Saturday, August 16, 2014


KIUNGO wa Argentina Javier Mascherano amekubali kusaini Mkataba mpya na Klabu yake Barcelona utakaomweka huko Nou Camp hadi Mwaka 2018.
Habari hizi zimetangazwa na Klabu ya Barcelona hii Leo na pia wamethibitisha Mchezaji huyo amesharudi Mazoezini baada ya kupewa muda zaidi wa kupumzika kufuatia Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil ambapo Argentina ilifungwa 1-0 na Germany kwenye Fainali Julai 13.
Imedokezwa kuwa ndani ya Mkataba huu mpya wa Mascherano kipo Kipengele kinachotaka ilipwe Euro Milioni 100 ikiwa atatakiwa kuhama kabla Mkataba wake kumalizika.
Mascherano ameichezea Barcelona Mechi 184 tangu ahamie hapo kutoka Liverpool Agosti 2010.

Mara nyingi Barcelona imekuwa ikimtumia kama Sentahafu licha ya yeye kuwa Kiungo mahiri kutokana na Barcelona kuwa na mapengo kwenye safu yao ya Difensi kutokana na majeruhi na kukosa Wachezaji wa Akiba wazuri wa nafasi hiyo.



LIGI kuu soka nchini England siku zote haina adabu kabisa!.
Kocha mpya wa Manchester United , Mholanzi, Louis van Gaal amekaribishwa na kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Swansea City ndani ya dimba la Old Trafford.
Hii ni mara ya kwanza kwa Man United kupoteza mechi ya ufunguzi wa msimu katika uwanja wake wa Old Trafford.
Swansea City walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 28 kupitia kwa Ki Sung-yueng.
Mshambuliaji na nahodha wa Man United, Wayne Mark Rooney aliisawazishia timu yake bao hilo katika dakika ya 53 baada ya kupiga tikitaka mpira wa kona uliochongwa na Juan Mata.
 Gylfi Sigurdsson ndiye aliibuka shujaa wa kuifungia bao la ushindi Swansea katika dakika ya 72 na kukalia usukani wa ligi kuu kwa saa kadhaa.
Baada ya kumalizika kwa mechi hiyo pointi za muhimu alizozungumza Van Gaal ni:
-Sio kwamba safu ya ulinzi ndio inatakiwa kuboreshwa bali ni timu nzima.
-Amesema hatapaniki kwasababu ya Man United kupoteza.
-Atawapa nafasi zaidi wachezaji kumpatia ushindi.

Kikosi cha Manchester United: De Gea, Jones, Smalling, Blackett, Lingard (Januzaj), Fletcher, Herrera, Young, Mata, Rooney (c), Hernandez (Nani)

Wachezaji wa akiba: Amos, James, M Keane, Fellaini, Kagawa

Kikosi cha Swansea: FabiaÅ„ski; Rangel, Williams, Amat, Taylor, Ki, Shelvey, Dyer, Sigurðsson, Routledge, Bony (Gomis)

Wachezaji wa akiba: Tremmel, Bartley, Richards, Tiendalli, Montero, Sheehan.

01 (5) 
Msanii wa kundi kijulikanacho kama International, Moses Nyama akiwaongoza wenzake wakati wa onyesho la Serengeti fiesta 2014, lililofanyika jana jioni Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba. Tamasha hilo linadhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya  Serengeti Premium Lager.
02 (4) 
Msanii wa bongo fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz‘, akiwapa mkono baadhi ya mashabiki wake katika tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana jioni. Tamasha hilo  linadhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya  Serengeti Premium Lager.
03 (4)  
Msanii maarufu wa nyimbo za asili, Saida Karoli, akilitawala jukwaa wakati wa onyesho la Serengeti fiesta lililofanyika katika Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba jana jioni. Tamasha hilo  linadhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya  Serengeti Premium Lager.
04 (4) 
Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi. Khamis Kagasheki (kulia), akimpongeza mmoja wa wasanii walioshinda katika Mashindo yaliyojulikana kama dansi la Serengeti fiesta 2014, Joylen Hamis, wakati wa tamasha la serengeti fiesta kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana jioni. Wa pili ni Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney. Tamasha hilo  linadhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya  Serengeti Premium Lager.
05 (2) 
Msanii wa muziki wa bongo fleva , Barnaba boy akifanya vitu katika onesho la Serengeti fiesta katika uwanja wa kaitaba mjini Bukoba jana jioni.Tamasha hilo  linadhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya  Serengeti Premium Lager.
06 
Umati wa wakazi wa mji wa Bukoba na maeneo ya jirani wakishangilia wakati wasanii wakongwe wa miondoko ya kiasili na kizazi kipya wakitoa burudani katika tamasha la Serengeti fiesta lililofanyika katika Uwanja wa Kaitaba, mjini humo jana jioni. Tamasha hilo  linadhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya  Serengeti Premium Lager.
07 
 Mmoja wa wasanii waliong’ara katika tamasha la Serengeti fiesta lililofanyika juzi, Ney wa Mitego akikonga nyoyo za mashabiki katika tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana jioni.Tamasha hilo  linadhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya  Serengeti Premium Lager.
08 
Msanii wa bongo fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz‘, akiimba katika tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana jioni.Tamasha hilo  linadhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya  Serengeti Premium Lager.
10 
Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney (kulia) akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mama Zipora Pangani wakati wa tamasha la Serengeti fiesta katika uwanja wa kaitaba mjini Bukoba jana jioni. Tamasha hilo linadhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya  Serengeti Premium Lager.

 

Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila akipunga mkono baada ya kutawazwa kuwa malkia wa Kanda ya Kinondoni katika shindano lililoshirikisha wanyange 16 waliokuwa wakiwania tiketi ya  kushiriki shindano la Miss Tanzania 2014. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamia leo. 

Shila ameungana na warembo wengine Camila Cindy John aliyeshika nafasi ya pili na Queenlatifa Hashim aliyeshika nafasi ya tatu ambao kwa pamoja wamepata tiketi ya kuiwakilisha Kanda ya Kinondoni katika mashindano ya taifa ya Miss Tanzania 2014 yanayotaraji kufanyika mapema mwezi Oktoba.
  Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila (klatikati) akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi wa taji hilo na kuwaongoza warembo wengine 15 waliokuwa wakiwania taji hilo. Wengine mshindi wa pili Camila Cindy John (kulia) na mshindi wa tatu Queenlatifa Hasim. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamia leo.
Warembo wakipita jukwaani na kivazi cha ufukweni


 Vazi la ubunifu.

 Hii ndio tano bora kutoka kulia ni Miss Photogenic 2014, Getruda Massawe, Qeenlatifa Hasim, Maria Shila, Doreen Bene na Camila Cindy John.
 Jaji Mkuu wa shindano hilo, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga ambao ndio waandaaji wa Miss Tanzania akitangaza tano bora.
 Warembo wakiwa jukwaani kabla ya kutangazwa 5 bora ya shindano hilo 2014

Jumamosi Agosti 16
14:45 Man United v Swansea [Old Trafford]
17:00 Leicester v Everton [King Power Stadium]
17:00 QPR v Hull [Loftus Road Stadium]
17:00 Stoke v Aston Villa [Britannia Stadium]
17:00 West Brom v Sunderland [The Hawthorns]
17:00 West Ham v Spurs [Boleyn Ground]
19:30 Arsenal v Crystal Palace [Emirates Stadium]

Jumapili Agosti 17
15:30 Liverpool v Southampton [Anfield]
18:00 Newcastle v Man City [St. James' Park]

Jumatatu Agosti 18
22:00 Burnley v Chelsea [Turf Moor]

waliotembelea blog