Tuesday, September 9, 2014


Robin van Persie anaamini Louis van Gaal ataiongoza Manchester United kwenye mafanikio baada ya kukiboresha Kikosi cha Timu yao kwa kununua Masta 6 wapya wenye hadhi ya Kimataifa.
Kwenye Siku ya mwisho ya Dirisha la Uhamisho, Man United iliwanasa Mchezaji wa Kimataifa wa Holland Daley Blind na Supastaa wa Colombia Radamel Falcao ‘El Tigre’ ambao walifuatia kuchukuliwa kwa Mchezali ghali huko Uingereza, Angel Di Maria, Mchezaji wa Kimataifa wa Argentina.

Kabla ya kusainiwa hao, Man United iliwanunua Luke Shaw, Mchezaji wa England, Anders Herrera wa Spain na Beki Kiraka wa Kimataifa kutoka Argentina, Marcos Rojo.
Wachezaji wote hao 6 hawajacheza pamoja tangu wanunuliwe na Jumapili wote wana nafasi kuingia dimbani kuikwaa QPR kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Uwanjani Old Trafford.

Licha ya kuambua Pointi 2 tu kati ya 9 katika Mechi zao 3 za kwanza na kutupwa nje ya Capital One Cup, Robin van Persie hajavunjika nguvu na ana matumaini makubwa na hamu kubwa ya kuungana na Wachezaji hao wapya.
Van Persie, ambae yuko na Kikosi cha Netherlands kinachocheza Mechi ya EURO 2016 dhidi ya Czech Republic, amesema: “Ninangojea kwa hamu kufanya Mazoezi na kucheza na Wachezaji hao wapya wa Kimataifa!”
Aliongeza: “Ile imani kuwa tutafanya vyema imeongezeka maradufu baada ya kuwanunua Wachezaji hawa wapya. Inavutia na kufurahisha sana ujio wa hawa wapya!”
Van Persie alisema: “Kwangu binafsi, ni kitu chema kucheza na Wachezaji bora Duniani!”

Licha ya baadhi ya Wachambuzi kuuponda Mfumo mpya wa Van Gaal wa Fomesheni ya 3-4-1-2 kwamba ndio umechangia kwa Man United kupoteza Pointi na Mechi Msimu huu, Van Persie amesisitiza ni wajibu wa Wachezaji kuufuata au kutupwa nje.

Van Persie ameeleza: “Ni kitu cha wazi na rahisi. Meneja ndie anachagua mbinu. Sisi Wachezaji wajibu wote ni kufuata kile anachotaka Meneja. Sisi ni Wachezaji, tunacheza. Tusijitumbukize kuhoji mbinu!”
Aliongeza: “Nikiwa Kepteni wa Holland nahusishwa kujadili mbinu lakini huwa sipendi kujiingiza. Kama ni 4-3-3 au 3-5-2 hicho si kisingizio cha kufungwa. Lazima tujirekebishe kumfuata Meneja. Hamna njia moja au nyingine katika Soka!”


Worth more? Paul Pogba (right) will earn just £23,000-per-week from his current deal with Juventus
Anataka zaidi? Paul Pogba (kulia) atalipwa paundi elfu 23 kwa wiki kwa wakati huu katika klabu yake ya Juventus

LIGI ya Italia imeshuka umaarufu wake ukilinganisha na ligi nyingine za ulaya na hii inatokana na mishara ya wachezaji wa Seria A iliyotangazwa jumatatu ya wiki hii.
Daniele de Rossi  ndiye mchezaji anayelipwa zaidi ambapo anachukua paundi laki moja kwa wiki na Gonzalo Higuain anamfuatia kwa kulamba paundi elfu 84 kwa wiki na wa tatu ni Carlos Tevez anayepokea paundi elfu 70 kwa wiki. 
Kwa mujibu wa gazeti la Gazzetta dello Sport, klabu za Serie A kwa sasa zinatumia karibia paundi milioni 500 kwa ajili ya malipo ya mishahara wa wachezaji chini ya kiwango cha mwaka 2011 na wachezaji wanaolipwa zaidi wanachukua hela ndogo ukilinganisha na wachezaji nyota wa ligi kuu England na La Liga.
Kwa mfano, Paul Pogba, anapokea paundi elfu 23 kwa wiki msimu huu licha ya kuwa miongoni mwa vijana wenye kiwango cha juu duniani na katika klabu yake ya Juventus.
Juventus, ndio klabu inayoongoza kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya mishara na ni klabu pekee ya Italia ambayo inaongeza mishahara ya wachezaji kutoka 2013/2014 ambapo Carlos Tevez na Arturo Vidal sasa wanapokea zaidi ya paundi elfu 60 kwa wiki.
Nyota wa Roma, Daniele De Rossi ndiye analamba mkwanja mrefu katika mkataba wake wenye thamani ya paundi milioni 5.2 bila kujumuisha posho.
Nyota wa zamani wa Cheslea na sasa Roma  Ashley Cole aliamua kwenda Italia baada ya kutoongezewa mkataba Chelsea na amesaini mkataba atakaomfanya apokee paundi elfu 35 kwa wiki katika kikosi hicho cha Rudi Garcia.
Big money: Former Manchester City striker Carlos Tevez (left) is the top earner at Juventus
Pesa ndefu: Nyota wa zamani wa Manchester City, Carlos Tevez (kushoto) ndiye analipwa zaidi katika klabu ya  Juventus
Love of the game: Ashley Cole (right) has taken a wag cut to join Roma and will earn £35,000-per-week
Mpenda soka: Ashley Cole (kulia) aljiunga na Roma na analamba paundi elfu 35 kwa wiki 

ROMA - Wanaolipwa zaidi

1. Daniele de Rossi - Paundi 100,000-kwa wiki
2. Marco Borriello - Paundi 54,000-kwa wiki
3. Miralem Pjanic - Paundi 49,000-kwa wiki
4. Gervinho - Paundi 45,000-kwa wiki
5. Kevin Strootman - Paundi 43,000-kwa wiki
 
8. Ashley Cole - Paundi 35,000-kwa wiki   

JUVENTUS - Wanaolipwa zaidi

1. Carlos Tevez - Paundi 69,000-per-kwa wiki
2. Gianluigi Buffon - Paundi 61,000-kwa wiki
3. Arturo Vidal - Paundi 61,000-kwa wiki
4. Andrea Pirlo - Paundi 58,000-kwa wiki
5. Fernando Llorente - Paundi 54,000-kwa wiki 
 
15. Paul Pogba - Paundi 23,000-kwa wiki 

'

Money men: United vice-chairman Edward Woodward (centre), Joel Glazer (left) and Richard Arnold (right)
Watu wa hela: Makamu mwenyekiti wa United Edward Woodward (katikati), Joel Glazer (kushoto) na Richard Arnold (kulia)

MANCHESTER wanatarajia kutangaza rekodi ya mapato leo ambayo inakadriwa kufikia paundi milioni 420 kwa msimu uliopita, huku wakipata faida ya paundi milioni 25 kutokana na mauzo ya mamilioni ya jezi duniani kote.
Mapato hayo ya mwaka pia yatahusisha fidia waliyomlipa kocha David Moyes na benchi lake la ufundi, lakini fedha hizo hazitahusisha hasara yoyote waliyoipata baada ya kushindwa kufuzu michuano ya UEFA kwa msimu huu.
Jezi ya heshima Old Trafford: Angel di Maria ndio mchezaji aliyeamua kuvaa jezi ya kipee namba 7 Manchester United
Boost: Di Maria looked impressive on his Manchester United debut and will improve them on and off the pitch
Kaongeza nguvu: Di Maria aliwavutiwa wengi katika mechi yake ya kwanza Manchester United na ataimarika zaidi akiendelea kucheza.

Taarifa zinafafanua kuwa mapato ya jumla yanakadriwa kuwa paundi milioni 429 hadi 432, na ni ongezeko la asilimia 18 hadi 19.


WAKATI Neymar akifurahishwa na uongozi wa Kocha mpya wa Brazil Dunga huku wakijitayarisha kuivaa Ecuador Jumatano huko New Jersey, USA baada ya Ijumaa kuifunga Colombia, Fulbeki Maicon ametimuliwa kwenye Timu hiyo.
Ripoti toka ndani ya Kambi ya Brazil huko Marekani zimedai Maicon, ambae anaichezea AS Roma ya Italy, amefukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu huku Mitandao ikijaa kila aina ya sababu na nyingine kudai ni ngono.
Kwenye Mechi hii ijayo na Ecuador, mbali ya kumkosa Maicon pia Brazil itamkosa Sentahafu David Luiz ambae ana tatizo la Goti lakini Neymar, ambae ndie Nahodha wa Brazil na ambae ndie aliefunga Bao walipoibwaga Colombia 1-0 hapo Ijumaa, ana matumaini makubwa ya ushindi.
Neymar amewaambia Wanahabari kuwa Dunga ana nia na ari ya ushindi na mambo hayo yatamsaidia Kocha huyo alietwaa mikoba ya Brazil kutoka kwa Luiz Felipe Scolari Mwezi Julai.
Nae Dunga amesema ushindi dhidi ya Colombia ambao umekuja mara tu baada ya kubondwa 7-1 na Germany kwenye Fainali ya Kombe la Dunia Mwezi Julai umetoa jibu na kubadili hali ya Timu.
Nao Ecuador wanaingia kwenye Mechi hii na Brazl wakitoka kwenye ushindi wa Bao 4-0 walipoichapa Bolivia huko Fort Lauderdale hapo Jumamosi.

TETESI TATU ZINAZOMZUNGUKA MAICON MPAKA SASA.
1. The first rumour was that Maicon was caught having sexual intercourse with teammate Elias.
2. The second rumour claimed he jerked off into David Luiz’s bottle of shampoo.
3. The third rumour, which originated on satirical Brazilian website Ole do Brasil, claims Maicon spread pepper and milk on Elias’s arse and then told him in the morning that he had been raped by four men.

waliotembelea blog