Waziri
Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (mbele
kulia) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Selestine
Gesimba wakati wa mapokezi yake leo tarehe 28 Desemba 2015 katika ofisi
yake mpya Mpingo House mara baada ya kuapishwa Ikulu mapema asubuhi ya
leo. Nyuma yake kulia ni naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo
Makani na anaeongoza utambulisho katikati yao ni Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru.
Waziri Wizara ya Maliasili
na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akisaini kitabu cha wageni mara tu
baada ya kuingia katika ofisi yake mpya iliyopo Mpingo House mapema leo
tarehe 28 Desemba 2015 baada ya kuapishwa Ikulu na Mhe. Rais Dkt. John
Pombe Magufuli. Wanaoshuhudia kulia ni Naibu Wazari wa Wizara hiyo Mhe.
Eng. Ramo Makani na Katibu Mkuu Dkt. Adelhelm Meru (kushoto).
Waziri Wizara ya Maliasili
na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) na Naibu Waziri Mhe. Eng. Ramo Makani
(kulia) mara baada ya kusaini kitabu cha wageni ofisini kwake mapema leo
tarehe 28 Desemba 2015.
Picha
ya pamoja kati ya Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne
Maghembe (wa pili kulia) na Naibu Waziri wake Mhe. Eng. Ramo Makani (wa
pili kushoto), Katibu Mkuu wa Wziara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (wa kwanza
kulia) na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Selestine Gesimba(kushoto).
Sehemu
ya wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa tayari kwa
mapokezi ya Waziri wao mpya Mhe. Prof. Jumanne Maghembe aliyeapishwa
Ikulu leo na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania Mhe. John Pombe
Magufuli.(Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii)