Jokate (kushoto) akizungumza
katika mkutano wa jukwaa la sanaa. Katikati ni katibu mkuu wa Chama cha
Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz), Hassan
Bumbuli na mbunifu mkongwe wa mavazi, Asia Idarous.
Mbunifu mkongwe wa mavazi nchini,
Asia Idarous (kulia) akisisitiza jambo katika mkutano wa jukwaa la
sanaa. Katikati ni Katibu mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za
Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz), Hassan Bumbuli na msichana mwenye
vipaji vingi, Jokate Mwegelo.
Katibu mkuu wa Chama cha Waandishi
wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz), Hassan Bumbuli
(Katikati) akizungumza katika mkutano wa jukwa la wasanii, kulia ni
Mbunifu mkongwe, Asia Idarous na msichana mwenye vipaji vingi, Jokate
Mwegelo.
Katibu mkuu wa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mngereza akifafanua jambo katika mkutano huo.
Msanii mkongwe wa maigizo na filamu nchini, Mzee Jangala akifuatilia mkutano wa jukwaa la sanaa.
Katibu mkuu wa na Baraza la Sanaa
la Taifa (Basata) Godfrey Mngereza akionyesha kipaji chake cha kupiga
zeze na kuimba kwa kushirikiana na wasanii wengine waliohudhuria mkutano
wa Jukwaa la Sanaa.
Msichana mwenye vipaji lukuki
nchini, Jokate Mwegelo amewataka wasanii kuwa wabunifu ili kupata
mafanikio katika sanaa na shughuli zao za kila siku.
Jokate alitoa wito huo wakati
akitoa mada katika Jukwaa la Sanaa la lililoandaliwa na Baraza la Sanaa
la Taifa (Basata) kwa kushirikiana na chama cha Waandishi wa Habari za
Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz).
Alisema kuwa sanaa ina wigo
mpana sana na kila msanii anatakiwa kuwa mbunifu ili kujiweka tofauti
na msanii mwingine na kujipatia fedha kwa kutumia ubunifu wake.
Kwa mujibu wa Jokate, yeye
aliamua kupitia kwenye fani ya urembo na mwaka 2006 alifanikiwa kushika
nafasi ya pili katika mashindano ya Miss Tanzania. Alisema kuwa aliamua
kutumia umaarufu wake kujipatia maendeleo pamoja na ukweli kuwa alisomea
mambo ya siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
“Elimu yangu ya mamo ya siasa
haina nafasi kwangu, nilianza kuwa mshehereshaji (MC) katika shughuli
mbalimbali, nikaingia katika fani ya ubunifu wa mabavi (Kidoti Fashion),
nikaanzisha kidoti club ili kupata marafiki ambao tutazungumza lugha
moja,” alisema Jokate.
Mrembo huyo hakuishia hapo kwa
kuingia katika fani ya utangazaji wa vipndi hasa Chanel O, uigizaji wa
filamu, utengenezaji wa nywele, ndala na sasa mwanamuziki.
“Hii yote ni kutafuta ‘chaneli’
za kupata fedha, nimefanikiwa na sasa nina makubaliano yenye thamani ya
Sh 8.5 bilioni na kampuni ya Kichina, Rainbow Shell Craft Company
Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake
ya Kidoti,” alisema.
Mbali ya Jokate, mbunifu maarufu
nchini, Asia Idarous naye aliwataka wasanii kuwa waaminifu na
kujitangaza katika shughuli zao ili kupata maendeleo.
Idarous alisema kuwa msanii
ambaye atakuwa mbunifu na kipaji cha hali ya juu, hataweza kupata
maendeleo kama atakosa sifa ya uaminifu ambayo mara nyingi uendana na
nidhamu katika kazi.
“Mimi nilianza kazi ya ubunifu
wa mavazi miaka ya 1980, mpaka leo nafanya kazi hii, wabunifu wengi
(hata Jokate) amepitia kwangu, siri kubwa ya mafanikio haya ni uaminifu
na nidhamu katika kazi, nimefanikiwa kuanzisha Vazi la Khanga nchini
Marekani na Lady in Red, leo hii ni maarufu,” alisema Idarous.
Katibu Mkuu wa Chama cha
Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz), Hassan
Bumbuli alitoa wito kwa wasanii chipukizi kufuata nyayo za Jokate na
Idarous ili kuweza kufanikiwa katika kazi zao za sanaa.
Bumbuli alisema kuwa ni vigumu
kupata mafanikio katika sanaa bila kuweka wazi kipaji chako hadharani na
hapo ndipo vyombo vya habari vitakuona na kuanza kuandika habari zao.