Sunday, July 19, 2015



ini2
Mikakati ya kumpata Rais mpya wa klabu ya Barcelona umeanza kwenye uwanja wa Nou Camp huku nahodha wao Andres Iniesta akiwaongoza wachezaji wa zamani na wa sasa kupiga kura.
ini
Josep Bartomero anapewa nafasi kubwa ya kushinda kiti hicho ndani ya klabu hiyo.
ini3
Wachezaji wa zamani na mahodha wa klabu hiyo kwa nyakati tofauti Carles Puyol na Xavi walikuwa ni miongoni mwa watu waliojitokeza kupiga kura ili kuiweka klabu yao kwenye mikono salama.
ini6
Josep Bartomeu ni mgombea ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa rais wa Barcelona lakini anapata upinzani mkali kutoka Joan Laporta, Austi Benedito pamoja na Toni Freixa.
ini7



Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Wanaccm na Wananchi wa Mkoa wa Geita, Wakati aliposimama kuwasalimia akitokea jijini Mwanza kuelekea Kijijini kwake Chato. Hapa ni Kivukoni Busisi Mkoani hapo, mapema asubuhi ya leo.


Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya Wanaccm na Wananchi wa Mkoa wa Geita, mara baada ya kuwasili mapema leo asubuhi.

Msafara wa Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Geita. PICHA ZOTE NA MICHUZIJR


AZAM FC imeanza vyema michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuwafunga KCCA ya Uganda bao 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mfungaji wa bao hilo la pekee ni  Nahodha, John Raphael Bocco Kipindi cha kwanza na Kipindi cha pili hakuna aliyeziona nyavu za mwenzake.


MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho amemuudhi Meneja mwenzake wa Everton baada ya kutangaza kuwa Chelsea imetoa Ofa ya kumnunua Beki John Stones.
Ofa hiyo ya kumnunua Beki wa Miaka 21 ya Pauni Milioni 20 imekataliwa na Everton.
Akiongea na Sky Sports News, Mourinho alisema: "Tumetoa Ofa kwa sababu tunampenda Beki huyo."
John Stones, ambae ameichezea England mara 4, alinunuliwa na Everton kutoka Barnsley Mwaka 2013 kwa Pauni Milioni 3.
Hata hivyo, kitendo cha Mourinho kutangaza waziwazi Ofa yao kimemkera mno Meneja wa Everton Roberto Martinez ambae alizungumza Jana huko Singapore mara baada ya kufungwa 3-1 na Arsenal kwenye Fainali ya Barclays Asia Trophy.
Martinez alisema: "Inasikitisha kwa Klabu kutamka hadharani. Sidhani kama sisi tunaweza kufanya hivyo na kuzumngumzia kuhusu Mchezaji. Joh Stones ni Mchezaji wa Everton, mwisho!"


Louis van Gaal amekiri Javier Hernandez 'Chicharito' atapata nafasi nyingine ya kupigania nafasi yake kwenye Kikosi cha Manchester United akiungana na Timu hiyo hapo Julai 25 huko Ziarani Marekani.
Chicharito, ambae aliifungia Man United Bao 59 katika Mechi154, alipelekwa kwa Mkopo huko Real Madrid Msimu uliopita baada Van Gaal kuamua atakuwa nyuma ya Wayne Rooney, Robin van Persie na Radamel Falcao katika kupewa namba.

Lakini, baada ya Man United kuifunga Club America 1-0 mapema Leo, Van Gaal aliulizwa hatima ya Chicharito na kueleza: "Chicharito anakuja Julai 25. Ana nafasi ya kudhihirisha uwezo wake hasa baada ya Falcao na Van Persie kuondoka, hivyo nafasi yake kubwa."

Hivi sasa Man United imebakiwa na Mastraika Wawili tu wanaotambulika ambao ni Kepteni Wayne Rooney na James Wilson na alipoulizwa kuhusu upungufu huo, Van Gaal alijibu: "Hapana tunae Rooney anaweza kucheza kama Straika mkuu. Wanahabari wote Msimu uliopita waliandika anapaswa kucheza hapo na mimi nawasikiliza. Na tunae Chicharito, na labda Wilson, na pengine kwa kushangaza..mpya., huu ni mchakato. Sina wasiwasi na nafasi hiyo."


Wachezaji wa Arsenal wakishangilia Ubingwa wao ambao umepatikana kwa kuifunga bao 3-1 EvertonArsenal 3-1 Everton, Mikel Arteta akiwa amebeba Kombe lao leo hiiMikel Arteta akiwa amebeba Kombe leoMesut Ozil ndiye aliyeifungia bao la tatu Arsenal kwa kufanya 3-1 dhidi ya Everton zote za Ligi Kuu EnglandRoss aliipatia bao la pekee EvertonSanti Cazorla kafunga la piliTheo Walcott akishangilia mara baada ya kufunga bao la kwanzaTheo WalcottJack na Tom kwenye kasiGibbs akiruka juu kugombea mpira Kikosi cha ArsenalKikosi cha Everton kilichoanza kikipata picha ya pamoja


Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Gor-Mahia

Mchezaji wa Yanga, Amis Tambwe akiwa chini huku wachezaji Collins Okoth (kulia) na Harun Shakava (kushoto) wa Gor Mahia ya Kenya wakiwania mpira wakati wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Kagame uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Yanga imefungwa mabao 2-1.

Mashabiki wa Yanga

WENYEJI Yanga wameanza vibaya kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada ya kufungwa mabao 2-1 na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa Kundi A kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia Wananchi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi jioni ya leo.
Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake,nje ya ofisi za CCM mkoa,ambao walijotokeza kumlaki kwa shange na furaha kubwa.Dkt Magufuli amewasili leo jijini Mwanza akitokea jijini Dar kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kwa ujumla.

Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi alipokuwa akiwasili jijini Mwanza jioni ya leo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa juu wa chama cha CCM,Magufuli yuko jijini Mwanza kujitambulisha kwa Wananchi.

Mke wa Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi Dkt.John Pombe Magufuli,Mama Janeth Magufuli akiwasalimia Wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake waliojiotokeza kwa wingi kuwapokea,Pichani kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake,nje ya ofisi za CCM mkoa wa Mwanza.



Baadhi ya Wananchi wakilikimbiza gari la Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli kwa shangwe kama waonekanavyo pichani ,wakati Magufuli lipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla jioni ya leo.

Baadhi ya Wananchi wa jiji la Mwanza wakiwa wamefunga barabara kwa muda wakishangilia ujio wa Mgombea Uraisi wa CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla jioni ya leo.

kuna wengine waliacha kazi kwa muda kama hizi na kuja kwenda kushangilia ujio wa Mh.Dkt John Magufuli

Wananchi wa Passians wakimpokea na kumshangila Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla jioni ya leo.

Baadhi ya Wanahabari wakiwa kazini.

Wananchi wa eneo la kona ya Bwiru wakiwa wamezuia msafara wa Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla.

Wananchi wa eneo la kona ya Bwiru wakiwa wamezuia msafara wa Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla.

Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh.Magesse Mulongo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa jiji hilo mapema leo mchana,kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu.

Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mh John Monela mara baada ya katika uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza mapema leo mchana.

Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alisalimiana na wafuasi wa chama hicho wakiwemo viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mwanza,alipowasili katika uwanja wa ndege wa jiji hilo mapema leo mchana.

waliotembelea blog