Wednesday, July 30, 2014

IMG-20140727-WA0011
Pichani ni Miss Tanzania USA 2014, Joy Kalemera katika pozi kabla ya mahojiano na Mtangazaji wa kipindi cha “Mimi na Tanzania” Hoyce Temu nchin Marekani.
Mpigie Kura Miss Tanzania USA, Joy Kalemera anayeshiriki kinyang’ayiro cha kumtafuta Miss Africa USA. Mtangazaji wa Mimi Na Tanzania Hoyce Temu ambaye pia ni Miss Tanzania 1999 yupo nchini Marekani na amefanya mahojiano na mrembo huyo.
Usikose kuangalia marudio ya mahojiano hayo kwenye kipindi cha “Mimi na Tanzania” Jumamosi ya tarehe 2 August ,2014 Saa saba mchana katika kituo cha Televisheni cha Channel Ten.
IMG-20140727-WA0013
Miss Tanzania 1999 ambaye pia ni Mtangazaji wa kipindi cha “Mimi na Tanzania” Hoyce Temu akipata ukodak na Miss Tanzania USA, Joy Kelemera baada ya mahojiano maalum nchini Marekani.
Joy Kelemera
Namna ya kushiriki kumpigia kura moja kwa moja kwenye profile yake Bonyeza hapa utakuwa umeingia kwenye profile ya Joy Kalemera na bonyeza kitufe chenye alama ya mkono (sehemu iliyozungushiwa duara na wino mweusi) na moja kwa moja utakuwa umempigia kura Mtanzania mwenzetu anayeiwakilisha vyema nchini yetu kwenye kinyan’ganyito hicho.
NOTE: Unaweza kupiga kura mara nyingi uwezavyo kila baada ya dakika mbili kwa kubofya sehemu ile ile.
Let us all wish her all the best! Ushindi wake ni wa Nchi! Piga Kura Sasa!
IMG-20140727-WA0014
Pichani ni Hoyce Temu, Joy Kalemera na camera crew/IskaJojo studios (katikati) aliyefanikisha kukerokodi maojiano hayo.
IMG-20140727-WA0015
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu na Miss Tanzania USA 2014, Joy Kalemera katika pozi za madaha.

DSC_0011
Sam Mapenzi (katikati) akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band ndani ya fukwe za Escape One katika show maalum kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid-El Fitr huku akipewa back Vocal na Sony Masamba pamoja na Aneth Kushaba AK47.
DSC_0015
Aneth Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani kuwapa raha mashabiki wa Skylight Band katika kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwenye ukumbi wa Escape One.
DSC_0306
Mashabiki wa Skylight Band mdogo mdogo wakiachia kwenye dancing floor.
DSC_0243
Sam Mapenzi akitoa burudani adimu mashabiki wa Skylight Band katika sikukuu ya Eid El Fitr kwenye kiota cha Escape One jijini Dar.
DSC_0237
Skylight Band ni #balsaa# hebu angalia mashabiki wanaojua burudani ya muziki wa Live wanavyosebeneka.
DSC_0189
Rappa Mkongwe Joniko Flower akitunzwa wekundu wa msimbazi na mmoja wa mashabiki wa Skylight Band aliyekunwa na uimbaji wa rapa huyo.
DSC_0018
Binti mwenye sauti ya kumtoa Nyoka pangoni Mary Lucos akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani).
DSC_0466
Mary Lucos wa Skylight Band akiwaduarisha mashabiki wa bendi hiyo katika sikukuu ya Eid El Fitr ndani kiota cha Escape One.
DSC_0487
Wadada wakijipinda kuzungusha nyonga zao.
DSC_0471
DSC_0139
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakiduarika.
DSC_0159
DSC_0023
Pichani juu na chini ni sehemu ya umati wa wakazi wa Dar wake kwa waume waliokusanyika ndani ya fukwe za Escape One kujipatia upepo mwanana huku wakiburudishwa na Skylight Band.
DSC_0024
DSC_0028
Mashabiki wa Skylight Band wakiendelea kuburudika na vinywaji mbalimbali huku wakisiliza burudani ya kutoka bendi ambayo kwa sasa ndio habari ya mujini.
DSC_0077
DSC_0337
Ale Mama mupe Saluti……!!! Twende kazi…..
DSC_0355
Muguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma….Yachuma chuma…!! Kikosi cha Skylight Band wakicheza sambamba na mashabiki wao katika kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwenye kiota cha Escape One.
DSC_0356
DSC_0388
Burudani ikiendelea na watu wakiendelea kusebeneka.
DSC_0401
Wadada walichizikaje…!?
DSC_0514
DSC_0411
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakionyesha umahiri wao wa kucheza moja ya staili za bendi hiyo kwa wanamuziki Joniko Flower na Sony Masamba.
DSC_0420
DSC_0235
Daudi Tumba akitweta jasho kuhakikisha mashabiki wa Skylight Band wanapata ladha nzuri ya muziki kupitia ala za Band hiyo huku Tumba ikihusika pia kutengeneza sauti nzuri kabisa.
DSC_0274
Pichani juu na chini ni Hashim Donode a.k.a Mzee wa Viduku akifanya yake!
DSC_0310
DSC_0069
Afisa Mtendaji Mkuu wa Skylight Band, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bendi hiyo Justine Ndege wakati Skylight Band ikiendelea kutoa burudani kwenye sherehe za sikukuu ya Eid -El- Fitr ndani ya kiota cha Escape One.
DSC_0217
Blogger William Malecela a.k.a LEMUTUZ mwandaaji wa Instagram Party itakayofanyika Jumamosi hii kwenye kiota cha Escape One akishow love na Fans wake mdau Joseph Magige.
DSC_0437
Sam Mapenzi kwenye ukodak na Customer care huku akionyesha Video mpya ya “Pasua Twende” kupitia simu yake ya kiganjani.
DSC_0394
Emma Bass wa Skylight Band (kulia) akipata ukodak na swahiba wake.
DSC_0379
Joniko Flower wa Skylight Band akishow love na mdau.
DSC_0296
Mratibu wa Skylight Band Lubea akipata ukodak na Mwimbaji Mary Lucos back stage.
DSC_0002
Mkurugenzi Mtendaji wa Skylight Band na Rais wa #WANAMANYOYA# Justine Ndege (katikati) akipata Ukodak Mkuu wa Itifaki wa #WANAMANYOYA# Eddie Viede pamoja na mdau wa Skylight Band James Rock Mwakibinga.
DSC_0228
Palinogaje wewe tu umekosekana….Si haba kesho pia ni siku tukutane viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0256
DSC_0251
Aneth Kushaba AK 47 a.k.a Komando Kipensi akishow love na Tophy mpiga bass wa Skylight Band back stage.

images
NA Mahmoud Ahmad Arusha
WANACHAMA wa vikundi vya kuweka na kukopa (VIKOBA) mkoani Arusha wametakiwa kutumia na kupanga vizuri matumizi ya fedha wanazokusanya ili ziwasaidie kutoka daraja moja hadi jingine katika maisha yao.
Kauli hiyo ilitolewa  wilayani Arusha na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha  
alipokuwa akiendesha utunishaji wa fedha kwa Umoja wa Wanavikoba wa Kata ya Engutoto yenye vikundi 20 na wanachama 600.
Katika utunishaji huo, Namelok alichangia Sh. Milioni 10 huku kiasi cha Sh. Milioni 12 kikipatikana katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Umoja wa Wanawake UTW wilayani Monduli.
Akizungumza na wanavikundi hao Mbunge Namelok aliwataka wanawake kujitokeza na kujiunga katika vikundi huku akiwataka kuacha kuogopa kufanya shughuli za ujasiriamali.
“Wanawake nawaomba sana muendelee kujitokeza na kujiunga katika Vikoba kwani huku ndipo eneo ambalo litatuwezesha tuwe na sauti ya kujitegemea kimapato.
“Lakini pia naomba niwakumbushe jambo muhimu hizi fedha tunazokusanya nawaomba sana muonyeshe mfano wa kuzitumia vizuri ili kesho zitusaidie kutoka daraja moja kwenda daraja jingine katika maisha yetu,” alisema Namelok.
Kwa upande wake Katibu wa UWT Kata ya Engutoto Glory Emmanuel alisema wana vikundi wengi waliopo kwenye vikoba wanakabiliwa na changamoto ya elimu ya ujasiriamali.
“Tunaomba suala la ofisi za vikoba uliangalie kwani vikundi havina ofisini.Pia wanachama hawana elimu hatua inayosababisha kukopa na kutumia sivyo kutokana na kutokuwa na elimu ndogo ya biashara,” alisema Glory.
Naye mwana kikundi Zaituni Mwishehe alibainisha jinsi alivyonufaika na kuwa katika vikundi hivyo vya kuweka na kukopa ambapo hadi sasa ameweza kujitegemea katika matumizi ya kawaida ndani ya nyumba.
“Sasa hivi naweza kulipia michango midogomidogo ya mwanangu shuleni. Lakini pia hata kutatua matatizo mengine ya kifamilia kupitia mikopo ninayochukua kwenye kikundi bila hata kumsubiria mume wangu,” alisema Zaituni.

01 
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Getrudi Mpaka akitoa salam za Mkoa huo kabla ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Mjini Magharibi leo july 30.
02 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis, makabidhiano hayo yamefanyika uwanja wa ndege mkongwe Kiembesamaki leo. (Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).
03 
Vijana wa Chipkizi wakiimba wimbo ya Mwenge.
04 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame akishika mwenge wa Uhuru ulipowasili Zanzibar.
05 
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Hamza Ibrahim kutoka Mjini Magharibi na maaskari wakiukimbiza Mwenge.

 
Ajali mbaya imetokea eneo la Pandambili ikihusisha Basi la MOROBEST linalofanya safari za Mpwapwa – Dar
- Inadaiwa watu wengi wamepoteza maisha
Mtandao huu unafuatilia taarifa kutoka eneo la tukio.

waliotembelea blog