Friday, February 21, 2014


Nchini Tanzania michuano ya kusaka ubingwa wa ligi kuu ya nchi hiyo inaingia mzunguko wa 19 jumamosi hii kwa mechi tano, zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Bukoba, Morogoro, Tanga na Arusha.
Mabingwa watetezi Yanga watakuwa nyumbani uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kumenyana na Ruvu Shooting ya mkoani Pwani, Nayo Kagera Sugar ya Kaskazini magharibi mwa nchi hiyo inaikaribisha Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mjini Morogoro kutakuwa na mpambano kati ya Mtibwa Sugar na Ashanti United, wakati Coastal Union ya Tanga itaumana na timu ngeni na ngumu katika ligi hiyo-Mbeya City katika mechi itakayopigwa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Kikosi cha maaskari jeshi wa Oljoro JKT watakuwa nyumbani kupambana na Askari wenzao Mgambo Shooting katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta mjini Arusha.
Jumapili hii itakuwa zamu ya mabingwa wa Zamani wa ligi hiyo, Simba watakao umana na JKT Ruvu, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huku Mechi kati ya Azam Fc na Tanzania Prisons ikichezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi
 

David Moyes alimsaini Juan Mata kutoka akiwa na matumaini na mategemeo makubwa. Juan Mata alionekana kama mtu atakayekuja kuleta mageuzi ya kuisadia timu hiyo kuingia hata kwenye Top 4. Hata hivyo hali imekuwa tofauti na matarajio, Manchester United ikishinda mchezo mmoja tu kati ya minne Mata aliyocheza. Moja ya vitu vinavyoachangia matatizo haya ni mbinu za kiufundi, hivyo je inafaa kwa Moyes kuangalia upya mbinu zake ili kupata matokeo mazuri kutoka kwa mchezaji wake wa gharama zaidi - Juan Mata?

Mahala aambapo amekuwa akichezeshwa Mata. 
Baadhi ya watu walihisi Moyes angebadili mfumo kwenda kutumia 4-2-3-1 ili kuweza kupata matokeo mazuri kutoka kwa Wayne Rooney, Mata na Adnan Januzaj nyuma ya mshambuliaji wa mbele Robin van Persie, ingawa hilo halijawezekana mpaka sasa. Mata amekuwa akichezeshwa kama kiungo wa kulia au kushoto. Dhidi ya Arsenal alichezeshwa kama kiungo wa kushoto, ingawa alijaribu kuingia ndani ili kuwa karibu na washambuliaji wawili wa mbele 
matttt
Kama mchoro wa picha unavyoonesha hapo juu, United walikuwa wanacheza na Arsenal inayogombea ubingwa ugenini, lakini hapo juu tunaona Mata alitumia muda mwingi katika maeneo ya ulinzi, akikaa sana nyuma katika eneo la kulinda zaidi lango la timu yake (kutokea kushoto pia). Huu mfumo kwa hakika huwezi kukupa matunda mazuri kutoka Mata ambaye anakuwa bora zaidi anapokuwa na mpira miguuni mwake. Ndio maana haishangazi kuona Mata hakuwa na mchezo mzuri siku hiyo, akitengeneza nafasi mbili tu kwa Van Persie.

Dhidi ya Fulham alicheza vizuri kiasi na kuwa na mpira muda mwingi, ingawa alifanya hivi akicheza kwenye winga ya kulia katika mchezo ambao ulitawaliwa na krosi kutoka kwa wachezaji wa kikosi cha Moyes. Man United ilijaribu kupiga krosi 82, staili ambayo sio tu imepitwa na wakati lakini pia ni staili ambayo ndani yake huwezi kuona ubora wa Juan Mata, ambaye hufanya vizuri kazi yake anapocheza katikati ya mistari ya safu ya ulinzi na kiungo, na sio pembeni.

Mahala kwa kubadilisha
Mata hakufanya vibaya dhidi ya Fulham, alitengeneza nafasi tano za kufunga kwa wachezaji wenzie na katika mechi nne alizocheza ametengeneza jumla ya nafasi 13 (namba ya nafasi alizotengeneza Ashley Young msimu mzima). Lakini angeweza kufanya vizuri zaidi. Dhidi ya Fulham alikuwa na mpira kwa muda mwingi na alikamilisha 96% ya pasi zake zote.
mattttaaaa
Lakini tatizo pekee la hizo pasi zilikuwa katika maeneo ya pembeni, hasa upande wa kulia. Haya sio maeneo ya kupata ubora wa Mata. Mata anahitaji kuchezeshwa kati kati ya safu ya ulinzi ya wapinzania na kiungo, mahala ambapo anaweza kutumia jicho lake la pasi nzuri kwenda kwa washambuliaji. Kama tunavyoona kwenye picha hapo juu, hakuwa na mamalka ya mchezo kwenye eneo hilo.

Wazo la kwanza mbadala na kumuondoa mshambuliaji mmoja na kumchezesha Mata namba 10, jambo litakalomfanya awe na mpira muda mrefu na kuutumia katika maeneo ambayo anataka, sio kurudi nyuma kama ambavyo alivyokuwa akifanya dhidi ya Arsenal. Alicheza kwenye eneo hili katika mchezo pekee wa ushindi wa United katika mechi nne zilizopita - mechi dhdi ya Cardiff, ambapo alitengeneza nafasi nne.

Moyes anaonekana hataki au anasita kuwatumia Januzaj, Mata na Rooney katika kikosi kimoja na Van Persie. Hii inawezakana inatokana kwamba wachezaji wake wote watatu wa zamani wana uwezo wa kuingia ndani nyuma ya mshambuliaji wa kati. Njia pekee ya kufanya mfumo huu kufanya kazi ni kuachana na mfumo wa krosi na kuachia mpira wa pasi zaidi kuelekea ndani utumike zaidi.

Hitimisho
Hivi sasa David Moyes hapati matunda bora ya Juan Mata. Mfumo wa kutumia krosi ambayo Mata anatumika katika winga sio mzuri katika kutaka kupata matunda ya Juan Mata. Mata anahitaji uhuru wa kufanya kazi yake katika maeneo yake ya kati ya uwanja, hasa kwenye eneo la nyuma ya mshambuliaji. Ikiwa Moyes atabadili mfumo kwenda 4-2-3-1 ambao unamfiti Mata, Januzaj na Rooney wakicheza nyuma ya Van Persie. Jambo pekee la kuzingatia ni kuhakikisha mabeki wa pembeni wanakuwa na uwezo wa kutoa msaada mkubwa wakati timu inaposhambuliwa. Moyes hana cha kupoteza hivi sasa - hasa baada ya mfumo wa sasa wa 4-4-2 kutokuwa na matunda kwa timu na kupelekea matokeo mabaya.




Mechi ya pili ya raundi ya kwanza kuwania Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Zambia (Shepolopolo) sasa itachezwa Februari 28 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Twiga Stars tayari ipo kambini kujiandaa kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni. Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage inafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Karume ambao ni wa nyasi za bandia kama ulivyo ule wa Azam Complex.

Shepolopolo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Februari 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.

Iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuiondoa Shepolopolo itacheza na mshindi wa mechi kati ya Botswana na Zimbabwe. Zimbabwe ilishinda mechi ya kwanza ugenini.

Wachezaji wa Twiga Stars waliopo kambini ni Amina Ali, Anastazia Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Everine Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma Mustafa, Fatuma Mwisendi, Fatuma Omari, Flora Kayanda, Happiness Mwaipaja, Maimuna Mkane, Mwajuma Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Pulkeria Charaji, Sherida Boniface, Sophia Mwasikili, Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.



Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 19 kesho (Februari 22 mwaka huu) kwa mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Bukoba, Morogoro, Tanga na Arusha.

Yanga itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting ya mkoani Pwani katika mechi itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Nayo Kagera Sugar inaikaribisha Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Uwanja wa Manungu uliopo Turiani mkoani Morogoro ndiyo utakaotumika kwa mechi kati ya Mtibwa Sugar na Ashanti United, wakati Coastal Union itaumana na Mbeya City katika mechi itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kutoka Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Maafande wa Oljoro JKT watakuwa nyumbani kupambana na Mgambo Shooting katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.

Jumapili (Februari 23 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa ni Simba dhidi ya JKT Ruvu, mechi ambayo pia itaoneshwa moja kwa moja na Azam Tv. Mechi kati ya Azam na Tanzania Prisons iliyokuwa ichezwe kesho (Februari 22 mwaka huu) Uwanja wa Chamazi sasa itachezwa Jumapili (Februari 23 mwaka huu) ambapo na itakuwa ‘live’.

Ligi hiyo itaendelea Jumatano (Februari 26 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Ashanti United na Azam itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex (Chamazi).


Arsene Wenger na Mesut Ozil ya Arsenal

 

Arsenal mbele Mesut Ozil bado hajapata nafuu kutoka tamaa ya adhabu miss ya yake dhidi ya Bayern Munich, kwa mujibu wa meneja Arsenal Wenger.
Ozil, 25, klabu rekodi ya kusainiwa, aliona yake doa-kick kuokolewa katika midweek Ligi ya Mabingwa hasara na kuomba radhi kwa kushindwa   kwa mashabiki katika Picha.
Wenger alisema: "Je, yule alright sasa Hakika si kwa sababu ya masaa 48 ni kidogo mfupi kupata juu ya hilo?."
Arsenal, pili katika Ligi Kuu, mwenyeji wa Sunderland siku ya Jumamosi.Zamani Arsenal kubwa Dennis Bergkamp itakuwa kuheshimiwa wakati sanamu yake ni ilizindua kabla ya mchezo.
Wenger anasema Ozil wanaweza kuchukua kuchukua faraja kutokana na ukweli Dutchman, ambaye alikosa penalti dakika ya mwisho katika Kombe la FA kushindwa kwa Manchester United, aliendelea kuwa favorite mashabiki.
"Tulikuwa na mifano kabla ya kama Bergkamp katika '99 na yeye alikataa kuchukua adhabu yoyote baada ya yake. Yeye anapata sanamu leo," alisema Wenger.
"Adhabu ni sehemu ya jinsi kujisikia na kiasi gani unataka. Kwa sasa tuna basi Ozil kuokoa, ni sehemu ya kazi na kupata zaidi ya tamaa na kuonyesha jinsi gani kujibu."
Wenger anasema mchezaji ni uwezekano wa kuchukua adhabu kama Mikel Arteta, ambaye anarudi kutoka kusimamishwa dhidi ya Sunderland, ni juu ya lami.
Ozil saini na Real Madrid kwa ajili ya £ 42.5m katika Septemba 2013, lakini imekosolewa kwa ajili ya maonyesho ya hivi karibuni na ni bila lengo katika mechi 14.
Arsenal mbia Alisher Usmanov alisema Ujerumani "si kucheza katika uwezo wake" na alitoa mfano wa kuchoka kama sababu iwezekanavyo baada ya kushindwa na Bayern."Nadhani Ozil ni classy mchezaji na juu ya muda mrefu, darasa anaelezea siku zote," alisema Wenger.
"Natamani kwamba siku moja Ozil kupata sanamu nje ya uwanja kama vizuri na mimi bado kuwa nzuri ya kutosha kuja na kuangalia yake."
Adhabu miss ya wake - wakati mechi dhidi ya mabingwa wa Ujerumani alikuwa goalless - imeonekana maamuzi, kama malengo kutoka Toni Kroos na Thomas Muller alitoa upande Pep Guardiola 2-0 faida kabla ya pili mguu tarehe 11 Machi.
"Asubuhi haina kujisikia vizuri aidha," Ozil aliandika juu ya Facebook. "Guys Sorry - haikuwa imepangwa kwa njia hiyo."
Kipa Wojciech Szczesny alitolewa kwa kufungwa adhabu - ambayo pia alikuwa amekosa - mapema katika mechi.
Wenger alithibitisha klabu bila nidhamu 23 mwenye umri wa miaka baada ya yeye alifanya mashambulizi mkono ishara kuondoka wakati lami.



Wanawake Mkuu wa Uingereza kushinda ya Olimpiki curling ya shaba, na jiwe ya mwisho ya mechi yao dhidi ya Uswisi.
timu ya Hawa MUIRHEAD, Vicki Adams, Claire Hamilton na Anna Sloan chuma ushindi 6-5 kushinda kwanza ya Olimpiki medali ya curling Uingereza tangu Rhona Martin ya dhahabu mwaka 2002.
GB ya watu uso Canada kwa dhahabu saa 13:30 GMT siku ya Ijumaa. Medali zao uhakika hufanya haul Uingereza wa nne bora yao katika Michezo ya majira ya baridi katika miaka ya 90.


Sat 22 Feb 2014 - Premier League
Sun 23 Feb 2014 - Premier League
  • Liverpool v Swansea 13:30
  • Newcastle v Aston Villa 13:30
  • Norwich v Tottenham 16:00
Sat 1 Mar 2014 - Premier League
  • Everton v West Ham 15:00
  • Fulham v Chelsea 15:00


Rais Yoweri Museveni wa Uganda atia saini mswada wa sheria dhidi ya picha za ngono.
Ikiwa unaishi Uganda na unapenda kuvaa nguo fupi, zinazokubana bana au zinazoonyesha sehemu za mwili ambazo zaweza kuwafanya watu wa jinsia nyingine kusisimkwa na kutamani kushiriki ngono nawe, basi jua uko taabuni.
Hii ni kwa sababu rais Yoweri Museveni ametia saini mswada dhidi ya picha za ngono ambao unapinga mavazi yasiyo ya heshima haswa yanayovaliwa na wanamziki na picha za watu wakiwa uchi. Mwandishi wetu wa Kampala Leylah Ndinda na taarifa zaidi. Kusikiliza taarifa hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

waliotembelea blog