Friday, March 31, 2017


TANGU wafungwe 4-0 na Chelsea huko Stamford Bridge hapo Oktoba 23, Manchester United imekuwa Timu pekee ‘Isiyofungika’ kwenye EPL, Ligi Kuu England, ikimaliza zaidi ya Miezi 5 bila kufungwa zikiwa ni mbio za Mechi 18.

Licha kusakamwa na Mechi kedekede wakiwa Timu pekee wenye Mechi nyingi kupita yeyote huko England, Jose Mourinho ameongoza Kikosi hicho kwa ufanisi mkubwa na kuwawezesha Mwezi Februari kutwa Taji kubwa walipobeba Kombe la Ligi, EFL CUP.
Mwezi Aprili wanakabiliwa na Mechi 9 na ingawa Mourinho amelalamikia ugumu wa Ratiba yao lakini hilo ni dalili tosha ya mafanikio yao Msimu huu wao wa kwanza chini ya Jose Mourinho ambao walikuwemo kwenye mbio za Mashindano Manne na kutolewa tu Wiki 2 zilizopita kwenye FA CUP.

Hilo limempa Mourinho nafasi ya kubadili Kikosi chake katika kila Mashindano na kumwezesha kupata Kikosi imara cha kucheza EPL bila kufungwa.

Related imageMtizame Mchezaji wa Kimataifa wa Armenia, Henrikh Mkhitaryan, ambae kwenye Mechi yake ya kwanza tu Klabuni hapo, walipofungwa na Man City Mwezi Septemba, alitolewa nje lakini hilo halikumkatisha tamaa kwani aliibukia kwenye UEFA EUROPA LIGI na kung’ara na kurudi tena Kikosi cha Kwanza.

Kushiriki Mashindano mengi kumemfanya Mourinho azungushe Wachezaji kwenye kila Mechi ya EUROPA LIGI, EFL CUP na FA CUP lakini kwenye Ligi panga pangua wapo David de Gea; Antonio Valencia, Phil Jones, Marcos Rojo, Matteo Damian; Ander Herrera, Michael Carrick; Henrikh Mkhitaryan/Juan Mata, Paul Pogba, Marcus Rashford; Zlatan Ibrahimovic.

Wafutiliaji wa hizo Mechi zao 18 ambazo hawakufungwa kwenye Ligi wamebaini Man United hufungwa Goli chache, 11 tu, lakini pia kufunga chache, Bao 29 tu.

Hiyo ndiyo sababu kubwa Man United wako Nafasi ya 5 kwenye Ligi wakiwa Pointi 17 nyuma ya Vinara Chelsea.

Kwa ujumla Man United wamefunga Bao 42 katika Mechi 27 za Ligi tofauti na wenzao kama Liverpool waliofunga 62, Chelsea 59, Tottenham Hotspur 55, City 54, Arsenal 56 na Everton 51.

Kitu muhimu kwa Kikosi cha Mourinho kutofungwa Mechi 18 za Ligi ni Difensi yake hasa ule upacha wa Sentahafu ya Marcos Rojo na Phil Jones huku Ander Herrera akiwa nguzo kubwa kwenye Kiungo.

Walipofungwa Mechi yao ya mwisho ya Ligi na Chelsea, upacha wa Sentahafu ulikuwa ni wa Eric Bailly na Chris Smalling na kuumia kwao kukatoa mwanya kwa Rojo-Jones kucheza pamoja na wao ni kati ya Wachezaji 6 waliocheza Mechi nyingi kwenye hizo 18 ambazo hawakufungwa wakifuatia Herrera, Ibrahimovic, Pogba na Kipa De Gea anaeongoza.

Lakini tatizo kubwa ni ufungaji ambao umebaki kwa Zlatan Ibrahimovic pekee aliefunga Jumla ya Mabao 26 Msimu huu na 11 kati ya Mechi 16 za Ligi zilizopita.

Sasa Mwezi Aprili Man United wanakabiliwa na Mechi 9 wakianzia Jumamosi Old Trafford kucheza na West Brom na kisha Jumanne Everton watatua Uwanja huo huo wakati Jumamosi inayofuatia watakuwa safarini Stadium of Light kuivaa Timu ya Mkiani Sunderland inayoongozwa na Meneja wa zamani wa Man United David Moyes.

Mbio hizi za kutofungwa za Mechi 18 za Ligi ndio bora kabisa kwenye Ligi Kuu England tangu Machi 2013 pale Kikosi chini ya Sir Alex Ferguson kilivyofanya hivyo.


VPL, LIGI KUU VODACOM, inarejea tena kwa kishindo Jumamosi hii Aprili Mosi kwa Mechi 3 na kubwa kabisa ni ile itayopigwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kati ya Mabingwa Watetezi Yanga na Timu ngumu Azam FC.
Hakika Mechi hii ni Bigi Mechi na itatoa mwanga mkubwa kama kweli Yanga wanaweza kutetea Ubingwa wao hasa kwa vile wapo Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Simba huku wote wakiwa wamecheza Mechi 24 kila mmoja na kubakiza Mechi 6 tu kila mmoja.

Azam FC wao wapo Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 9 nyuma ya Yanga wakiwa bado wana matumaini finyu ya Ubingwa.

Mechi nyingine za hiyo Jumamosi, ambazo hasa nyingi ni vita za kutoshuka Daraja, ni huko Songea kati ya Maji Maji FC na Toto Africans wakati nyingine ni Mjini Mbeya kati Mbeya City na Ruvu Shooting.

Jumapili zipo Mechi 4 na Macho Kodo ni huko Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba kati ya Kagera Sugar, walio Nafasi ya 4, wakiwavaa Vinara Simba.

Nyingine za Jumapili ni Jijini Dar es Salaam kati ya African Lyon na Stand United, Mjini Mbeya ni Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar na huko Mwadui Complex, Shinyanga ni Mwadui FC na JKT Ruvu.

VPL – LIGI KUU VODACOM
Jumamosi Aprili 1

Yanga v Azam FC
Maji Maji FC v Toto Africans
Mbeya City v Ruvu Shooting

Jumapili Aprili 2

Kagera Sugar v Simba
African Lyon v Stand United
Tanzania Prisons v Mtibwa Sugar
Mwadui FC v JKT Ruvu

Jumamosi Aprili 8
Stand United v Tanzania Prisons
Kagera Sugar v JKT Ruvu
Yanga v Toto Africans
Mtibwa Sugar v Azam FC

Jumapili Aprili 9
Mbeya City v Ndanda FC
Maji Maji FC v African Lyon

Jumatatu Aprili 10
Mbao FC v Simba

Kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea Man United ya England Juan Mata jina lake limerudi kwenye headlines baada ya kufanyiwa upasuaji wa groin, Mata ambaye mwanzoni mwa wiki hii alikuwa akilalamika mazoezini kuwa anasumbuliwa na groin amefanyiwa upasuaji.
Taarifa zilizotoka usiku wa March 31 2017 kuhusu kiungo huyo ni kuwa upasuaji wake umeenda salama lakini kutokana na tatizo lake, kuna uwezekano mkubwa wa kukosa mechi zote za kumalizika za Man United tofauti na awali alivyotazamiwa kuwa anaweza kukosa mechi tatu tu.

Juan Mata ambaye alijiunga na Man United akitokea Chelsea mwaka 2014 , hajawahi kukosa mechi za Man United katika kipindi cha miaka yote mitatu aliyokuwepo klabuni hapo pasipokuwa na majeruhi, mara zote amekuwa akikosekana kwa sababu za msingi ikiwemo majeruhi.

Wednesday, March 22, 2017


Sir Alex Ferguson atarudi tena Old Trafford kwenye Benchi wakati wa Mechi ya Kumtukuza Kiungo wa Manchester United Michael Carrick kwa Utumishi Ulitukuka wa muda mrefu Klabuni hapo.
Ferguson, aliestaafu Umeneja Mwaka 2013 baada ya kuitumikia Man United kwa Miaka 27, ataongoza moja ya Timu katika Mechi hiyo Maalum.
Timu atakayoongoza Sir Alex Ferguson itaitwa Manchester United 2008 XI na itaundwa na Wachezaji waliotwaa Ubingwa wa England na UEFA CHAMPIONS LIGI Mwaka 2008 wakiwa chini yake.
Timu hiyo itacheza na Timu itakayoitwa Michael Carrick All-Star XI ikiongozwa na aliewahi kuwa mmoja wa Mameneja wa Michael Carrick, Harry Redknapp.

Carrick, mwenye Miaka 35 na ambae amedumu Man United kwa Miaka 11 hadi sasa, ameelezea kurejea kwa Sir Alex Ferguson: “Ni heshima kubwa kurejea kwake na kuwa sehemu ya hiyo Gemu. Yeye pengine ndio sababu pekee nilijiunga na Man United, sina uwezo kumshukuru inavyostahili!”

Miongoni mwa Majina makubwa ya Wachezaji Soka watakaoshiriki Mechi hiyo maalum ni Edwin van der Sar, Gary Neville, Rio Ferdinand, Paul Scholes na Ryan Giggs wakiichezea Man United na upande wa Michael Carrick All-Star XI watakuwemo Steven Gerrard, Frank Lampard na Michael Owen.
Ferguson was manager at United for 27 years between 1986 and 2013Ferguson amekuwa Meneja wa United kwa miaka 27 kwenye miaka ya 1986 na 2013

Friday, March 17, 2017


Juan Mata(kushoto) akipongezwa na wenzake kwa bao lake la pekee katika mchezo huo wa marudiano.Juan Mata helped Manchester United move into the last eight of the Europa League.cha pili dakika ya 70 Juan Mata aliwafungia Man United bao na kubadilisha matokeo ya awali na kuwa (2-1 kwenye Agg.) Hku katika Mchezo huo wa raundi ya 16 Man United wakimbadilisha Paul Pogba dakika ya 48 aliyeumia na kuondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Fellaini. Manchester United pia walimbadilisha Beki Blind dakika ya 64 na kumuingiza Jones. Pia katika mchezo huo Zlatan alicheza vyema kipindi cha kwanza na kidogo afunge aligonga mwamba.Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Man Unied 0 Rostov 0.

Monday, March 6, 2017


Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes jana amewanoa wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) katika siku yake ya kwanza nchini katika kuadhimisha miaka 100 ya benki ya standard Chartered tangu kuanzishwa kwake.
“Ni muhimu sana kwa kuwafundisha vijana wadogo soka katika umri huo ni wito kwa viongozi wa soka hapa Tanzania na wadau wote wa michezo kuweka nguvu zao za kutosha kwa vijana maana ni tegemeo la siku za usoni,
“Ni muhimu kama taifa kuwekeza kwa vijana kuwaweka mazingira na miundombinu ya kutosha kabisa ili kuweza kuinua vipaji vyao vya soka na ndio staili inayotumiwa na mataifa yaliopiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya mpira wa miguu,” amesema Barnes.

Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes akizungumza jambo na walimu wa viwanja vya JK Youth Park mara baada ya kuwasili uwanjani hapo kwa ajili ya kuifunda timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) akiwa kwenye ziara ya siku tatu nchini. Katika siku yake ya tatu (leo) nchini gwiji huyo wa soka atashuhudia fainali ya timu tatu kutoka nchini za Tanzania, Uganda na Kenya ambao watapambana vikali kuwania kombe la Standard Chartered 2017 safari ya kuelekea Anfield mjini Liverpool nchini Uingereza.
Barnes amesistiza muhimu wa kuwafunda vijana wadogo wakiwa katika umri mdogo kabisa kama njia bora ya kuwaandaa kuwa wachezaji bora siku za usoni na kuwa tegemeo katika nchini yao.
Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Masoko wa Benki hiyo, Bi Juanita Mramba amesema kwamba Azania Group of Companies kutoka Tanzania, Capital Fm-Kenya na Coca Cola ya Uganda watamenyana vikali kwenye fainali hizo kesho kwenye viwanja vya Jk Youth Park, Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
“Tumeweza kumleta John Barnes kushiriki kwenye mazoezi ya vijana chini ya miaka 15 kwa ajili ya kuwaanda kwenye mashindano ya AFCON ya vijana mwakani, lakini pia amekuja kwa ajili ya tukio la benki hiyo kutimiza miaka 100 tangu kuanza shughuli zake mwaka 1917 za kibenki nchini,” amesema Mramba.
 

Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akizungumza machache na timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) kabla ya kuelekea uwanjani kuwafunda kwa vitendo katika viwanja vya JK Youth Park, Gerezani, jijini Dar es Salaam. Aliongeza kwamba takribani timu 32 zilishiriki kwenye mashindano ya awali ya kutafuta mwakilishi wa Tanzania katika fainali zitakazofanyika kesho na timu mbili kutoka Uganda na Kenya.
Mramba alifafanua kwamba gwiji huyo wa soka aliyetamba miaka ya 1990 atakuwa nchini kwa siku tatu na kushiriki kwenye program ya kuwafundisha vijana wa umri chini ya miaka 15 kuwapa mbinu za soka tangu wakiwa vijana wadogo.
Kwa upande wake, Msemaji wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Bw Alfred Lucas amesema kwamba hii ni fursa adimu kwa vijana kupata nafasi ya kufundishwa soka na mmoja wa magwiji wa soka wa dunia.
“Hii ni nafasi yao muhimu sana katika kujifunza mambo ya soka na kupanua uelewa wao kuhusu mpira wa miguu wakiwa bado vijana wadogo kabisa maana ni mastaa wa taifa wa baadaye,” alisema.

Aidha, kocha wa timu ya Serengeti Boys, Kim Poulsen aliwashukuru benki ya Standard Chartered kwa kufanikisha ujio wa gwiji hilo la soka kuja kushiriki kwenye mazoezi na kutoa mchango wa mafunzo kwa vijana wake.
Aliongeza kwamba ni muhimu kwa wadau wengine wa michezo kuiga mfano wa benki hiyo na kuweza kuwaleta magwiji wa soka duniani kama chachu ya maendeleo ya soka kwa nchini zinazoendelea kama Tanzania.
Gwiji hilo la soka kutoka klabu ya Liverpool anatarajiwa kuondoka leo jioni baada ya fainali hizo kwenye viwanja vya JK Youth Park mjini Dar es Salaam.

Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kuwawekea mazingira na miundombinu ya kutosha watoto ili kuweza kuinua maendeleo ya soka nchini.

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa kuendelea kuweka mazingira mazuri kwenye soka la watoto chini ya umri wa miaka 15 kama njia bora ya kukuza vipaji nchini wakati wa kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji wa Soka wa timu ya Liverpool, John Barnes katika viwanja vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa John Barnes na umuhimu wa kuinua vipaji kwa watoto chini ya miaka 15.

Pichani juu na chini ni John Barnes akiwapa mbinu mbalimbali wakati wa mazoezi kwa watoto chini ya umri wa miaka 15 (Serengeti Boys) baada ya kupata fursa ya kuwepo nchini kushuhudia fainali za mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 safari ya kuelekea Anfield katika kuadhimisha miaka 100 tangu benki ya hiyo kuanzishwa nchini yatakayofanyika leo katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) wakitoana jasho baada ya kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji wa soka wa timu ya Liverpool, John Barnes (hayupo pichani) katika viwanja vya JK Youth Park, jijini Dar es Salaam.
Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa wateja wa benki ya Standard Chartered waliopata nafasi ya kukutana na gwiji huyo katika viwanja vya JK Youth Park.

waliotembelea blog