Wednesday, January 29, 2014

Justin Bieber mashakani
Mwanamziki mashuhuri wa muziki wa 'pop' kutoka Canada Justin Bieber amefunguliwa mashtaka ya kumpiga dereva wa gari la kifahari la kukodisha mwezi Disemba mwaka uliopita.
Bwana Bieber aliye na umri wa miaka 19 alikaribishwa katika katika kituo cha polisi cha Toronto na kikosi kikubwa cha wapiga picha za televisheni pamoja na unyende wa mashabiki wake chipukizi.
Amefunguliwa mashtaka chini ya juma moja baada ya kukamatwa mjini Florida marekani kwa shutuma za kuendesha gari akiwa mlevi na mashtaka mengine.
Mwanasheria wa Marekani anayemwakilisha mwimbaji huyo amesema mteja wake hana makosa.
Kwa mujibu wa polisi wa Toronto, yapata saa 02:50 saa za Canada tarehe 30 Disemba, gari la kifahari liliwasili kumchukuwa bwana Bieber na wenzake watano katika kilabu moja ya starehe ili kuwarejesha katika chumba chao cha hoteli.
Na wakati walipokuwa njiani, dereva huyo pamoja na mmoja wa abiria wake, aliyetajwa kama bwana Bieber, wanasemekana kuanza kufokeana maneno makali.
Abiria huyo "alimgonga dereva wa limousine hiyo kwenye kisogo mara kadhaa", polisi wamesema.
Dereva huyo anasemekana kusimamisha gari lake na kisha kutoka nje na kuwaita polisi. Mshukiwa 'alichana mbuga' kabla ya polisi kuwasili.
Bwana Bieber alijisalimisha kwa polisi Jumatano. Anatarajiwa kufikishwa kizimbani tarehe kumi mwezi Machi.
Justin Bieber amekuwa na 'vituko' katika siku za hivi karibuni
Howard Weitzman, wakili wa Bwana Bieber mjini California, amesema msanii huyo hana hatia na kwamba anatarajia kesi hiyo itachukuliwa kama kosa dogo tu.
Kuendesha gari akiwa mlevi
Kadhalika siku ya Jumatano, ombi la kutaka bwana Bieber atimuliwe nchini marekani lilipata sahihi laki moja.
Ombi hilo liliwasilishwa kwenye mtandao mmoja wa Ikulu ya White House na raia mmoja wa Marekani.
Rais wa Marekani hana madaraka ya kuamuru mtu kuondolewa kwa lazima nchini Marekani, na haijabainika iwapo Ikulu ya White House itajibu ombi hilo.
Bwana Justin Beiber amejikuta matatani mara kadhaa na maafisa wa polisi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Mapema asubuhi Alhamisi iliyopita, bwana Bieber alikamatwa kwenye Ufukwe wa Miami baada ya afisa mmoja wa polisi kumfumania akiendesha kwa kasi gari la kukodi aina ya Lamborghini rangi ya njano kwenye barabara ya umma.
Akimshuku kuwa alikuwa mlevi afisa huyo alimtia mbaroni.
Kadhalika alifunguliwa mashtaka ya kupinga kukamatwa na pia kuendesha gari akiwa na leseni iliyopita muda wa matumizi.

Mshambulizi Sergio Aguero wa Man City
Klabu ya Manchester City imechupa hadi kileleni mwa ligi kuu ya soka nchini England baana ya kuonesha soka safi dhidi ya klabu ya Tottenham katika uga wa White Hart Lane.
Kikosi cha kocha Manuel Pellegrini kilihitaji ushindi dhidi ya Spurs ili kuwapiku Arsenal kwenye jedwali la msimamo wa ligi hiyo, na matumaini hayo yalianza kuonekana mapema wakati Aguero alipovuna bao la kwanza, hii ikiwa ni mara ya nane mfululizo akiifungia City katika mechi nane mfululizo.
Yaya Toure aliiweka Man City kifua mbele kwa bao la pili, dakika ya tano kipindi cha pili kupitia mkwaju wa penalti uliozua utata ambapo mlinda ngome wa Spurs Danny Rose alitimuliwa uwanja kwa kulishwa kadi nyekundu japo alionekana kuugusa mpira kwanza kabla ya kuadhibiwa kwa kumchezea rafu Edin Dzeko.
Dzeko aliongeza bao la tatu na ingawa Etienne Capoue alifunga bao la kufuta machozi kwa Spurs, bado kulikuwa na fursa kubwa kwa Man City kuendelea kuinyeshea Spurs mvua ya magoli kupitia mchezaji wa akiba Stevan Jovetic aliyefunga bao lake la kwanza katika ligi kuu tangu uhamisho wake wa pauni £22m kutoka klabu ya Fiorentina ya Italia.
Aguero afunga mabao 50
Baada ya mechi hiyo Sergio Aguero sasa ameandikisha rekodi ya kufunga takriban mabao 50 ya ligi kuu baada ya mechi 81, na kuibuka kuwa mtu wa tano kufunga kiasi hicho cha mabao, baada ya Andy Cole, Alan Shearer, Ruud van Nistelrooy na Fernando Torres.
Kisha City ikaongeza maumivu zaidi kwa Spurs baada ya kile kipigo cha mabao 6-0 mwezi November mwaka uliopita, pale Vincent Kompany alipokamilisha kibarua kwa kufunga bao la tano na la ushindi.
Kwenye matokeo ya mechi nyinginezo Chelsea ilipata pigo kwenye harakati zake za kutafuta uongozi kwenye jedwali baada ya kulazimika kutoka sare ya kutofungana na West Ham katika uwanja wa nyumbani Stamford Bridge.
Kwingineko Aston Villa iliishinda West Brom mabao 4 - 3 nayo Sunderland ikainyuka Stoke 1-0.

Hii ndiyo orodha ya saba bora tarehe 30-01-2014:
1 Man City 53
2 Arsenal 52
3 Chelsea 50
4 Liverpool 46
5 Tottenham 43
6 Everton 42
7 Man Utd 40



Wabunge wa Ukraine
Bunge la Ukraine limeidhinisha sheria inayotoa msamaha kwa waandamanaji waliozuiliwa wakati wa vurugu zilikumba taifa hilo katika siku za hivi karibuni.
Vyama vya upinzani vilisusia kura hiyo kulalamikia kifungu katika mswada wa sheria hiyo ambacho kinasema msamaha utatolewa tu ikiwa waandamanaji watasalimisha majengo ya serikali ambayo wameteka katika siku za hivi karibuni.
Waandamanaji katika baarabara za mji mkuu wa Kiev kadhalika wamekatalia mbali hatua hiyo.
Maandamano hayo yalianza mwezi Novemba mwaka uliopita baada ya rais Viktor Yanukovych kubatili uamuzi wa kusaini mkataba wa kibiashara kati ya Ukraine na umoja wa ulaya.
Kisha baadaye akatia saini mkataba wa mkopo wa takriban dola bilioni 15 na Urusi.
Maandamano bado yanaendelea nchini Ukraine
Hapo jana jumatano, mkuu wa sera za za kigeni katika umoja wa Ulaya Catherini Ashton alisema kuwa amegutushwa na vurugu zilizosababisha maafa katika mji wa mkuu wa Kiev na maneo mengine ya taifa hilo.
" Ni lazima nisema kuwa nimegutushwa sana anasema Bi. Ashton, na ripoti na ripoti ambazo nimepata kuhusu hali ilivyo na bila shaka mojawepo wa maswala muhimu tunayopaswa kushugulikia ni kuzuia vurugu na vitisha. Nina wasiwasi kuhusu watu ambao inaonekana wametoweka. Kuna gumzo kali kwamba ukijadili hili na watu wengi, kuhusu watu kuwa katika hali iliyo sawa na mateka na mengine yanayotokana na vurugu ni sharti yakome. Ni swala lenye umuhmu mkubwa,'' anasema Bi Catherine Ashton
Catherine Ashton - ambaye yuko mjini Kiev kufanya mazungumzo na bwana Yanukovych pamoja na makundi ya upinzani amesema Ukraine inahitaji suluhu ya kisiasa itakayopatikana kwa haraka na kumshirikisha kila mmoja.
Hapo jana jioni mswada huo wa kutoa msamaha ulipitishwa kwa kura 232 dhidi ya 11, huku chama cha Bwana Yanukovych cha Party of the Regions kilicho na idadi kubwa ya wabunge kikiunga mkono.
Lakini wabunge 173 hawakupiga huku wabunge wa upinzani wakipiga mayowe kupinga kura hiyo.

 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokreasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee wakiondoka baada ya kuhutubia mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Ifakara jana.

  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akimtambulisha mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Dama, uliofanyika katika Kata ya Tungi mjini Mororgoro jana.

  Afande Sele akiwahutubia wananchi wa Kata ya Tungi mjini Morogoro jana, katika mkutano wa hadhaa wa Operesheni M4C Pamoj Daima, ambao pia ulihutubia na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.
  wakazi wa mji wa Ifakara, wakitawanyika baada ya mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana.
 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mtibwa,
 Baadhi ya wa mji wa Ifakara wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana.


 Mwenyekiti wa Chama ch Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia


 .Maelefu ya wakazi wa mkji wa Ifakara,


 


 

 Kocha wa Manchester City akijionea mwenyewe wenzao bao 5-1 kwao White Hart Lane.

 
 Bao la nne kwa City limefungwa na Stevan Jovetic katika dakika ya 78, Huku Spurs wakicheza pungufu wakiwa 10. Spurs Mchezaji wao alifanya makosa na hatimaye Kompany akawashona bao la tano na kufanya 5-1 dhidi ya wenyeji Spurs.
Yaya Toure na Dzeko wakipongezana baada ya kupata bao.

Yaya Toure akifunga mkwaju wa penati
 
 
 
 

 
 Kocha wa Spurs akitoa maelekezo kwa wachezaji baada ya kuona wanapitiwa kimchezo na kufungwa fungwa katika kipindi cha pili.




Samuel Eto'o akiachia shuti kali

J




Jose Mourinho akipagawa na kulalamikaLosing ground: Chelsea failed to get three points at home, losing ground to Man City in the title raceJoseakicheki mechi


 


Maelfu waliachwa bila makao kutokana na vita Sudan Kusini
Serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa itawafungulia mashitaka wahusika wakuu wa njama ya mapinduzi dhidi ya serikali ya Rais Salva Kiir.
Serikali ya Kiir, imesema kuwa njama hiyo ndiyo iliyosababisha mapigano kati ya serikali na waasi waliokuwa wanaongozwa na Riek Machar.
Baadhi wanahofia kuwa hatua hii huenda ikasababisha uhasama zaidi na kutishia mkataba wa amani kati ya waasi na serikali.
Pande zote mbili kwenye mgogoro wa Sudan Kusini zilitia saini mkataba wa kusitisha vita Ijumaa iliyopita, lakini vita vimepungua tu bali havijasitishwa.
Duru zinasema makabiliano yangali yanaendelea huku zaidi la watu 800,000 wakilazimika kutoroka makwao.
Mkuu wa misaada katika Umoja wa Mataifa,Valerie Amos, anakamilisha ziara yake ya siku tatu nchini humo ambako ameshuhudia vita na uhalifu dhidi ya binadamu.
Wanaume wanne waliozuiliwa watafikishwa mahakamani na wengine watatu akiwemo Riek Machar, pamoja na mjumbe mmoja wa amani kutoka upande wa waasi,Taban Deng -- aliyetia saini mkataba wa amani watakabiliwa na sheria watakapokamatwa.
Rais Kiir alimtuhumu Machar pamoja na waliokuwa maafisa wa serikali kwa kupanga njama ya mapinduzi dhidi ya serikali yake baada ya mapigano kuzuka mjini Juba mwezi Disemba mwaka jana.
Maafisa 11 wa zamani walikamatwa wakati Machar aliyepinga kupanga njama ya mapinduzi akitoroka.
Makabiliano mapya yameripotiwa kutokea katika jimbo la Unity karibu na anakotoka bwana Machar.
Wafanyakazi wa misaada wamesema kuwa wanakabiliwa na wakati mgumu na kuwa wanahitaji msaada zaidi kuwasaidia waathiriwa wa mapigano hayo.

Image
Umoja wa Mataifa umesema idadi ya raia wanaotafuta hifadhi katika kambi zake nchini humo inazidi kupanda. Naibu wa msemaji wa umoja wa Mataifa Fahran Haq amewaambia waandishi wa habari kuwa kikosi cha kulinda amani cha umoja wa Mataifa kilichoko Sudan Kusini, UNMISS, kimeripoti kuzorota kwa hali ya usalama katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Unity ambako kuna viwanda muhimu vya mafuta na mapigano ya mara kwa mara yameripotiwa kati ya wanajeshi na waasi wanaomuunga mkono aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar. Haq amesema idadi ya watu waliopewa hifadhi katika kambi za Umoja wa Mataifa kote nchini humo imeongezeka na kufikia watu 79,000 kutoka idadi ya awali ya 76,000. Nusu ya idadi hiyo iko kazika kambi mbili za Umoja wa Mataifa mjini Juba.
Raia wengi wa Sudan Kusini wanaendelea kutoroka nchini humo kutokana na hofu kwamba makubaliano ya kusitisha vita huenda yasitekelezwe. Huyu hapa ni mmoja wa raia wanaoishi katika kambi ya wakimbizi nchini Uganda. "Bado kuna dalili za kuendelea mapigano, licha ya muafaka wa kusitisha mapigano. Serikali haitaki kuwapa waasi nafasi yoyote, nao waasi wanataka madaraka, na watajaribu wawezavyo kujipanga upya na kushambulia. Kwa hivyo kuna hofu mapigano yanaweza kuanza tena"
Takribani watu 47,000 wamepewa hifadhi nchini Uganda na msemaji wa Shirika la Kuwashughulikia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa nchini Uganda Lucy Beck anasema hali ni mbaya katika kambi hizo."Kufikia jana walikuwa karibu 197, lakini wale wanaowasili ni wanyonge baada ya kusafiri kwa muda mrefu bila pesa za kutosha. duru nchini Sudan Kusini zinasema kuna watu wengi ambao hawajafanikiwa kufika Uganda, au wangali njiani".
Mkuu wa shirika la misaada ya kibinadaaamu wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos ambaye hapo jana alizuru mji wa Malakal amesema uhalifu wa kivita umefanyika Sudan Kusini na kuongeza kuwa watu aliozungumza nao wamepoteza kabisa imani na wanataka kuhamishwa hadi maeneo mengine nchini humo au hata katika nchi nyingine. Mashirika ya kutoa misaada nchini humo yamesema kiasi ya watu 10,000 wameuawa katika mzozo huo ulioanza tarehe 15 mwezi uliopita.
Na wakati hali ikiendelea kuwa tete nchini humo, Waziri wa sheria wa Sudan Kusini Paulino Wanawilla Unago amesema kuwa kiongozi wa waasi Riek Machar na wenzake sita wanastahili kushtakiwa kwa makosa ya uhaini kuhusiana na jukumu lao katika umwagaji damu uliofanywa nchini humo. Waziri huyo amesema wanasiasa wengine saba waliokamatwa baada ya vurugu kuzuka, wataachiliwa huru, ikiwa ni mojawapo ya masharti ya waasi katika meza ya mazungumzo.
Miongoni mwa wale waliowekwa kizuizini ni Pagan Amum, ambaye alikuwa katibu mkuu wa chama tawala, aliyekuwa waziri wa usalama wa taifa Oyai Deng Ajak, balozi wa zamani nchini Marekani Ezekiel Lol Gatkuoth na aliyekuwa naibu waziri wa ulinzi Majak D'Agoot.

Image
Tayari kikosi cha umoja wa Ulaya kimepewa ruhusa na Umoja wa mataifa ya kwenda Jamhuri ya Afrika Kati ili kuwalinda raia.Kwenye azimio lililopitishwa kwa kauli moja na wanamemba 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa ni kwamba viongozi wa makundi yaliohusika na ukiukaji wa haki za binaadamu wataekewa vikwazo na Umoja huo.Taarifa kamili na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo . Kusikiliza taarifa hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Wanajeshi wa DRC walisaidiana na vikosi vya UN kupambana na waasi wa M23
Mjumbe maalum wa Marekani katika Maziwa makuu,amesema kuwa hali ya usalama katika eneo hilo inaendelea kuimarika, baada ya waasi wa kundi la M23 kukubali kusalimisha silaha mwezi Novemba.
Akiongea baada ya ziara yake ya siku tisa nchini humo, Russell Feingold alisema kuwa baada ya M23 kukubali kusitisha vurugu hizo za zaidi ya mwaka mmoja, makundi mengine ya waasi pia yalihitaji kusalimisha silaha zao.
Lakini ameongeza kuwa wakati changamoto nyingi bado zipo, nchi hiyo imepiga hatua ya kwanza katika kuimarisha hali ya usalama nchini humo.
Wakati huohuo, mapigano makali yameibuka Jumanne,kati ya jeshi la serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo na waasi wa ADF.
Kufuatia mapigano hayo vijiji vya Amisi na Nadwui vilivyokuwa ngome za waasi wa ADF vimechukuliwa na vikosi vya serikali.
Vijiji hivyo viko kilometa takriban 100, kutoka mji wa Beni.
Wakazi wa maeneo hayo wamefurahia kurejeshwa kwa vijiji hivyo mikononi mwa jeshi la serikali.

Mechi kati ya Liverpool na Everton
Klabu ya Liverpoool inaendeleza kampeni yake ya kutaka kuwa miongoni mwa timu nne bora katika Ligi Kuu ya England baada ya kuichachawiza Everton mabao 4-0 katika mchuano wa katikati ya juma ulioandaliwa Jumanne katika uwanja wa Anfield.
Mechi hiyo ilitajwa kama muhimu zaidi kuwahi kushirikisha pande hizo mbili baada ya kipindi cha miaka 30.
Liverpool ilitangulia kuzibusu nyavu za Everton mapema kuvuna mabao matatu; moja kupitia mkwaju wa kichwa kutoka kwa Steven Gerrad na huku Daniel Sturrige akifuma mabao mawili dakika tatu baadaye..
Everton ilipata pigo baada ya mshambulizi wa kutegemewa Romelu Lukaku kuondoka uwanjani juu ya machela baada ya kupata jeraha la kiwiko cha mguu. Aligongwa vibaya na Gareth Barry alipokuwa akijaribu kumnyima Steven Gerrard fursa ya kufunga bao.
Rodgers apongeza "juhudi kuu" za Liverpool
Ushindi huo mnono wa Liverpool tangu November 1982 umekiwezesha kikosi hicho cha Brendan Rogers kujipiga kifua juu ya matumaini ya kulidaka taji la ligi kuu. Brendan Rogers amesifu juhudi kubwa za wachezaji wake.
Katika matokeo ya mechi nyinginezo Manchester United iliishinda Cardiff mabao 2-0, Norwitch City na New Castle United zikatoka sare ya kutofungana, nao viongozi wa ligi Arsenal wakapata pigo katika kampeni yao kwa kulazimishwa kutoka sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya Southampton.
Swansea iliichabanga Fulham 2-0, Crystal Palace 1 Hull 0 na Liverpool.
Leo Jumatano Manchester City itashuka dimbani ugenini kutafuta alama za kushika usukani kwenye jedwali dhidi ya Totteham Hotspurs, Aston Villa watamenyana na West Brom, Chelsea itaialika West Ham, Sunderland itaikaribisha Stoke.

UNAMFAHAMU ASKOFU ANAEISHI KAMA RAIS HAPA BONGO??!!.. MSAFARA WAKE UNAGHARIMU ZAIDI YA SHILING MILIONI 200


Maisha ya Askofu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako, Geor Davie anayevuma zaidi jijini Arusha na Dar es Salaam ni ya kifahari, anaabudiwa zaidi ya manabii na analindwa kuliko marais mbalimbali duniani.

Davie ambaye hujulikana zaidi kwa jina la Mtume, ana msafara mrefu kwenye ziara zake anazokwenda kutoa huduma ambao husheheni magari mengi ya kifahari kuliko marais wengi.
OneloveTz tuna mlolongo wa matukio ya Davie ambayo yanajieleza kwa picha ambazo zinabainisha namna mtumishi huyo wa Mungu anavyokula bata.

MSAFARA WA SHS. MIL. 200
Matukio yanaonesha kuwa, baadhi ya misafara ya Davie imekuwa na msururu mrefu wa magari ambayo hayapungui kumi.

Uchunguzi umeonesha kuwa, magari hayo, kila moja linanunuliwa kati ya shilingi milioni 20 na 40, hivyo thamani ya ‘mikoko’ peke yake inaleta wastani wa jumla ya zaidi ya shilingi milioni 200 bila ya mafuta ambayo nayo hugharimu fedha nyingi.

ULINZI DAH!
Kila sehemu ambayo Davie hufika kwa lengo la kutoa huduma, huzungukwa na walinzi kati ya nane na 10 ambao huvaa nadhifu, suti nyeusi na miwani nyeusi.

Walinzi hao, humzunguka Davie na kufanya anapotembea asikaribiwe na watu kwa urahisi, huku wakimuongoza hatua kwa hatua.

Habari zinadai kuwa walinzi hao wameajiriwa na Kanisa la Huduma ya Ngurumo ya Upako na hulipwa mishahara kwa ajili ya kumlinda kiongozi huyo.

GARI LAKE LINA BENDERA MBILI
gari la Davie ambalo hupambwa na bendera mbili kama ilivyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa kawaida, gari la rais hupambwa na bendera mbili, moja ikiwa ya taifa na nyingine ya rais.
Hata hivyo, blog hii halijapata ufafanuzi kuhusu bendera mbili za gari la Davie, ingawa waumini wake wanasema kwamba ni alama ya huduma ya kanisa lake.

NI RED CARPET KILA ANAPOKWENDA
Davie anaheshimiwa kwa kiasi kikubwa na waumini wa huduma ya kanisa lake, hivyo hutandikiwa zulia jekundu ‘red carpet’ kila anapokwenda kutoa neno, huku akizungukwa na walinzi wake.

FULL KUABUDIWA
Neno la Davie siyo tu kwamba linampa wafuasi bali pia kwa wengine humuabudu kwa imani kuwa amejaliwa ufunuo mkubwa wa matatizo ya binadamu aliopewa na Mwenyezi Mungu.
blog hili lina picha za watu wakisujudu na kumshika viatu kwa imani kwamba tendo hilo huwapa utakaso wa kiroho na matatizo mbalimbali.


UNAMFAHAMU ASKOFU ANAEISHI KAMA RAIS HAPA BONGO??!!.. MSAFARA WAKE UNAGHARIMU ZAIDI YA SHILING MILIONI 200


Maisha ya Askofu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako, Geor Davie anayevuma zaidi jijini Arusha na Dar es Salaam ni ya kifahari, anaabudiwa zaidi ya manabii na analindwa kuliko marais mbalimbali duniani.

Davie ambaye hujulikana zaidi kwa jina la Mtume, ana msafara mrefu kwenye ziara zake anazokwenda kutoa huduma ambao husheheni magari mengi ya kifahari kuliko marais wengi.
OneloveTz tuna mlolongo wa matukio ya Davie ambayo yanajieleza kwa picha ambazo zinabainisha namna mtumishi huyo wa Mungu anavyokula bata.

MSAFARA WA SHS. MIL. 200
Matukio yanaonesha kuwa, baadhi ya misafara ya Davie imekuwa na msururu mrefu wa magari ambayo hayapungui kumi.

Uchunguzi umeonesha kuwa, magari hayo, kila moja linanunuliwa kati ya shilingi milioni 20 na 40, hivyo thamani ya ‘mikoko’ peke yake inaleta wastani wa jumla ya zaidi ya shilingi milioni 200 bila ya mafuta ambayo nayo hugharimu fedha nyingi.

ULINZI DAH!
Kila sehemu ambayo Davie hufika kwa lengo la kutoa huduma, huzungukwa na walinzi kati ya nane na 10 ambao huvaa nadhifu, suti nyeusi na miwani nyeusi.

Walinzi hao, humzunguka Davie na kufanya anapotembea asikaribiwe na watu kwa urahisi, huku wakimuongoza hatua kwa hatua.

Habari zinadai kuwa walinzi hao wameajiriwa na Kanisa la Huduma ya Ngurumo ya Upako na hulipwa mishahara kwa ajili ya kumlinda kiongozi huyo.

GARI LAKE LINA BENDERA MBILI
gari la Davie ambalo hupambwa na bendera mbili kama ilivyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa kawaida, gari la rais hupambwa na bendera mbili, moja ikiwa ya taifa na nyingine ya rais.
Hata hivyo, blog hii halijapata ufafanuzi kuhusu bendera mbili za gari la Davie, ingawa waumini wake wanasema kwamba ni alama ya huduma ya kanisa lake.

NI RED CARPET KILA ANAPOKWENDA
Davie anaheshimiwa kwa kiasi kikubwa na waumini wa huduma ya kanisa lake, hivyo hutandikiwa zulia jekundu ‘red carpet’ kila anapokwenda kutoa neno, huku akizungukwa na walinzi wake.

FULL KUABUDIWA
Neno la Davie siyo tu kwamba linampa wafuasi bali pia kwa wengine humuabudu kwa imani kuwa amejaliwa ufunuo mkubwa wa matatizo ya binadamu aliopewa na Mwenyezi Mungu.
blog hili lina picha za watu wakisujudu na kumshika viatu kwa imani kwamba tendo hilo huwapa utakaso wa kiroho na matatizo mbalimbali.

- See more at: http://onelovetz.blogspot.com/2014/01/unamfahamu-askofu-anaeishi-kama-rais.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+blogspot%2FhgdRs+%28Onelove+Tz%29&utm_content=FaceBook#sthash.a37k9DV2.dpuf
- See more at: http://onelovetz.blogspot.com/2014/01/unamfahamu-askofu-anaeishi-kama-rais.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+blogspot%2FhgdRs+%28Onelove+Tz%29&utm_content=FaceBook#sthash.a37k9DV2.dpuf

waliotembelea blog