbeck, Mathieu Debuchy, Abou Diaby, Wojciech Szczesny na David Ospina.
Kuhusu balaa hilo, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameeleza: “Hali hii ya majeruhi ni tatizo kwani tuna Mechi nyingii.”


RATIBA - LIGI KUU ENGLAND
Jumamosi Novemba 29

15:45 West Brom v Arsenal
18:00 Burnley v Aston Villa
18:00 Liverpool v Stoke
18:00 Man United v Hull
18:00 QPR v Leicester
18:00 Swansea v Crystal Palace
18:00 West Ham v Newcastle
20:30 Sunderland v Chelsea

Jumapili Novemba 30
16:30 Southampton v Man City
19:00 Tottenham v Everton

*********************************** 

RATIBA - SERIE A
Jumamosi Novemba 29

2000 Sassuolo v Verona
2245 Chievo v Lazio

Jumapili Novemba 30
1700 AC Milan v Udinese
1700 Cesena v Genoa
1700 Empoli v Atalanta
1700 Palermo v Parma
2000 Juventus v Torino
2245 AS Roma v Inter Milan

***********************************

RATIBA - LA LIGA
Ijumaa Novemba 28

22:45 Real Sociedad v Elche

Jumamosi Novemba 29
18:00 Getafe v Athletic Bilbao
20:00 Espanyol v Levante
22:00 Malagav Real Madrid
00:01 Celta Vigo v Eibar

Jumapili Novemba 30
14:00 Atletico Madrid v Deportivo La Coruna
19:00 Sevilla v Granada
21:00 Cordoba v Villarreal
2300 Valencia v Barcelona

*********************************** 

RATIBA - BUNDESLIGA
Ijumaa Novemba 28

22:30 SC Freiburg v Stuttgart

Jumamosi Novemba 29
17:30 Bayer Leverkusen v Cologne
17:30 FC Augsburg v Hamburg
17:30 Hertha Berlin v Bayern Munich
17:30 Schalke v Mainz
17:30 Werder Bremen v SC Paderborn 07
20:30 Hoffenheim v Hannover 96

Jumapili Novemba 30
17:30 Wolfsburg v Borussia Monchengladbach

19:30 Eintracht Frankfurt v Borussia Dortmund

Bayern, baada ya Mechi 12 za Ligi, wako kileleni wakiwa Pointi 7 mbele ya Timu ya Pili Wolfsburg.
Hertha Berlin wao wako Nafasi ya 13 wakiwa Pointi 16 nyuma ya Bayern.

Wolfsburg wao Jumapili watakuwa Nyumbani kuiva Borussia Monchengladbach ambao wako Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 3 nyuma yao. Vigogo Borussia Dortmund, ambao Msimu huu wameporomoka vibaya kwenye Bundesliga wakiselelea Nafasi ya 16 ikiwa ni Nafasi ya 3 toka mkiani, Jumapili wako Ugenini kuivaa Eintracht Frankfurt ambayo iko Nafasi ya 12 wakiwa Pointi 4 mbele ya Dortmund.

waliotembelea blog