Kuna mengi huwa yanaandikwa mitandaoni
na kwenye magazeti kuhusu soka mtu wangu wa nguvu, Jumamosi ya January 9
naomba nikusogezee TOP 5 ya headlines stories zilizoandikwa sana
mitandaoni Jumamosi ya January 9.
Klabu ya Real Madrid ya Hispania imeingia katika mbio za kuwania saini ya beki wa klabu ya Everton ya Uingereza John Stones, beki huyo alikuwa anawaniwa na klabu ya Chelsea ya Uingereza na dirisha la usajili wa wakati wa majira ya joto Chelsea walijaribu kutuma ofa tatu kwa Everton lakini zilikataliwa.
Manchester United inatajwa kuwa katika mipango ya kumshawishi kocha wa klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Laurent Blanc ajiunge na klabu yao, kwani bado hawana imani sana na kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal ambaye mkataba wake unamalizika 2017. Blanc aliwahi kuichezea Man United katika kipindi cha mwaka 2001 hadi 2003.
Kocha mpya wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Zinedine Zidane ameweka wazi kuwa hawana mpango wa kumuuza staa wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo kwenda katika klabu yoyote, hivyo hiyo ni taarifa ya kuvikatisha tamaa vilabu vya Man United na PSG vinavyohusishwa kumuhitaji nyota huyo “Ronaldo ni zaidi ya kusema hauzwi, roho yake ipo Real Madrid, ikiwa mimi nipo hapa na uhakika kuwa hawezi kwenda popote”
Klabu ya Arsenal kupitia kwa kocha wake Arsene Wenger imetajwa kuthibitisha kuwa ipo karibu kukamilisha usajili wa kiungoa wa Basle Mohamed Elneny siku kadhaa zijazo “Bado mpango wake ni mgumu kukamilika, lakini tunaweza kukamilisha naweza kusema ndani ya siku mbili au tatu”
Mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2015 Pierre Emerick Aubameyang amemaliza uvumi wa yeye kuwa katika mpango wa kujiunga na Arsenal na kusema kuwa hana mpango wa kuondoka Borussia Dortmund kwa hivi karibuni.