NA Mahmoud Ahmad Arusha
WANACHAMA wa vikundi vya kuweka
na kukopa (VIKOBA) mkoani Arusha wametakiwa kutumia na kupanga vizuri
matumizi ya fedha wanazokusanya ili ziwasaidie kutoka daraja moja hadi
jingine katika maisha yao.
Kauli hiyo ilitolewa wilayani Arusha na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha
alipokuwa akiendesha utunishaji wa fedha kwa Umoja wa Wanavikoba wa Kata ya Engutoto yenye vikundi 20 na wanachama 600.
Katika utunishaji huo, Namelok
alichangia Sh. Milioni 10 huku kiasi cha Sh. Milioni 12 kikipatikana
katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Umoja wa
Wanawake UTW wilayani Monduli.
Akizungumza na wanavikundi hao
Mbunge Namelok aliwataka wanawake kujitokeza na kujiunga katika vikundi
huku akiwataka kuacha kuogopa kufanya shughuli za ujasiriamali.
“Wanawake nawaomba sana
muendelee kujitokeza na kujiunga katika Vikoba kwani huku ndipo eneo
ambalo litatuwezesha tuwe na sauti ya kujitegemea kimapato.
“Lakini pia naomba niwakumbushe
jambo muhimu hizi fedha tunazokusanya nawaomba sana muonyeshe mfano wa
kuzitumia vizuri ili kesho zitusaidie kutoka daraja moja kwenda daraja
jingine katika maisha yetu,” alisema Namelok.
Kwa upande wake Katibu wa UWT
Kata ya Engutoto Glory Emmanuel alisema wana vikundi wengi waliopo
kwenye vikoba wanakabiliwa na changamoto ya elimu ya ujasiriamali.
“Tunaomba suala la ofisi za
vikoba uliangalie kwani vikundi havina ofisini.Pia wanachama hawana
elimu hatua inayosababisha kukopa na kutumia sivyo kutokana na kutokuwa
na elimu ndogo ya biashara,” alisema Glory.
Naye mwana kikundi Zaituni
Mwishehe alibainisha jinsi alivyonufaika na kuwa katika vikundi hivyo
vya kuweka na kukopa ambapo hadi sasa ameweza kujitegemea katika
matumizi ya kawaida ndani ya nyumba.
“Sasa hivi naweza kulipia
michango midogomidogo ya mwanangu shuleni. Lakini pia hata kutatua
matatizo mengine ya kifamilia kupitia mikopo ninayochukua kwenye kikundi
bila hata kumsubiria mume wangu,” alisema Zaituni.
0 maoni:
Post a Comment