Tuesday, November 17, 2015


Bao la kwnza limefungwa na Dele Alli dakika ya 39 kipindi cha kwanza na kipindi cha pili Wayne Rooney dakika ya 48.
Mchezo huu ukiongozwa na Mwamuzi Jonas Eriksson


Dakika ya 1 tu Tanzania walikuwa wameshapigwa bao na Yacine Brahimi kwenye marudiano ya mchezo wao wa Kitaifa wa kirafiki wakiongozwa na Refa Neant Alioum kwenye Uwanja wa Stade Mustapha Tchaker, El Bouleïda (Blida) Algeria.

MAGOLI:
Goli la kwanza limefungwa dakika ya 1 na Yacine Brahimi
la pili likifungwa dakika ya 23 na Faouzi Ghoulam, Bao la tatu dakika ya 43 limefungwa na Riyad Mahrezna hivyo kwenda mapumziko Tanzania ikiwa nyuma ya bao 3-0 nyuma ya Wenyeji
wao Algeria. Bao la (4)nne limefungwa na Slimani islam kwa mkwaju wa penati dakika ya 49 na kufanya Algeria kuongoza bao 4-0.
Faouzi Ghoulam alifunga tena bao kwa mkwaju wa penati dakika ya 59. Dakika ya 72 bao tena kupitia kwa Carl Medjani. Dakika ya 75 Slimani islam anaifungia bao la 7 na kufanya 7-0(Agg 9-2).


KADI ZA NJANO:
Farid Mussa, Himid Mao, Kelvin Patrick Yondani, Haji Mngwali, Mudathiri Yahya na dakika ya 41 tena Mudathiri Yahya alifanya rafu tena na kuoneshwa kadi ya njano ya pili na kutolewa na mwamuzi Neant Alioum kwa kadi nyekundu.
Kipindi cha pili dakika ya 48 Nadir Haroub alioneshwa kadi ya njano. Dakika ya 57 Aishi Manula nae analambishwa njano.


RED KADI: 
Mudathiri Yahya Dakika ya 41



Mchezaji wa timu ya mpira wa Kikapu ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ephraim Mlawa (kushoto) akichuana na Juvenary Shichose wakati Bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo hicho lililofanyika, mwishoni mwa wiki katika Kituo cha Michezo cha JMK Youth Park na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kutoa vifaa vya michezo kwa timu zilizoshiriki mchezo wa soka. (Picha na Francis Dande)

Timu za mpira wa kikapu kutoka Chuo cha IFM zikichuana katika Bonanza la michezo la wanafunzi wa chuo hicho.

Kikosi cha timu ya Soka ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), BBF kikiwa katika picha ya pamoja.


Kikosi cha timu ya Soka ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), DIT kikiwa katika picha ya pamoja.


Mshauri wa wanafunzi wa Chuo cha IFM, Khamis Kihongoa akikagua timu ya DIT wakati wa Bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo cha IFM.

Mshauri wa wanafunzi wa Chuo cha IFM, Khamis Kihongoa akikagua timu ya DIT wakati wa Bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo cha IFM.

Mshambuliaji wa timu ya DIT, Shaban Juma (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya BBF, Yohana Galus wakati wa bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.


Manchester United ndio inaongoza kwa kutoa Wachezaji wengi wa Kimataifa kwa huko England na pia Barani Ulaya.Msimu huu, Wachezaji wengi wameteuliwa kuzichezea Timu zao za Taifa na Wachezaji wanaocheza Ligi Kuu England ndio wanaongoza kwa Ulaya huku Man United wakiwa juu kwa kutoa Wachezaji wengi zaidi.
Kwa mujibu wa Takwimu za CIES Football Observatory Digital Atlas, Asilimia 41 ya Wachezaji waliocheza Ligi Kuu England Msimu huu wamechezea pia Timu zao za Taifa Msimu huu huu.
Man United wapo juu kwa kutoa Wachezaji Asilimia 72 ya wale walioteuliwa na Meneja wao Louis van Gaal kucheza Mechi za Ligi Kuu England Msimu huu ambao pia waliteuliwa kucheza Timu zao za Taifa.
Ijumaa iliyopita, Wachezaji wa Man United waliovaa Jezi za Nchi zao ni Michael Carrick, Phil Jones, Chris Smalling, Wayne Rooney na Juan Mata ambao walicheza wakati Spain inaichapa England 2-0, wakati Anthony Martial na Morgan Schneiderlin walikuwa kwenye France iliyoichapa Germany ambayo ilikuwa nayo Bastian Schweinsteiger huku Daley Blind akiichezea Netherlands na Matteo Darmian akiichezea Nchi yake Italy.


Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kitafanya mazoezi leo jioni saa 1 Algeria, sawa na saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki katika uwanja wa Mustapher Tchaker utakaotumika kwa mchezo wa leo jumanne dhidi ya wenyeji Algeria.
Stars inayonolewa na kocha mzalendo, Charles Boniface Mkwasa iliwasili salama jana jioni katika mji wa Blida, uliopo takribani kilometa 75 kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Houari Boumediene jijini Algiers.
Mkwasa amesema mchezo huu watajituma kadri ya uwezo kuhakikisha wanapata ushindi, makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa awali yamefanyiwa kazi na anaamini vijana wake watapambana kusaka ushindi katika mchezo huo.
Wachezaji wote 21 wapo katika hali nzuri, hakuna mchezaj majeruhi hata mmoja, hivyo kocha Mkwasa ana wigo mpana wa kumtumia mchezaji yoyote anayemuhitaji kwa ajili ya mchezo huo.

Mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018, utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Mali na utaanza saa 1:15 usiku (Algeria) sawa na saa 3:15 usiku kwa saa nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki.


Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’, Abdallah Kibadeni ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kujiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza kutimua vumbi Jumamosi Novemba 21, nchini Ethiopia.
Kibadeni anayesaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, amesema wachezaji aliowaita wapo katika hali nzuri na wamekua wakifanya mazoezi na kikosi cha Taifa Stars ambapo wao kama benchi la ufundi wamepata nafasi ya kuwa nao kwa muda mrefu na kutambua maendeleo yao.
“Tumechagua wachezaji kulingana na mahitaji ya timu, tumekua na wachezaji hawa kwa muda mrefu katika vipindi mbalimbali, tuna amini tuliowachagua watafanya vizuri katika michuano hiyo mikongwe barani Afrika” amesema Kibadeni.

Wachezaji walioitwa ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa), Juma Abdul (Yanga) na Kelvin Yondani (Yanga).

Viungo Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Said Ndemla (Simba), Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Deus Kaseke (Yanga), washambuliaji John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga) na Saimon Msuva (Yanga).
Michuano ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21 na kumalizika Disemba 6, ambapo Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A, lenye wenyeji Ethiopia, Rwanda na Somalia.

Wachezaji Said Mohamed, Juma Abdul, Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Salum Abubakar na Ibrahim wanaendelea na mazoezi jijini Dar es salaam chini ya kocha msaidizi Juma Mgunda wakati wanawasubiri wachezaji wengine walioko nchini Algeria na kikosi cha Taifa Stars.
Kundi B lina Bingwa Mtetezi Kenya, Burundi, Uganda na Zanzibar, huku kundi C likiundwa na timu za Sudan, Sudani Kusini, Djibouti na waalikwa wa michuano hiyo timu ya taifa kutoka Malawi.


Ligi Daraja la Pili nchini (SDL) imeanza kutimua vumbi jana katika viwanja 12 mikoa mbali, huku timu 24 zikisaka nafasi nafasi nne za kupanda Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao wa 2016/2017.

Katika michezo iliyochezwa jana matokeo yalikuwa ni Alliance 2 -0 Madini, JKT Rwamkoma 1- 3 Bulyanhulu, Mvuvuma 0 – 0 Green Warriors, Singida United 1 -0 Transit Camp, Mirambo 1 – 0 Abajalo Tabora.
Karikaoo 1 – 0 Cosmopolitan, Mshikamano 1- 1 Changanyikeni, Villa Squad 0 – 2 Abajalo Dar es salaam, Mkamba Ranger 0 -0 The Mighty Elephant, Sabasaba 0 - 1 Mbeya Warriors, Wenda 0 – 0 African Wanderes.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea Novemba 28, kwa timu 24 kucheza katika viwanja 12 mbalimbali nchini kusaka pointi muhimu.


 Mfalme mzee Yusuphy akiwa anawatumbuiza wapenzi wa bendi ya Jahazi modern taaraba Woinde Shizza,Arusha



Bendi ya muziki wa taarabu ijulikanayo kwa jina la Jahazi  modern taarab inayomilikiwa na  mfalme mzee yusuphy inatarajia kutua rasmi jijini Arusha kwa ajili ya kuitambulisha  album mpya inajulikana kwa jina la Mahaba niuee.



Akizungumza na waandishi wa habari muandaaji wa onyesho hilo ambaye ni mkurugenzi wa phide entertainment, Phidesia Mwakitalima alisema kuwa  bendi hiii ya jahazi inatarajiwa kutua jijini Arusha na kufanya onyesho lao December 11  ambapo litafanyika ndani ya ukumbi wa Triple A com lex uliopo ndani ya jiji hili.



Alisema kuwa mpaka sasa utaratibu wote umekamilika na wanangoja tu siku ya onyesho ambapo alieleza kuwa onyesho hili litakuwa rasmi kwa ajili ya kutambulisha albamu mpya ya jahazi pamoja na kutambulisha nyimbo zilizopo katika alibamu hiyo.



Aidha alitaja baadhi ya nyimbo zilizopo katika albamu hiyo na ambazo zitatambulishwa kwa wapenzi wa jahazi modern taarabu kuwa ni pamoja na nyimbo iliyobeba albamu  Mahaba niueee,alibainisha kuwa pamoja na uzinduzi huu hii pia itakuwa  ni sehemu ya ziara yao kufunga mwaka Tanzania nzima kwa bendi hii ya muziki wa Taarabu.



Phidesia aliwasihi wakazi wa mji wa Arusha pamoja na vitongoji vyake wajitokeze kwa wingi kwani wasanii wote ,waimbaji wote wacheza show wote na wake wote wa mzee yusuphy watakuwepo katika onyesho hilo.



Aliwataja baadhi ya wadhamini wa onyesho hilo kuwa ni pamoja na Geo security, kwa udhamini mkubwa wa Geo Security Arusha kampuni  bora ya ulinzi, security power fance na alarm  ambapo alisema na katika siku hiyo ya onyesho  watakuwepo pia kwa ajili ya usalama wa wapenzi wote   kuhakikisha mnarudi salama majumbani salama .

waliotembelea blog