Wednesday, September 2, 2015


Manchester United wametoa Ofa a Pauni 100,000 kumnunua Kinda wa Miaka 17 anaechezea Newport County, Beki Regan Poole, ambae Dili yake huenda ikapanda na kufikia Pauni 400,000.
Hivi sasa Kijana huyu yuko huko Man United akipimwa afya yake.


Winga wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester United David Beckham usiku wa Septemba 1 alipewa Tuzo ya Heshima. Licha ya kuwa amestaafu bado mchango na uwezo wake aliyo uonyesha katika soka bado unatambulika na kuheshimika.
Hizi ni picha za tukio lenyewe mtu wangu
2BE2BA0A00000578-3218853-image-a-51_1441140484174
2BE258EB00000578-0-image-a-3_1441137700174

2BE2BA0600000578-3218853-image-a-52_1441140491971
Tuzo hizo za 20 ambazo hujulikana kama Legend of Football Award alipewa na wanachama wa kamati ya Football Extravaganza na alipewa Tuzo hiyo katika ukumbi wa The Grosvenor House London usiku wa Septemba 1.


Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry, ameongea maneno ya kumtetea kocha wa Arsenal Arsene Wenger baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili. Henry ambaye ana heshima kubwa katika klabu hiyo amemkingia kifua Wenger juu ya lawama za kuto sajili.
Licha ya kuwa Henry kauli yake ya mwanzoni ilikuwa ni kumshawishi Wenger asajili mshambuliaji wa kati mmoja mahiri, akiwa anaamini kuwa Arsenal haiwezi twaa taji la Ligi Kuu Uingereza kwa Olivier Giroud pekee, sasa ana kauli tofauti kidogo, kwani baada ya dirisha la usajili kufungwa Henry ana mtetea Wenger na kusema ana kikosi imara.
Real-Madrid-vs-Manchester-City
Karim Benzema
” Sifikirii kama Wenger hakutaka kusajili wachezaji wengine kama ndivyo hilo lingekuwa suala jingine lakini alisema kama mipango yake itakuwa imekamilika atajaribu kusajili, lakini unampataje Benzema kutoka Real Madrid ambapo anacheza kila wiki na Cavani kutokea PSG ambaye anafunga magoli? ni ngumu”>>> Henry
“Sifikirii kama hakutaka kusajili mchezaji yoyote, alitaka kusajili kama tulivyokuwa tunajua ila suala hilo halikutokea. Sioni kama wanaelekea kuchukua ubingwa wa Ligi msimu huu, lakini nafikiri Wenger anaamini atashinda ubingwa wa Ligi akiwa na timu hiyo ni nzuri kwa mtazamo wake”>>> Henry
Newcastle-vs-Arsenal
Peter Cech
Arsenal ambayo ipo nyuma ya Manchester City kwa point tano haijafanya usajili wowote mkubwa katika dirisha hili la usajili zaidi ya kumsajili aliyekuwa golikipa wa Chelsea Peter Cech. Hivyo wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo hawana imani na mwenendo wa sasa wa timu yao.



Klabu ya Manchester United imemsajili mshambuliaji mwenye umri wa miaka 19 kwa dau la pound milioni 36 akitokea klabu ya Monaco ya Ufaransa, Anthony Martial lakini mashabiki wamekuwa wakihoji kiwango hicho cha fedha kwa mchezaji huyo chipukizi, huenda ni kwa sababu hawa mfahamu.
2BE5EC8600000578-3219385-image-a-8_1441184638572
Martial ni mchezaji au mtu mwenye tabia za kupenda kukaa ndani, kupenda kupikiwa chakula na mama yake, ni mpenzi wa kuangalia Tv na kukaa na familia yake wakati ambapo anakuwa kamaliza kucheza mechi au kufanya mazoezi.
2BE5E9F700000578-3219385-image-a-14_1441184760864
Mshambuliaji huyo amemuoa Samantha na wana mtoto mmoja wa kike anaitwa Toto, huku wakitarajia kupata mtoto wa pili kwani mpenzi wake ni mjamzito kwa sasa. Dau la uhamisho wa Martial ambalo linafikia pound milioni 58 pamoja na bonus, linamfanya atajwe kama mchezaji mdogo mwenye thamani zaidi.
2BE5EF0C00000578-3219385-Martial_s_infant_daughter_Toto_dons_a_Monaco_kit_with_her_name_a-a-3_1441190703880
Martial ambaye watu na vyombo vingi vya habari za michezo hupenda kumlinganisha na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Thierry Henry, huwa na tabia ya kupenda kuchat na mpenzi wake muda mchache kabla ya mechi na kusikiliza muziki.
2BE5E15600000578-3219385-Martial_is_married_to_childhood_sweetheart_Samantha_and_the_coup-a-2_1441190703782
2BE676B500000578-3219385-image-a-2_1441188472682
2BE7396100000578-3219385-image-a-4_1441192866031
Hii ni video moja kati ya magoli yake aliyofunga akiwa na Monaco

waliotembelea blog