Saturday, July 12, 2014


434489_heroa
Bado mabishano ya kuwalinganisha yataendelea bila kujali nini kitatokea kesho jumapili, vinginevyo Messi anamaliza maisha yake ya soka kwa kutwaa kombe la dunia, hapo sasa atawashawishi wengi kuwa mkali kama  Maradano na Pele.
WAKATI umewadia. Mara nyingi kumekuwepo na mjadala wa nani mkali kati ya Diego Maradona na Lionel Messi. Wengi wanasema Messi hajashinda kombe la dunia, lakini jumapili ya kesho nahodha huyo wa Argentina anaweza kumaliza kila kitu.
Nyota huyo mwenye miaka 27 itasimama kwa dakika 90 tu zitakazoweza kumfanya kuwa mchezaji mkubwa zaidi duniania ambaye ameweka kila aina ya rekodi, makombe, magoli na vinginevyo. Mfungaji huyo wa muda wote wa Barcelona akiwa na mabao 354, Messi ameshinda makombe 21 akiwa na wakatalunya, ni mchezaji pekee katika historia kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia (Ballons d`Or)  mara nne mfululizo na pia aliongeza medali ya dhahabu ya Olympic na kombe la dunia la vijana chini ya miaka 20 akiwa na  jezi za taifa lake. Kuna kitu kimoja tu kinakosekana.
Kama alama ya taifa, Maradano aliiongoza Argentina mwaka 1986, naye Messi anacheza fainali yake ya kwanza ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani. 
 Bado watu wanabishana kuwalinganisha wakali hao kwa kuangalia utaifa wao, staili moja ya uchezaji na magoli mengi waliyofunga, lakini kiukweli, Messi amepata mafanikio makubwa zaidi ya kocha huyo wa zamani wa Argentina kwa ngazi ya klabu hasa unapoangalia magoli na makombe.

Maafisa wa usalama nchini Brazil

Afisa mmoja mwandamizi nchini Brazil Jose Mariano Beltrame amesema kuwa mji wa Rio de Jeneiro unajiandaa kuweka usalama wa hali ya juu katika historia ya fainali ya kombe la dunia kati ya Argentina na Ujerumani siku ya jumapili.
Zaidi ya maafisa elfu ishirini na tano wa polisi,maafisa wa zima moto,pamoja na majeshi yatashirikishwa katika hatua hiyo.
Rais wa Brazil Dilma Roussef anatarajiwa kuhudhuria fainali hizo katika uwanja wa Maracana akiandamana na marais wengine tisa akiwemo rais Vladmir Putin wa Urusi na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.
Meli ishirini na tano zitakuwa zinapiga doria katika pwani ya mji huo.
Usalama vilevile utaimarishwa katika maeneo ambayo maelfu ya raia wa Argentina wanapiga kambi.

KAGERA SUGAR: TUMEGONGA MWAMBA KUPATA MBADALA WA THEM FELIX `MNYAMA`, LAKINI TUMENASA VIJANA CHIPUKIZI Kitaifa

ded5f-kagera-sugar1
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WAKATA miwa wa Kaitaba, Kagera Sugar, rasmi wameanza kambi kujiwinda na mikikimikiki ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Murage Kabange amezugumza na Mtandao huu na kufafanua kuwa jana walifika Bukoba kambini na leo hii ndio wameanza kusaka kasi mpya kuelekea msimu mpya.
“Mungu ametusaidia tumefika Bukoba kambini jana, kwahiyo leo tumeanza kambi yetu rasmi kujiwinda na ligi kuu”. Alisema Kabange.
Kabange aliongeza kuwa kusogezwa mbele kwa michuano ya ligi kuu ni faraja kwao kwani watapata muda mzuri wa kukijenga kikosi chao kilichosheheni vijana wapya.
“Ni kweli ligi imesogezwa mpaka septemba 20, kwa upande mwingine ni nafuu kwetu ili tuweze kujipangga vizuri”.
“kama unavyojua, tuna vijana wengi wapya, kwahiyo naona kwetu inakuwa  faraja, tutaweza kuwaweka pamoja wachezaji wapya na wa zamani. Tunashukuru kwa kuweza kupata muda huu ulioongezwa”. Aliongeza Kabange.
Kuhusu matatizo ya kikosi chao msimu uliopita ambao walishika nafasi ya tano kwa kujikusanyia pointi 38, Kabange alisema: “Sisi tulikuwa na usumbufu zaidi katika safu ya ushambuliaji, kama ulivyo wimbo wa Taifa Tanzania, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu kuchukua vijana chipukizi ambao wanaweza kutusaidia kama tulivyowatengeneza”.
“Them Felix `Mnyama` ameondoka kuelekea Mbeya City fc,  tulikuwa na mpango na kocha wangu kuchukua mshambuliaji kutoka Uganda, lakini mipango hiyo imeshindikana. Kwahiyo wachezaji tuliowasajili ni Watanzania watupu na naamini tukifanya nao mazoezi tunaweza kufika pale tulipokusudia”. Alifafanua Kabange
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=3398#sthash.GI6nBXh0.dpuf


 

ded5f-kagera-sugar1
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WAKATA miwa wa Kaitaba, Kagera Sugar, rasmi wameanza kambi kujiwinda na mikikimikiki ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Murage Kabange amezugumza na Mtandao huu na kufafanua kuwa jana walifika Bukoba kambini na leo hii ndio wameanza kusaka kasi mpya kuelekea msimu mpya.
“Mungu ametusaidia tumefika Bukoba kambini jana, kwahiyo leo tumeanza kambi yetu rasmi kujiwinda na ligi kuu”. Alisema Kabange.
Kabange aliongeza kuwa kusogezwa mbele kwa michuano ya ligi kuu ni faraja kwao kwani watapata muda mzuri wa kukijenga kikosi chao kilichosheheni vijana wapya.
“Ni kweli ligi imesogezwa mpaka septemba 20, kwa upande mwingine ni nafuu kwetu ili tuweze kujipangga vizuri”.
“kama unavyojua, tuna vijana wengi wapya, kwahiyo naona kwetu inakuwa  faraja, tutaweza kuwaweka pamoja wachezaji wapya na wa zamani. Tunashukuru kwa kuweza kupata muda huu ulioongezwa”. Aliongeza Kabange.
Kuhusu matatizo ya kikosi chao msimu uliopita ambao walishika nafasi ya tano kwa kujikusanyia pointi 38, Kabange alisema: “Sisi tulikuwa na usumbufu zaidi katika safu ya ushambuliaji, kama ulivyo wimbo wa Taifa Tanzania, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu kuchukua vijana chipukizi ambao wanaweza kutusaidia kama tulivyowatengeneza”.
“Them Felix `Mnyama` ameondoka kuelekea Mbeya City fc,  tulikuwa na mpango na kocha wangu kuchukua mshambuliaji kutoka Uganda, lakini mipango hiyo imeshindikana. Kwahiyo wachezaji tuliowasajili ni Watanzania watupu na naamini tukifanya nao mazoezi tunaweza kufika pale tulipokusudia”. Alifafanua Kabange.


Diamond Platinumz alipokewa kwa shangwe jana (July 10) katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere na wadau mbalimbali wa muziki na mashabiki wake akitokea Marekani alikoenda kushiriki katika tuzo za BET.
 
Wema Abraham Sepetu alifika pia katika uwanja huo kumpokea asali wake wa Moyo na alipata nafasi ya kuzungumza na Fadhili Haule, mtangazaji wa kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm aliyetaka kupata maoni yake kuhusu video mbili mpya za Diamond zilizotoka hivi karibuni ‘MdogoMdogo na Bum Bum aliyomshirikisha Iyanya’.
 
Wema alifunguka huku akiweka akilini kuwa anamzungumzia asali wake wa moyo hivyo lugha na points zote alizitumia vyema.
 
“Well, honestly nimeipokea vizuri. Kitu chochote anachokifanya mpenzi lazima utakiona kizuri hata kama ni kafanya kibaya utakiona kizuri tu. Kwa hiyo amejitahidi, he is on another level na huwezi kumfananisha na msanii yoyote Tanzania na haangushi mashabiki wake. Unachokitegemea anafanya zaidi” Amesema.
 
Ameeleza kuwa kwenye video ya MdogoMdogo alifanya kitu tofauti na watu walichokuwa wanategemea kwa jinsi wanavyomfahamu Diamond na mitindo yake.
 
“Watu walikuwa wanategemea kuwa video itakuwa…labda ataenda uswahilini sijui nini, lakini yeye kaifanya very international and nimeipenda the fact kwamba kuna uinternational lakini pia kuna uafrika ndani yake, so it’s nice.”
 
“Bum Bum, it’s nice. Like Bum Bum imeenda sana International like soko la nje sanasana. Na ndio maana hamjaona akirelease audio yake. And the video…yaani everything is nice, siwezi kum-criticize baby wangu.” Ameeleza Wema Sepetu.
 
Katika hatua nyingine, Wema ambaye ameahidi kuwa pamoja na Diamond katika yote amesema tayari ameshazungumza nae kuhusu hatua aliyoifanya ya kumkutanisha na waigizaji wa kimataifa na mashabiki wao wakae mkao wa kupokea kitu kikubwa katika tasnia ya filamu.


Liverpool imethibitisha kwamba wamekubali kumuuza Straika wao Luis Suarez kwa Barcelona.
Wiki ijayo Suarez atasafiri kwenda Barcelona kupimwa Afya yake na kusaini Mkataba wa Miaka Mitano.
Hivi sasa Suarez yupo kwenye Kifungo cha Miezi Minne alichopewa na FIFA baada kumuuma Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini wakati wa Mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italy huko Brazil hapo Juni 26.

Tanga mwanzoni mwa Msimu uliopita Suarez amekuwa akitaka kuihama Liverpool na Mwaka Jana bado kidogo ahamie Arsenal ambao walitoa Ofa ya Pauni Milioni 40 na Pauni Moja juu ili kumnunua lakini walikataliwa.
Baada ya hapo Suarez akasaini Mkataba mpya wa muda mrefu na Liverpool na kuifungia Bao 30 kwenye Ligi Kuu England na kuibuka Mchezaji Bora wa Mwaka baada kuteuliwa na PFA, Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa huko England, na FWA, Chama cha Wanahabari wa Soka, pia cha England.
Inaaminika Barcelona wameafiki kulipa Dau la Pauni Milioni 75 ambalo ndio lipo kwenye Kipengele cha Mkataba wa Suarez na Liverpool ikiwa atataka kuhama kabla Mkataba wake kumalizika.
Ikithibitisha kuhama kwa Suarez, taarifa ya Liverpool ilisema: “Liverpool FC inathibitisha Luis Suarez ataondoka Klabuni baada kufikia makubaliano ya Uhamisho na FC Barcelona. Mchezaji sasa yupo huru kukamilisha taratibu za Uhamisho.”

If the shirt fits: Barcelona staff have already got on the job of printing Suarez's No 9 shirtsKwa upande wake, Suarez alitoa shukrani kwa Klabu na Mashabiki wake ambao amewataka kuelewa uamuzi wake. 

waliotembelea blog