Wednesday, November 25, 2015



Ni mrembo, ana sauti na figure nzuri na kama wewe ni mfuatiliaji wa Coke Studio Africa basi utakuwa unakutana nae kila wiki kwenye ‘mashup’ sessions za Coke Studio na msanii kutoka Nigeria, M.I hapa namzungumzia Avril staa wa muziki kutoka Kenya.
Nimekutana na interview aliyofanya Avril siku chache zilizopita na Daily Nation’s Buzz ya Kenya na kikubwa alichokigusia kwenye interview hiyo ni sababu ya yeye kuacha kushare na watu kwenye mitandao ya kijamii picha za mume wake mtarajiwa.
AVRIL4
Avril.
Kwenye kupiga stori, Avril aliigusia issue ya kutokupost tena picha za mchumba wake kwenye social media akidai kitendo hicho kilikuwa kinamsumbua sana mchumba wake…
>>> “Watu wamekuwa wafuatiliaji sana utakuta amekaa sehemu mwenyewe hana habari ya hiki wa kile na watu wanapokutana naye na kuhisi kuwa ni yeye wanakimbilia kwenye Instagram yangu kuhakikisha kuwa ni yeye, na wengine utakuta wanaanza kumuongelea kwa nguvu mpaka mwenyewe anasikia, kitendo hicho kinamkera kwasababu hapendi umaarufu huo. Baadaye nikaona bora kuyaheshimu maamuzi yake…” <<< Avril
AVRIL1
Avril na mchumba wake.
Kuhakikisha kuwa wawili hao wanapata muda mwingi wa kuwa private kwenye mitoko yao, Avril anasema anajitahidi kutafuta sehemu ambazo zitakuwa ngumu kwa watu kuwaona na kuwagundua…
>>> “Tumeweza kupata sehemu chache za kwenda na kujificha; tunajua jinsi ya kujificha. Nikiwa natoka kwenda kwenye event yoyote ile, yeye huchelewa kidogo kufika ili watu wasimpatie attention kubwa itakayomfanya ajisikie vibaya…” <<< Avril.
AVRIL3
Siku ya jumatatu Avril aliitembelea studio za Radio Citizen na kudokeza kidogo mipango yake ya harusi, harusi ambayo kwa mujibu wa Avril itafungwa mwaka 2016…
>>> “Harusi yangu itafungwa mwakani (2016). Mara nyingi sherehe ya harusi inafanyika kwa ajili ya wazazi. Pale ambapo pande zote mbili za familia zitakutana na utambulisho utakamilika, basi tutabarikiwa na kheri za kufunga harusi… kwa upande wangu , familia yangu bado inachukuwa time ya kuijua familia ya mwenzangu kuona kama nimevuruga ama nipo sehemu salama.” <<< Avril.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog