Wednesday, October 28, 2015



 Said Ndemla akiwatoka wachezaji wa Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo ambapo katika mchezoa huo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Hamis Kiiza. (Picha na Francis Dande)
 Peter Mwalyanzi wa Simba akienda chini. 
 Timu zikiingia uwanjani.
 Timu za Coastal union na Simba zikiingia uwanjani.
Kikosi cha Simba. 
Benchi la ufundi la Simba. 
 Benchi la ufundi la Coastal Union
 Kikosi cha Coastal Union.
 Wachezaji wa Simba wakishangilia bao pekee lililofungwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Hamis Kiiza (katikati) dhidi ya Coastal Union ya Tanga wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Mshambuliaji wa Simba, Mwinyi Kazimoto, akimtoka mchezaji wa Coastal Union ya Tanga, Ibrahim Twaha katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
LEO Manchester United wako kwao Old Trafford kucheza Mechi ya Raundi ya 4 ya Kombe la Ligi, Capital One Cup, dhidi ya Middlesbrough ambayo ipo Daraja la chini la Championship.
Baada ya kutoka Sare na CSKA Moscow, kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI na Manchester City, kwenye Ligi Kuu England, Man United Leo wanapambana na Boro kwa mara ya kwanza tangu Msimu wa Ligi Kuu England wa 2008/09 wakati Boro iliposhushwa Daraja.
Wakati Man United inatoka kwenye Sare, Boro wanatoka Mechi yao ya Ligi ambayo waliichapa Wolves 3-1 baada ya kuwa nyuma kwa Bao 1-0 na kushika Nafasi ya 4 katika Daraja la Championship.
Kwenye Mechi hii, Man United itawakosa Majeruhi Antonio Valencia, Luke Shaw and Paddy McNair, Ashley Young na James Wilson lakini ipo nafasi kubwa kwa Chipukizi kutoka Brazil, Andreas Pereira, akacheza hasa baada ya kuchezeshwa na kufunga Bao katika Mechi ya Raundi iliyopita ya Mashindano haya dhidi ya Ipswich Town.
Nae Meneja wa Boro, Aitor Karanka, amedokeza huenda akapumzisha Wachezaji wake kadhaa ili kutilia mkazo kwenye Ligi yao wakawania kupanda Daraja kurudi Ligi Kuu England.
Lakini, huenda Boro wakamtumia mkongwe Stewart Downing, ambae aliwahi kuichezea England, hasa baada ya Jumamosi kufunga Bao safi la Friki walipoichapa Wolves.
Refa wa Mechi hii atakuwa Lee Mason.

Capital One Cup
Raundi ya 4
Saa 10:45 Usiku
Jumanne Oktoba 27

Liverpool v Bournemouth
Manchester City v Crystal Palace
Southampton v Aston Villa
23:00 Manchester United v Middlesbrough
Kikosi cha Man United kinaweza kuwa hivi:



Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi cha wachezaji 28 watakoingia kambini Jumapili jioni kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria Novemba 14 jijini Dar es salaam, na marudiano kufanyika Novemba 17 nchini Algeria.
Akiongea na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Mkwasa amesema kikosi chake hicho kitaweka kambi nchini Omani kwa takribani siku 10 kujiandaa na mchezo kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018 dhidi ya Algeria.
Katika kikosi hicho, Mkwasa amewaita wachezaji wapya sita wakiwemo Salim Mbonde, Jonas Mkude, Salum Abubakar, Elias Maguri, Ramadhani Kessy na Malimi Busungu na kufanya idadi ya wachezaji 28.
Wachezaji aliowaita ni Magolikipa ni Ally Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi wa pembeni Kessy Ramadhani, Mohamed Hussein (Simba), Juma Abdul, Haji Mwinyi (Yanga) na Shomari Kapombe (Azam), Walinzi wa kati ni Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub (Yanga).
Viungo ni Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar, Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank Domayo (Azam), Jonas Mkude na Said Ndemla (Simba), washambuliaji wa pembeni Farid Musa (Azam), Saimon Msuva (Yanga) na Mrisho Ngasa (Free State Stars – Afrika Kusini).
Washambuliaji wa kati ni John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – Congo DR).(P.T)


Loic Remy akiisaidia Chelsea kusawazisha kwa kufanya 1-1 na mtanange kwenda dakika 1201-0 Jonathan Walters akiifunga Chelsea dakika ya 52 kipindi cha pili, katika dakika za majeruhi Loic Remy ameisawazishia Chelsea bao na kufanya 1-1 na mpira kwendelea katika dakika za ziada 30 kwenye Uwanja wa Britannia Stadium huku Stoke wakiwa pungufu 10 uwanjani baada ya mwenzao Phillip Bardsley kupata kadi nyekundu dakika ya 90.Hali tete!!Diego Costa aumia na kutolewa nje
VIKOSI:
Chelsea starting XI

Begovic, Zouma, Cahill, Terry, Baba, Ramires, Mikel, Willian, Oscar, Hazard, Diego Costa.
Stoke City starting XI

Stoke City starting XI
Butland, Bardsley, Shawcross, Wollscheid, Muniesa, Whelan, Adam, Afellay, Arnautovic, Diouf, Walters.


Joao alipofanya 2-03-0Ushindi!!3-0!!!Raha tupu kwa Meneja wa SheffiedMeneja wa Arsenal, Arsene Wenger akichanganyikiwa kwa kichapoShangwe kwa MashabikiSheffield Wednesday 3, Arsenal 0. Sam Hutchinson anaiwezesha timu yake bao la tatu kipindi cha pili dakika ya 51 na kuwafanya Arsenal waduwae na kujiuliza kwenye uwanja wa Hillsborough, EnglandRoss Wallace wa (Sheffield Wednesday) anaipatia bao la kuongoza katika dakika ya 27, Dakika ya 40 Lucas João alipachika bao la pili kwa kichwa mpira ukipigwa kwa kona na kupeana pasi kisha na kupiga kwa juu na Joao kufunga bao na kufanya 2-0 dhidi ya Arsenal. Nyumba imeungua!!Raha ya bao!!Kipa wa Arsenal Petr CechNi shida!Wachezaji wawili wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain na Theo Walcott wameumia na kulazimika kutolewa nje mapema kipindi cha kwanza na timu ya Sheffied kupata mwanya wa kupata bao.Theo nae yale yale!!VIKOSI:
Arsenal starting XI

Cech, Debuchy, Chambers, Mertesacker, Gibbs, Flamini, Kamara, Oxlade-Chamberlain, Campbell, Iwobi, Giroud.

waliotembelea blog