Wednesday, December 14, 2016


MCHEZAJI wa Kimataifa wa Algeria Riyad Mahrez ametwaa Tuzo ya BBC ya Mchezaji Bora Afrika kwa Mwaka 2016.
Mahrez, Mzaliwa wa France mwenye Miaka 25, aliisaidia mno Leicester City kutwaa Ubingwa wa England Mwezi Mei kwa mara ya kwanza katika Historia yao na hilo limempa Tuzo hii maarufu na inayosifika ya BBC, Shirika la Utangazaji la Uingereza.
Mapema Mwaja huu, Mahrez alitunukiwa Tuzo ya PFA ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa England baada ya kuifungia Bao 17 na kutoa Msaada wa Bao 11 kwenye EPL, Ligi Kuu England, na kuwa Mchezaji wa Kwanza kutoka Afrika kuwahi kushinda Tuzo hiyo ya PFA, Professional Footballers Association, ambacho ni Chama cha Kutetea Maslahi ya Wanasoka wa Kulipwa.

Mahrez alishinda Tuzo hii ya BBC kwa kuzoa Kura nyingi za Mashabiki na kuwabwaga Wagombea wengine ambao ni Yaya Toure, Sadio Mane, Pierre-Emerick Aubameyang na Andre Ayew.
Mahrez, ambae alijiunga Leicester Mwaka 2014 akitokea Klabu ya France Le Havre kwa Dau la Pauni 400,000, sasa anaungana na kina Didier Drogba na Staa wa Liberia George Weah ambao waliwahi kushinda Tuzo hii.


CRISTIANO RONALDO ameshinda Tuzo maarufu na iliyotukuka ya Ballon d'Or kutoka Listi ya Wagombea 30 akiwemo alieishika kmWaka Jana Lionel Messi. Cristiano Ronaldo lifts the European ChampionshipHii sasa ni mara ya 4 kwa Ronaldo kutwaa Tuzo hii akizidiwa mara 1 tu na Messi.
Ballon d'Or inasimamiwa na Jarida maarufu France Football na Mshindi wake hupatikana kwa Kura za Wanahabari 173 toka kila pembe ya Dunia.
France Football imekuwa ikisimamia Ballon d'Or kila Mwaka tangu 1956 lakini kwa Miaka 6 iliyopita wamekuwa wakishirikiana na FIFA na Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka kuitwa FIFA Ballon d'Or
Lakini Mwezi Septemba FIFA ikajitoa na kuanzisha Tuzo yao ikuwemo zile za Kinamama, Timu ya Mwaka na Washindi wake wanategemewa kutangazwa kwenye Hafla maalum hapo Januari 9 huko Zurich.
Ronaldo, ambae amefunga Bao 48 katika Mechi 52 kwa Klabu yake Real Madrid na Nchi yake Portugal kwa Mwaka huu 2016, hakuwepo huko France kuipokea Tuzo hiyo kwa vile yuko Japan na Real ambao watashiriki Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.
Mwaka huu, Ronaldo aliisaidia Real kutwaa Ubingwa wa Ulaya na pia Portugal kubeba EURO 2016, Kombe la Mataifa ya Ulaya.
Ronaldo, ambae pia ametwaa Ballon d'Or katika Miaka ya 2008, 2013 na 2014, ameeleza: “Kwangu mimi hii ni heshima kubwa kutwaa huu Mpira wa Dhahabu kwa mara ya 4. Ni ndoto iliyotimia. Nimefurahi sana! Nawashukuru Wachezaji wenzangu, toka Timu ya Taifa na Real Madrid. Basikia fahari na furaha kubwa!”

RONALDO katika Namba:

4 – Ushindi Ballon d'Or Miaka ya 2008, 2013, 2014 na 2016 akiteuliwa mara 8 kugombea.
137 – Mechi kwa Portugal.
68 – Goli kwa Portugal.
4 – Mwaka huu amekuwa Mchezaji wa Kwanza kufunga katika Fainali za EURO (2004, 2008, 2012 na 2016).
80 – Pauni Milioni walizolipa Real Madrid kumnunua kutoka Manchester United 2009.
17 – Rekodi ya Bao nyingi kwa Msimu Mmoja wa UEFA CHAMPIONS LIGI (2014).
270 – Idadi ya Magoli kwa Real Madrid katika Mechi 248 za La Liga.
9 – Jumla ya Mabao kwenye EURO akifungana na Michel Platini kuwa Wafungaji Bora wa Mashindano hayo ya Mataifa ya Ulaya.
14.1 – Pauni anazovuna kutoka kwa Udhamini wa Nike.
48,756,584 – Wafuasi Mtandao wa Twitter.
118,164,346 – Wafuasi Mtandao wa Facebook

WAGOMBEA 30 WA 2016 Ballon d'Or:

Sergio Aguero (Manchester City), Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund), Gareth Bale (Real Madrid), Gianluigi Buffon (Juventus), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Kevin de Bruyne (Manchester City), Paulo Dybala (Juventus), Diego Godin (Atletico Madrid), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Gonzalo Higuain (Juventus), Zlatan Ibrahimovic (Manchester United), Andres Iniesta (Barcelona), Koke (Atletico Madrid), Toni Kroos (Real Madrid), Robert Lewandowski (Bayern Munich), Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Riyad Mahrez (Leicester City), Lionel Messi (Barcelona), Luka Modric (Real Madrid), Thomas Muller (Bayern Munich), Manuel Neuer (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Dimitri Payet (West Ham), Pepe (Real Madrid), Paul Pogba (Manchester United), Rui Patricio (Sporting Lisbon), Sergio Ramos (Real Madrid), Luis Suarez (Barcelona), Jamie Vardy (Leicester City), Arturo Vidal (Bayern Munich).


DROO ya Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONS LIGI imefanyika huko Nyon, Uswisi na Mabingwa Watetezi Real Madrid kupangwa kucheza na Napoli.
Arsenal ya England itacheza na Vigogo wa Germany wakati PSG ikiivaa FC Barcelona.
Manchester Citi itaikwaa Monaco wakati Mabingwa wa England Leicester City wakicheza na Sevilla ya Spain.
DROO KAMILI:
Sevilla v Leicester
PSG v Barcelona
Leverkusen v Atletico Madrid
Porto v Juventus
Bayern Munich v Arsenal
Benfica v Borussia Dortmund
Real Madrid v Napoli
Manchester City v Monaco
Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL zitachezwa Tarehe 14/15 na 21/22 Februari na Marudiano ni Tarehe 7/8 na 14/15 Machi.

TAREHE MUHIMU:MECHI ZA MTOANO:
14/15 na 21/22 Feb 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Kwanza
7/8 na 14/15 Machi 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Pili
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)


Leo Jumatano zipo Mechi 8 za EPL na Vinara Chelsea wapo Ugenini Stadium of Light kucheza na Sunderland, Liverpool Ugenini na Boro, Man United Ugenini na Crystal Palace wakati Spurs wako kwao kucheza na Hull City.
Mechi hizo ni mwendelezo wa Mechi 2 za Jana za Raundi ya 16 ya EPL ambapo Arsenal walipoteza nafasi ya kutwaa uongozi wa Ligi walipotandikwa na Everton 2-1 huko Goodison Park Jijini Liverpool.
Matokeo haya yabaibakisha Chelsea kileleni hata kama Leo watafungwa kwani wana Pointi 37 wakifuata Arsenal wenye 31 na wa 3 ni Liverpool wenye Pointi 31zikifuata Man City 30, Spurs 27 na Man United 24.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumatano Desemba 14

2245 Middlesbrough v Liverpool
2245 Sunderland v Chelsea
2240 West Ham United v Burnley
2300 Crystal Palace v Manchester United
2300 Manchester City v Watford
2300 Stoke City v Southampton
2300 Tottenham Hotspur v Hull City
2300 West Bromwich Albion v Swansea City
 

Jumamosi Desemba 17
1530 Crystal Palace v Chelsea
1800 Middlesbrough v Swansea City
1800 Stoke City v Leicester City
1800 Sunderland v Watford
1800 West Ham United v Hull City
2030 West Bromwich Albion v Manchester United

Jumapili Desemba 18

1630 Bournemouth v Southampton
1900 Manchester City v Arsenal
1900 Tottenham Hotspur v Burnley

Jumatatu Desemba 19
2300 Everton v Liverpool

waliotembelea blog