Sunday, November 29, 2015


Bale akipongezwa kwa bao lake la kwanza kwa Real Bale na Cristiano RonaldowakipongezanaRonaldo akishangilia PatashikaVuta nikuvute!


Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) leo hii imekabidhiwa bendera ya Taifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam. Akiongea wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo ya vijana, Ole Gabriel amewashukuru TFF kwa kuwekeza katika soka la vijana, na kusema mafaniko yote yanandaliwa chini, hivyo analipongeza Shirikisho kwa kuamua kuwalea na kuwaendeleza vijana hawa wenye vipaji kwa manufaa ya taifa ya baadae.


Tottenham wameikosa nafasi ya kupanda kwenye Ligi Kuu England na kukamata Nafasi ya 4 baada ya kutoka 0-0 na Chelsea kwenye Mechi ya Dabi ya London iliyochezwa White Hart Lane.
Sare hii imewabakisha Tottenham Nafasi ya 5 na kuwaweka Chelsea Nafasi ya 14.
Katika Kipindi cha Kwanza, Kipa wa Chelsea, Asmir Begovic, ndie alisumbuka sana kwa kuokoa michomo kadhaa ikiwepo ile ya out Son Heung-min, kwa Kichwa, na Shuti la chini la Mousa Dembele.
Leo Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alimpia Benchi Diego Costa na kumuanzisha Eden Hazard kama Fowadi kitu ambacho kilimkera Costa alieonekana kuvua gwanda lake la juu na kulitupa alipo Mourinho alipoona haingizwi.


Schweinsteiger aliisawazishia bao Man United katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko sare ya 1-1.
Kipindi cha kwanza dakika ya 24 Vardy anaipa bao la kuongoza Timu yake Leicester City na kuongoza bao 1-0 dhidi ya Man United.VIKOSI:
Leicester City wanaoanza XI:
Schmeichel, Simpson, Morgan, Huth, Fuchs, Mahrez, Kante, Drinkwater, Albrighton, Okazaki, Vardy
Akiba: De Laet, King, Schlupp, Ulloa, Dyer, Schwarzer, Inler
Manchester United wanaoanza XI: De Gea, Darmian, Smalling, Blind, McNair, Carrick, Schweinsteiger, Young, Mata, Martial, Rooney
Man Utd akiba: Depay, Romero, Fellaini, Schneiderlin, Rashford, Jackson, Andreas Pereira

Manchester United wametoka Sare 1-1 huko King Power Stadium walipotoka 1-1 na Leicester City na matokeo haya kuiruhusu Man City kutwaa uongozi wa Ligi Kuu England.
Leicester walitangulia kufunga kwa Bao la Jamie Vardy katika Dakika ya 24 na kumfanya avunje Rekodi ya Mchezaji wa zamani wa Man United, Ruud Van Nistelrooy, aliyoiweka Mwaka 2003 ya kufunga katika Mechi 11 mfululizo za Ligi Kuu England.
Man United walisawazisha katika Dakika ya 45 kwa Bao la kichwa la Bastian Schweinsteiger na walistahili kushinda kwenye Kipindi cha Pili kwa jinsi walivyotawala lakini tatizo lao sugu la kutokuwa na Wachezaji wenye kasi na Wafungaji liliwakisha.

Saturday, November 28, 2015


LIGI KUU ENGLAND:
Jumamosi Novemba 28
1800 Aston Villa v Watford
1800 Bournemouth v Everton
1800 Crystal Palace v Newcastle
1800 Man City v Southampton
1800 Sunderland v Stoke
2030 Leicester v Man United

Jumapili Novemba 29
1500 Tottenham v Chelsea
1705 West Ham v West Brom
1915 Liverpool v Swansea
1915 Norwich v Arsenal



Kocha wa klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani ambaye amewahi kuifundisha kwa mafanikio klabu ya FC Barcelona ya Hispania Pep Guardiola amekuwa akihusishwa kutakiwa kujiunga na klabu ya Manchester City ya Uingereza kwa muda mrefu sasa ila November 27 ameingia tena katika headlines kuhusiana na mpango huo.
2EC81B8E00000578-3336115-image-a-61_1448617745414
Headlines za kocha huyo kuwa njiani kujiunga na Man City zinapata nguvu kutokana na mkataba wake wa kuifundisha Bayern kuwa utamalizika mwishoni mwa msimu wa 2015/2016 na Man City wameahidi kumlipa kocha huyo zaidi ya mshahara wa pound milioni 13.2 ambao analipwa kocha wa sasa wa Chelsea Jose Mourinho.
g
Hawa ndio makocha wanaoongoza kwa kulipwa mishahara mikubwa duniani na Guardiola anashika nafasi ya tatu.
Dalili tatu za kocha huyo kuwa atajiunga na Man City ni kutokana na kutosaini mkataba mpya na klabu ya FC Bayern, kutotokea katika mkutano na waandishi wa habari November 27 na badala yake kuwakilishwa na beki wake Jerome Boateng na yeye kutajwa kuwa na appointment zake binafsi ndio maana hakutokea na tatu kuahidiwa kuwa atakuwa kocha anayeongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa duniani.
November 27 mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee vitu vitatu exclusive usivyovifahamu kutoka kwa staa wa soka wa Tanzania aliyewahi kutamba na vilabu vya Simba na Yanga Danny Mrwanda, wengi tumezoea kumsikia na kumuona akipachika magoli uwanjani ila November 27 ana majibu matatu kuhusu maisha yake ya soka.
1- Kama ulikuwa hufahamu Danny Mrwanda aliwahi kuacha shule na kuelekeza nguvu zake katika soka baada ya kumaliza kidato cha sita hivyo baba na mama yake mzazi walichelewa sana kumuelewa na kumuunga mkono kwa uamuzi huo“Nilisoma hadi form six lakini baadae nikaacha kuendelea na shule ili nicheze soka ila naamini nilifanya maamuzi sahihi kwa sababu sikuwahi kujutia ila nikasema mambo yasipoenda vizuri narudi shule ila mambo yalikuwa safi tu”
B15B1MN0413w
2- Aliwahi kuingia katika headlines na kupigwa faini ya Tsh 500,000/= baada ya kutowapa mikono wachezaji wa Simba wakati wa mchezo kati ya Simba dhidi ya Yanga vipi ana bifu na Simba au viongozi? “Mimi mpira ni kazi yangu hivyo sina sababu ya kuwa na chuki na mtu yoyote, kilichotokea pale ni kuwa niliennda kuchukua maji katika benchi lakini niliporudi ndio wenzangu wakawa wamepita wanasalimiana na mimi nikawa nimechelewa”
MRWANDA
3- Kuna wakati alikuwa anavaa jezi namba 9, jezi ambayo mastaa wenzake wa Yanga kama Tambwe na Kpah Sherman waliiacha kuitumia baada ya yeye kuiacha na kuna stori za kuwa jezi hiyo Yanga wachezaji wanaikimbia kwa sababu inaaminika kuwa ina nuksi ni kweli?



Jumapili ya November 29 klabu ya Arsenal itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu Uingereza dhidi ya Norwich City katika uwanja wa Carrow Road, huu utakuwa mchezo wa 14 kwa Arsenal, Arsenal ambao watacheza mchezo wao November 29 mjini Norwich wamesafiri leo November 28 kuelekea huko ila safari yao imeingia katika headlines.
Arsenal ambao wameamua kusafiri kwa kutumia ndege binafsi kutoka London kwenda Norwich wameingia katika mzozo na watu wa mazingira kutokana na kusafiri kwa kutumia ndege ambayo imetumia dakika 14 hivyo wanadaiwa kuchafua mazingira, kwani safari ya umbali mfupi wangeweza kutumia usafiri wa basi.
2EDCEFFC00000578-3336779-image-a-144_1448659081324
Hata hivyo kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amejitetea na kujibu kuwa wameamua kutumia usafiri wa ndege kutokana na barabara kuwa katika matengenezo, hivyo kama wangetumia usafiri wa basi wangekaa sana njiani, ndio maana wamefanya hivyo kukwepa msongamano. Hii sio mara ya kwanza kwa Arsenal kuingia katika mzozo na watu wa mazingira kwa kosa kama hilo, kwani waliwahi kuingia katika headlines hiyo mwaka 2012 baada ya kusafiri umbali wa maili 100 kwa kutumia ndege binafsi.

Bado watu wengi wanaogopa jiji la Paris Ufaransa kutokana na hali ya kiusalama kuaminika kuwa ndogo, Paris iliingia katika headlines November 13 2015 baada ya kufanyika shambulio la kigaidi, tukio ambalo lilifanya baadhi ya wachezaji wa Paris Saint Germain kuogopa kurejea Paris kutokana na kuhofia usalama wa maisha yao.
Tukio la shambulio la kigaidi lilitokea November 13 siku ya mchezo wa kirafiki kati ya Ufaransa dhidi ya Ujerumani mchezo ulichezwa uwanja wa Stade de France na kusababisha baadhi ya wachezaji kulala uwanjani kutokana na hali ya usalama kwa baadhi ya mitaa ya Paris kutokuwa nzuri licha ya kuwa hawakushambulia uwanjani hapo, watu 130 walipoteza maisha kufuatia shambulio hilo, klabu ya PSG ambayo makao makuu yake ni Paris imeamua kuimarisha usalama wa wachezaji wake.
psg-favorit-marseille-monaco-pengusik-700x500
Awali Edson Cavani na David Luiz walikuwa wanaogopa kurudi Paris ila klabu yao imeamua kuwaongezea ulinzi wachezaji wote katika makazi yao binafsi . Winga wa kimataifa wa Brazil Lucas Moura amethibitisha kuwa uongozi wa klabu yao kuweka ulinzi katika makazi ya mastaa hao pamoja na kubadili utaratibu wao wanapokwenda uwanjani.
187122915_3037682
Lucas Moura
“Wameongeza ulinzi majumbani kwetu, klabu imeweka ulinzi katika milango ya nyumba za wachezaji, lakini pia tuna utaratibu mwingine wakati tunapokuwa tunaenda uwanjani hatutembei tena mbele ya mashabiki kama ilivyokuwa awali ila tunaenda na basi moja kwa moja hadi katika Parking za magari” >>> Lucas Moura



Hii ni kwa watu wangu wa nguvu wapenda soka la Ulaya, Ligi Kuu soka Tanzania bara imesimama ila barani Ulaya Ligi bado zinaendelea kama kawaida, Ligi Kuu Uingereza inaendelea tena Jumamosi ya November 28 na Jumapili ya November 29 sawa na Ligi Kuu Hispania (LALIGA). Hispania itachezwa michezo tisa weekend hii wakati Uingereza itachezwa michezo 10. Naomba nikusogezee ratiba kamili ya mechi za weekend hii.
1
Ratiba ya mechi za Uingereza kwa saa za Afrika Mashariki Jumamosi ya November 28
  • Aston Villa Vs Watford Saa 18:00
  • Bournemouth Vs Everton Saa 18:00
  • Crystal Palace Vs Newcastle Saa 18:00
  • Man City Vs Southampton Saa 18:00
  • Sunderland Vs Stoke Saa 18:00
  • Leicester Vs Man Utd Saa 20:30
Jumapili ya November 29
  • Tottenham Vs Chelsea Saa 15:00
  • West Ham Vs West Brom Saa 17:05
  • Liverpool Vs Swansea Saa 19:15
  • Norwich Vs Arsenal Saa 19:15
2
Ratiba ya mechi za Hispania kwa saa za Afrika Mashariki Jumamosi ya November 28
  • Barcelona Vs Real Sociedad Saa 18:00
  • Atl Madrid Vs Espanyol Saa 20:15
  • Málaga Vs Granada CF Saa 22:30
  • Las Palmas Vs Deportivo de La Coruña Saa 00:00
  • Celta de Vigo Vs Sporting de Gijón Saa 00:05
Jumapili ya November 29
  • Getafe Vs Villarreal Saa 14:00
  • Eibar Vs Real Madrid Saa 18:00
  • Rayo Vallecano Vs Ath Bilbao Saa 20:15
  • Sevilla Vs Valencia Saa 22:30



Licha ya kuwa mwaka 2015 staa wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kufanya mipango yake mingi na kwa asilimia kubwa kufanikiwa, miongoni mwa ishu alizofanya Cristiano Ronaldo kwa mwaka 2015 ni kuzindua movie ya maisha yake halisi, perfume, viatu vyake lakini hii sio taarifa njema kwake.
football-boots-cristiano-ronaldo-nike-safari-launch
November 27 kutoka El Economista wametangaza kuwa kampuni ya vifaa vya michezo ya kimarekani Nike imetangaza kumtaja staa wa FC Barcelona Neymar kuwa ndio staa namba moja kwa sasa anayeuza brand ya bidhaa zao, rekodi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Ronaldo kwa miaka kadhaa ila November 27 Neymar ndio ameandikwa kumzidi Ronaldo.
neymar-promo-nike-reuters
Stori kutoka 101greatgoals.com inatajwa kuwa Neymar kwa mwaka 2016 ndio anatazamiwa kuwa staa atakayefanya vizuri kwa mauzo ya Nike na ndio maana kwa sasa anatajwa kuwa namba moja na Ronaldo kushuka, licha ya kuwa Ronaldo amefanya vizuri kwa miaka kadhaa. Ronaldo na Neymar wote wanamkataba wa kutangaza bidhaa za Nike .

Thursday, November 26, 2015


FC Barcelona na Neymar zinakaribia kusaini Mkataba mpya ambao utamfanya Kepteni huyo wa Brazil kuzoa Euro Milioni 15 kwa Msimu.
Donge hilo nono litamfanya awe Mchezaji wa 3 Duniani anaelipwa Mshahara wa juu kabisa akiwa nyuma ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Hivi sasa Neymar inasemekana analipwa Euro Milioni 8.8 kwa Mwaka.
Habari hizi zimetobolewa na Jarida la Marca huko Spain ambalo limesema Mkataba huo mpya utaongeza juu Dau lake ikiwa Klabu nyingine itataka kumnunua ndani ya Mkataba kutoka Euro Milioni 180 za sasa na kufikia Euro Bilioni 1 ingawa Wawakilishi wa Neymar wanataka Kipengele hicho kigote kwenye Euro Milioni 250.

Mkataba huo mpya utamweka Neymar, mwenye Miaka 23, Klabuni Barca hadi Juni 2021.

Hivi karibuni kulikuwa na minong’ono kuwa Neymar ataondoka Barca kutokana na kuwepo Kesi inayohusisha Uhamisho wake kutoka Klabu ya Brazil Santos kwenda Barca ambayo Baba yake Mzazi Neymar nae amehusishwa kwenye njama zinazodaiwa Barca ilifanya ili kukwepa kulipa Kodi huko Spain kwa kuficha gharama halisi za Uhamisho huo.

Hivi sasa Neymar anang’ara mno kiasi ambacho Wachambuzi wanatambua muda si mrefu atatwaa Ballon D'Or hasa ukizingatia umri wake ni mdogo ukilinganisha na Messi na Ronaldo ambao sasa wanaanza ‘kuzeeka’ Kisoka.



Jana klabu ya Manchester City ilikubali kipigo cha bao 1-0  dhidi ya Juventus ikiwa ni ligi ya mabingwa Ulaya.
Kiungo wa Juve Paul Pogba jana usiku alionesha uzalendo kwa taifa lake hilo baada ya kuvalia viatu maalumu vyenye rangi ya bendera ya Ufaransa kama sehemu ya kuwaenzi wahanga wa shambulio la kigaidi lililotokea katika jiji la Paris, Ufaransa.
Football Soccer - Juventus v Manchester City - UEFA Champions League Group Stage - Group D - Juventus Stadium, Turin, Italy - 25/11/15 Juventus' Paul Pogba's boots Action Images via Reuters / Andrew Couldridge Livepic EDITORIAL USE ONLY.
Kiungo huyo alikuwa mmoja wa watu waliokuwepo uwanjani wakati magaidi wanafanya mashambulizi nje ya uwanja wa Stade de France wiki iliyopita huku watu wasiopungua 124 wakipoteza maisha.


Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba amesema matarajio yake ya sasa ni kuona anarudi kwenye klabu yake ya zamani ya Chelsea kama kocha.
Drogba, ambaye kwa sasa anacheza soka ya kulipwa ya Montreal Impact huko Canada, aliifungia Chelsea jumla ya mabao 164 wakati akiitumikia klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo amesema angependa kuihudumia klabu hiyo baada ya kukamilika kwa kipindi chake cha  uchezaji.
”Tayari nimekubaliana na wakurugenzi wa klabu hiyo kuwa ninaweza kurejea kuwa meneja kwa sababu klabu hiyo ilinisaidia sana, pia imenikuza katika kipaji changu cha mpira”..
Drogba ndiye aliyeifungia Chelsea bao lililoipa ushindi na taji la mabingwa wa bara Ulaya mwaka wa 2012 pia aliisaidia Chelsea kunyakuwa mataji 4 ya ligi kuu ya Uingereza kabla ya kuhamia Canada kujiunga na klabu ya Montreal Impact.

Wednesday, November 25, 2015


Mpaka dakika 90 zinakatika hakuna mbabe! huku Man United ikipata nafasi nyingi za kufunga na kushindwa kuziona nyavu za wapinzani wao kwenye Uwanja wa Old trafford.DepayMartial akivutwa jezi!Van GaalRooney akiendesha mpiraVIKOSI:
Manchester United:
De Gea, Darmian, Smalling, Rojo, Blind, Schweinsteiger, Schneiderlin, Lingard, Rooney, Memphis, Martial.
Akiba: Romero, McNair, Young, Fellaini, Mata, Pereira, Wilson.

PSV: Zoet, Arias, Bruma, Moreno, Brenet, Hendrix, Guardado, Propper, Narsingh, De Jong, Locadia.
Akiba: Pasveer, Isimat, Pereiro, Schaars, Maher, Poulsen, Bergwijn
Refa: Pavel Kralovec

Rooney Kaanza mtanange huu..dhidi ya PSV

waliotembelea blog