RAIS MAGUFULI KUENDELEZA JITIHADA ZA MARAIS WALIOPITA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI.
Rais John Magufuli akiwapungia wananchi waliofurika kwenye
uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam wakati alipoingia kwenye uwanja huo
kuongoza sherehe za miaka 55 ya Uhuru Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Rais John Magufuli akikagua
gwaride katika sherehe za miaka 55 ya uhuru kwenye uwanja wa taifa
jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiteta na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika sherehe za
miaka 55 ya uhuru kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Makamu wa Rais, Samia Suluhu
akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kuwasili kwenye
uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuhudhuria sherehe za miaka 55 ya
Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Rais Joh Magufuli akisalimiana na
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Uhuru
jijini Dar es salaam kuongoza sherehe za miaka 55 ya Uhuru jijini Dar es
salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Makomando wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania wakionyesha uwezo wao wa kukabiliana na adui bila
kutumia silaha za moto katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru kwenye
uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Makomando wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania wakionyesha uwezo wao wa kukabiliana na adui bila
kutumia silaha za moto katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru kwenye
uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………..
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO-Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano
itaendeleza jitihada zilizoachwa na Serikali za awamu zilizopita ili
kuzidi kuwaletea maendeleo Watanzania.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es
Salaam wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania
bara yaliyofanyika katika uwanja wa uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli alisema kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano imeanza jitihada za kuboresha huduma za
maendeleo ya jamii, ambapo katika bajeti ya mwaka 2016/17 imeamua
kutenga asilimia 40 ya bajeti katika miradi mbalimbali ya maendeleo
ikiwemo umeme, miundombinu, afya, elimu.
“Mbali na kujiwekea vipaumbele
mbalimbali kwa maendeleo ya nchi, kumekuwa na changamoto kadha wa kadha
zinazozikabili nchi ikiwemo ufisadi, rushwa ndani ya baadhi ya
watendaji” alisema Rais Magfuli
Aidha Rais Magufuli alisema
juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ni kuboresha maslahi kwa
watanzania kwa kuchukua hatua mbalimbali za kuwawajibisha wale wote
wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi.
Akifafanua zaidi Rais Magufuli
aliwataka watanzania kudumisha amani na kulinda muungano uliyopo kwani
amani ni msingi wa maendeleo ya nchi bila amani hakuna maendeleo.
Rais Magufuli pia alitoa wito kwa
wantanzania kuendelea kufanya kazi kiwa bidii kwani kila mwananchi ana
haki ya kufanya kazi, na kusema kuwa waasisi wa nchi walileta uhuru kwa
maendeleo ya nchi kwani Uhuru ni kazi.
“Serikali ya Tanzania imejipanga
kufanya kazi, tutafanya kazi kwelikweli, watendaji niliowachagua
wanafanya kazi hivyo watanzania kwa ujumla mnatakiwa kuonesha
ushirikiano kwao kwa maendeleo ya nchi yetu” alisema Rais Magufuli.
Mbali na hayo Rais Magufuli
alisema kuwa ndani ya miaka 55 ya Uhuru Tanzania imepata mafanikio
makubwa ambapo Tanzania imelinda Uhuru wa nchi, sambamba na kulinda
mipaka iliyopo.