Tuesday, September 9, 2014


Robin van Persie anaamini Louis van Gaal ataiongoza Manchester United kwenye mafanikio baada ya kukiboresha Kikosi cha Timu yao kwa kununua Masta 6 wapya wenye hadhi ya Kimataifa.
Kwenye Siku ya mwisho ya Dirisha la Uhamisho, Man United iliwanasa Mchezaji wa Kimataifa wa Holland Daley Blind na Supastaa wa Colombia Radamel Falcao ‘El Tigre’ ambao walifuatia kuchukuliwa kwa Mchezali ghali huko Uingereza, Angel Di Maria, Mchezaji wa Kimataifa wa Argentina.

Kabla ya kusainiwa hao, Man United iliwanunua Luke Shaw, Mchezaji wa England, Anders Herrera wa Spain na Beki Kiraka wa Kimataifa kutoka Argentina, Marcos Rojo.
Wachezaji wote hao 6 hawajacheza pamoja tangu wanunuliwe na Jumapili wote wana nafasi kuingia dimbani kuikwaa QPR kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Uwanjani Old Trafford.

Licha ya kuambua Pointi 2 tu kati ya 9 katika Mechi zao 3 za kwanza na kutupwa nje ya Capital One Cup, Robin van Persie hajavunjika nguvu na ana matumaini makubwa na hamu kubwa ya kuungana na Wachezaji hao wapya.
Van Persie, ambae yuko na Kikosi cha Netherlands kinachocheza Mechi ya EURO 2016 dhidi ya Czech Republic, amesema: “Ninangojea kwa hamu kufanya Mazoezi na kucheza na Wachezaji hao wapya wa Kimataifa!”
Aliongeza: “Ile imani kuwa tutafanya vyema imeongezeka maradufu baada ya kuwanunua Wachezaji hawa wapya. Inavutia na kufurahisha sana ujio wa hawa wapya!”
Van Persie alisema: “Kwangu binafsi, ni kitu chema kucheza na Wachezaji bora Duniani!”

Licha ya baadhi ya Wachambuzi kuuponda Mfumo mpya wa Van Gaal wa Fomesheni ya 3-4-1-2 kwamba ndio umechangia kwa Man United kupoteza Pointi na Mechi Msimu huu, Van Persie amesisitiza ni wajibu wa Wachezaji kuufuata au kutupwa nje.

Van Persie ameeleza: “Ni kitu cha wazi na rahisi. Meneja ndie anachagua mbinu. Sisi Wachezaji wajibu wote ni kufuata kile anachotaka Meneja. Sisi ni Wachezaji, tunacheza. Tusijitumbukize kuhoji mbinu!”
Aliongeza: “Nikiwa Kepteni wa Holland nahusishwa kujadili mbinu lakini huwa sipendi kujiingiza. Kama ni 4-3-3 au 3-5-2 hicho si kisingizio cha kufungwa. Lazima tujirekebishe kumfuata Meneja. Hamna njia moja au nyingine katika Soka!”

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog