Wednesday, November 25, 2015


Mpaka dakika 90 zinakatika hakuna mbabe! huku Man United ikipata nafasi nyingi za kufunga na kushindwa kuziona nyavu za wapinzani wao kwenye Uwanja wa Old trafford.DepayMartial akivutwa jezi!Van GaalRooney akiendesha mpiraVIKOSI:
Manchester United:
De Gea, Darmian, Smalling, Rojo, Blind, Schweinsteiger, Schneiderlin, Lingard, Rooney, Memphis, Martial.
Akiba: Romero, McNair, Young, Fellaini, Mata, Pereira, Wilson.

PSV: Zoet, Arias, Bruma, Moreno, Brenet, Hendrix, Guardado, Propper, Narsingh, De Jong, Locadia.
Akiba: Pasveer, Isimat, Pereiro, Schaars, Maher, Poulsen, Bergwijn
Refa: Pavel Kralovec

Rooney Kaanza mtanange huu..dhidi ya PSV

Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger ni miongoni mwa makocha wanaotajwa kuwa wagumu wa kutumia fedha nyingi katika kuwekeza kununua wachezaji na kuboresha kikosi chake, Wenger mara nyingi majina ya wachezaji wakubwa na wanaouzwa kwa gharama za juu huwa anashindwa kuwasajili na mwisho wa siku wanasajiliwa na timu nyingine.
November 25 kauli ya kocha wa Arsenal Arsene Wenger imeingia katika headlines baada ya kuulizwa swali na muandishi kutokana na mwenendo wa tabia yake ya matumizi ya fedha hususani tukiwa tunaelekea katika dirisha dogo la usajili la mwezi January, hakubaliani na watu wanaomuita yeye bahili.
arsene-wenger-manages-a-smile-pic-getty-89992389
“Hapana sikubaliani na wewe kuwa mimi mbahili kama nitapata nafasi ya kukutoa out ndio utakapojua namna ambavyo huwa napenda kutumia fedha, rafiki zangu huwa hawanifirii hivyo, kwa sasa tunaenda kucheza na Olympiacos na tunaamini tutafuzu hatua ya 16 bora ya UEFA” >>> Arsene Wenger
Wenger usiku wa November 25 alifufua matumaini ya kikosi chake kusonga mbele katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya baada ya kufanikiwa kuifunga klabu ya Dinamo Zagreb kwa jumla ya goli 3-0, hivyo  matumaini ya kwenda hatua inayofuata yapo endapo watafanikiwa kushinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Olympiacos.


Usiku wa leo kutakuwa na mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya kati ya PSG ya Ufaransa dhidi ya klabu ya Malmo ya Sweden.
Zlatan Ibrahimovic atakuwa nyumbani katika mji wa Malmo, Sweden wakati atakapokuwa na timu yake…lakini mashabiki wa nyumbani wameamua kuonyesha heshima kubwa kwake kwa kumkaribisha kwa staili ya aina yake ikiwa ni miaka 14 tangu aihame timu hiyo ya nyumbani.
mji
Moja ya makumbusho ya jengo lililojengwa mwaka 1546 mjini Malmo ambapo kumeandaliwa tafrija ya kumpokea Zlatan.
Jengo refu kuliko yote katika mji huo wa Malmo umepambwa kwa herufi kubwa ya Z ikiwa na maana ya jina lake Zlatan.Hii ni moja ya ishara ya kumkaribisha tena staa huyo lakini safari hii akiwa na timu ya ugenini.
jina
Jengo refu zaidi Sweden lililopambwa kwa herufi Z likimaanisha Zlatan
Zlatan amewaambia  mashabiki wa Malmo wanaweza kuimba jina lake kama walivyokuwa wakifanya awali wakati akiitumikia timu hiyo.

mahakama
Malmo ndiyo ilikuwa timu yake ya kwanza kubwa iliyomkuza kisoka kabla ya kununuliwa na Ajax ya Uholanzi.



Ni mrembo, ana sauti na figure nzuri na kama wewe ni mfuatiliaji wa Coke Studio Africa basi utakuwa unakutana nae kila wiki kwenye ‘mashup’ sessions za Coke Studio na msanii kutoka Nigeria, M.I hapa namzungumzia Avril staa wa muziki kutoka Kenya.
Nimekutana na interview aliyofanya Avril siku chache zilizopita na Daily Nation’s Buzz ya Kenya na kikubwa alichokigusia kwenye interview hiyo ni sababu ya yeye kuacha kushare na watu kwenye mitandao ya kijamii picha za mume wake mtarajiwa.
AVRIL4
Avril.
Kwenye kupiga stori, Avril aliigusia issue ya kutokupost tena picha za mchumba wake kwenye social media akidai kitendo hicho kilikuwa kinamsumbua sana mchumba wake…
>>> “Watu wamekuwa wafuatiliaji sana utakuta amekaa sehemu mwenyewe hana habari ya hiki wa kile na watu wanapokutana naye na kuhisi kuwa ni yeye wanakimbilia kwenye Instagram yangu kuhakikisha kuwa ni yeye, na wengine utakuta wanaanza kumuongelea kwa nguvu mpaka mwenyewe anasikia, kitendo hicho kinamkera kwasababu hapendi umaarufu huo. Baadaye nikaona bora kuyaheshimu maamuzi yake…” <<< Avril
AVRIL1
Avril na mchumba wake.
Kuhakikisha kuwa wawili hao wanapata muda mwingi wa kuwa private kwenye mitoko yao, Avril anasema anajitahidi kutafuta sehemu ambazo zitakuwa ngumu kwa watu kuwaona na kuwagundua…
>>> “Tumeweza kupata sehemu chache za kwenda na kujificha; tunajua jinsi ya kujificha. Nikiwa natoka kwenda kwenye event yoyote ile, yeye huchelewa kidogo kufika ili watu wasimpatie attention kubwa itakayomfanya ajisikie vibaya…” <<< Avril.
AVRIL3
Siku ya jumatatu Avril aliitembelea studio za Radio Citizen na kudokeza kidogo mipango yake ya harusi, harusi ambayo kwa mujibu wa Avril itafungwa mwaka 2016…
>>> “Harusi yangu itafungwa mwakani (2016). Mara nyingi sherehe ya harusi inafanyika kwa ajili ya wazazi. Pale ambapo pande zote mbili za familia zitakutana na utambulisho utakamilika, basi tutabarikiwa na kheri za kufunga harusi… kwa upande wangu , familia yangu bado inachukuwa time ya kuijua familia ya mwenzangu kuona kama nimevuruga ama nipo sehemu salama.” <<< Avril.

Band ya Yamoto tayari imeondoka jana usiku kuelekea Marekani tayari kwa ziara yao ya wiki tatu baada ya kupata mwaliko kutoka kwa Watanzania wanaoishi huko.
Mkubwa Fella amezungumzia safari hiyo kuwa ni mwaliko walioupata kutoka kwa Watanzania wenzao wanaoishi USA ambapo watakwenda kufanya show na wameondoka na timu nzima ya watu nane.
ziarani
Kundi la Yamoto Band wakiwa Uwanja wa ndege jana usiku tayari kwa safari ya Marekani.
Akizungumzia show watakazofanya huko Mkubwa Fella amesema..“Itakuwa ni ziara ya wiki tatu na watarejea Tanzania tarehe 16, show ya kwanza watafanya Tarehe 27 Kenshaz City, na ya pili watafanya tarehe 12 huko Washington , hii ni mara ya kwanza kwa Yamoto kupata mualiko kwenda US, nimefurahi sana na kila siku nasema tutaendelea kutoa furaha mpya Marekani, mashabiki wetu wategemee mazuri zaidi“..Mkubwa Fella.
Ameongeza kuwa baada ya ngoma ya ‘Cheza kwa Madoido’ wametengeneza ngoma nyingine inaitwa ‘Mama’ na wanatarajia wakirudi wataachia ngoma yao ambayo wamemshirikisha Zena Mohamed kutoka kundi la Five Stars.


Oscar Oscar akipetaNyumba inaungua..Willian akipongezwa na CostaMeneja Jose Mourinho Ben alioneshwa na mwamuzi kadi nyekundu hivyo timu yake kucheza pungufu muda woteGary Cahill akijipongezaPongezi1-0Eden Hazard

Pedro Patashika..Oscar akijionea mchezaji wa timu pinzani akifanya yakehttp://i1.mirror.co.uk/incoming/article6894427.ece/ALTERNATES/s1227b/Maccabi-Tel-Aviv-vs-Chelsea-Champions-League-Group-Stage.jpgWillian akishangilia bao
Bao za Chelsea zimefungwa na Gary Cahill dakika ya 20'
Willian dakika ya 73 na lile la Oscar dakika ya 77 hivyo kuumaliza kwa dakika 90 Chelsea wakiwa wababe kwa kuibuka na ushindi wa bao 3-0.

VIKOSI:
MACCABI TEL-AVIV: Rajković; Dasa, Ben Haim, Carlos García, Ben Harush; Alberman, Zahavi, Rikan, Igiebor; Peretz, Ben Chaim
Akiba: Lifshitz, Ben Basat, Itzhaki, Azulay, Tibi, Mitrovic, Vermouth

CHELSEA: Begovic; Azpilicueta, Cahill, Terry (c), Rahman; Fabregas, Matic; Willian, Oscar, Hazard; Costa

Akiba: Blackman, Ivanovic, Zouma, Mikel, Loftus-Cheek, Pedro, Remy
Vijana wa MACCABI TEL-AVIV wakifanya mazoezi

waliotembelea blog