Monday, July 8, 2013



MATUKIO YA TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI TAIFA 

 

Baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo katika Tamasha la Usiku wa Matumaini Taifa jana.

 
Msaada kwenye tuta kuhusiana na hii style bado mimi sijaielewa wewe je?

 
Kombe lililokuwa linawaniwa na wabunge wa Yanga na Simba...
Msanii Mboto akicheza kiduku kutokana na wimbo uliokuwa unaimbwa na mzee Yusuph, Msanii huyu jana alicheza sana kiduku mpaka watazamaji wakaacha kumsikiliza mc na kuanza kumshangilia yeye kitendo kichomfanya mshereheshaji huyo kumuomba aache kucheza kwanza..

Wasanii M 2the P akiwa na Bright Job nao wachezaji wa timu ya Bongo Flava baada ya kumaliza mechi yao na Bongo muvi..wakiwa wamevalia matishirt yenye ishara ya kumuenzi msanii mwenzao Mangwea aliyefariki mwishoni mwa mwezi May huko Afrika ya Kusini, pia wasanii wote wa Bongo flava walivalia matisht hayo yaliyoandikwa R.I.P Ngwea

Mchizi Mox, M 2the P na Bright Job Taifa...

Washereheshaji Stive Nyerere  na Mkweli uwanja wa Taifa jana...


Baadhi ya watu waliohudhuria Tamasha la Usiku wa matumaini




 Shangwe baada ya kupata ushindi.....

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

WAFUASI WA RAIS ALIYEPINDULIWA MORSI WAUAWA NCHINI MISRI. 

 




 MAAFISA wa Afya Misri wamesema takriban watu 42 wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Cairo nje ya kambi ya kijeshi ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi walikua wamekusanyika na wanaamini anazuiliwa hapo. Watu wengine 300 wamejeruhiwa.

Kundi la Muslima Brotherhood limewataka raia wa Misri kuwapinga wale linawaita wanaopokonya raia uhuru na demokrasia. 

Brotherhood imelaumu jeshi kwa kuwaua raia wake.
Katika kikao na waandishi wa habari, wafuasi hao walimlaani vikali mkuu wa jeshi Abdel Fattah Al-Sisi na kumtaja kama muuaji aliyewashambulia raia wenzake.

Haya yanajiri huku ghasia zikiendelea baada ya kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi.

Waandamanaji hao wanasema vikosi maalum viliwafyatua risasi baada ya swala ya fajir huku wengine wakishambuliwa walipokusanyika nje ya makao ambako bwana Morsi anadhaniwa kuzuiliwa wakitaka watawala kumwachilia huru.


 Msemaji wa chama cha Muslim brotherhood amesema kuwa idadi ya waliofariki katika ghasia hizo imefikia 30 huku zaidi ya watu 500 wakijeruhiwa.

Lakini katika taarifa yake, jeshi la nchi hiyo limesema kuwa kundi moja la kigaidi lilikuwa likijaribu kuing
ia katika kambi hiyo na kumuua mwanajeshi mmoja.

Limeongezea zaidi ya watu 200 walitiwa mbaroni wakimiliki silaha kama vile visu.

Duru kutoka wizara ya afya zilisema kuwa afisaa mmoja wa jeshi aliuawa.

Bwana Morsi, aliyekuwa rais wa kwanza wa kiisilamu kuchaguliwa kidemopkrasia Misri, aling'olewa mamlakani na jeshi, siku ya Jumatano baada ya kufanyika maandamano makubwa.

Mmoja wa waandamanaji Mahmud al-Shilli, aliambia shirika la habari la AFP kuwa wanajeshi waliwarushia gesi ya kutoa machozi lakini kikundi cha wanaume waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia ndio waliwafyatulia risasi.

Katika taarifa iliyosomwa kwenye vyombo vya yhabari vya serikali, jeshi lililaumu kikundi cha watu wlaiokuwa wamejihami ambao limesma ni mgaidi waliokuwa na njama ya kuvamia kambi ya jeshi.
BBC.

 

 

 

MWANAFUNZI WA CHUO CHA VETA MKOANI DODOMA AJILIPUA KWA PETROL.....KISA NI WIVU WA MAPENZI ...!!




Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi (Veta) mkoani Dodoma, Taliki Juma, (22) amefariki dunia baada ya kujilipua kwa kutumia mafuta ya petroli na kujeruhi wengine nane.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 10.30 jioni Nzuguni eneo la Machaka, nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma Mjini.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Suzan Kaganda, jana alisema Taliki alijilipua katika saluni inayomilikiwa na Irene Mapunda inayojulikana kwa jina la Tonny Hair Dressing Saloon.

Alisema mwanafunzi huyo aliyekuwa akisomea fani ya ufundi magari, alienda kununua Petroli lita tano katika kituo cha Mafuta cha Nanenane na kuimwaga ndani ya chumba cha  Saluni ya Irene.


Watu waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini hawakufanikiwa kwani Taliki aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wote waliokuwa karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo,” alisema.


Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Mugina Hussein (32), Swaibu Kassimu (20), Easte Silau (30) na Fredrick Gabriel (21), wote wafanyabiashara na wakazi wa Nzuguni.


Wengine ni mwanafunzi wa darasa la nne Benson Mushi (11), Japhet Japhet (18), Meshack John (18) na mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya City, Shaban Pili (20).

Alisema majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambapo nane wamelazwa wodi namba moja ya wanaume na mmoja amelazwa wodi namba 10 ya wanawake.

Kaganda alisema tathimini ya hasara iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika.

Aidha, alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa, chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi.

Hata hivyo, alisema  Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili.


MUUGUZI WA ZAMU

Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Magreth Maki, alisema kuwa Taliki alifariki jana katika hospitali hiyo kutokana na majeraha makubwa aliyopata wakati wa tukio hilo.

Hata hivyo, alisema hali ya majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo wanaendelea vizuri isipokuwa mmoja ambaye bado hali yake si nzuri.

“Bado wanaendelea kutibiwa vidonda walivyovipata kutokana na tukio hilo, hali yao inaendelea vizuri isipokuwa mmoja ambaye hali yake ni serious (mbaya), “alisema Muuguzi huyo wa zamu.

 




Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya City mjini Dodoma, Shaban Pili (18), akiwa katika wodi namba moja katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Shaban ni mmoja wa majeruhi walioungua moto katika tukio la mwanfunzi wa Chuo cha Veta Dodoma kujilipua na kufariki Dunia lilitokea Nzuguni eneo la Machaka nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 
MAJERUHI WANENA
Akizungumza na NIPASHE, baba mzazi wa Benson Mushi, Dickson Mushi, alisema kuwa mwanae alikumbana na mkasa huo alipokwenda kupeleka nguo zake kwa ajili ya kunyoosha.


“Mwanangu alikwenda karibu na saluni hiyo kwa ajili ya kwenda kunyoosha nguo zake ndipo alipokutana na mkasa huu. Amekuwa na kawaida ya kwenda kuonyoosha karibu na saluni hiyo,”alisema Mushi alipokuwa akizungumza na gazeti hili nje ya wodi.


Kwa upande wake, majeruhi mwingine Shaban Pili, alisema alikumbwa na mkasa huo katika jitihada za kumuokoa marehemu baada ya kusikia kelele za kuomba msaada kutoka kwa wafanyabiashara waliopo jirani na saluni hiyo.

“Tuliangaika kuvuta mlango wa saluni na tukafanikiwa, tulipomuuliza kulikoni amejimwagia petroli, alitujibu kuwa tumwache lakini ghafla aliwasha kiberiti na kujilipua,”alisema na kuosha mkono aliungua sana wakati alipokuwa akimvuta marehemu nje ya saluni hiyo.

Naye majeruhi Meshack John, alisema alikuwa amekaa karibu na saluni hiyo, ndipo alipokuja marehemu (mtoto wa baba yake mdogo) na kumuomba ampatie Sh. 15,000.

“Nilimuuliza ya nini? Akanijibu kuwa baba kanituma (baba yake mdogo ambaye ni mmliki wa bucha analouza nyama katika eneo la Nzuguni), nikakataa na kuwaomba ushauri wenzangu kama nimpatie ama la,”alisema.

Hata hivyo, baada ya mashauriano ya muda mrefu akaamua kumpatia kiasi hicho cha fedha na akaondoka zake na kwenda kununua mafuta ya petroli lita tano.

Alisema baadaye alirejea na lita tano za mafuta na kisha kujifungia ndani ya saluni kabla ya kujimwagia.

“Akajimwagia, mama mmoja naye amelazwa hapa hapa, akasema Taliki anajiwasha huko moto naona mafuta yanatiririka huku nje,”alisema.

Alisema hali hiyo ilisababisha wasogeze mlango wa saluni na kabla hawajachukua hatua moto ukaanza kuwaka.
 

“Tulikuwa majeruhi tisa lakini mwenzetu Taliki alifariki dunia leo asubuhi kwa kuwa yeye alijimwagia mafuta kabla kujilipua moto,”alisema.


Kwa upande wa chanzo la tukio hilo, alisema kuwa marehemu alikuwa na ugomvi na wenzake ambao aliwashutumu kwamba wanamtangazia kuwa anauhusiano wa kimapenzi na mmiliki wa saluni hiyo (Irene).

“Walikuwa wanamtangazia kuwa amekuwa akimhonga (mmiliki wa saluni) pesa…Ijumaa walipigana sana  na wenzake hadi alirudi nyumbani kuchukua panga akitaka kuja kuwakatakata wenzake akidai kwanini wampakazie jambo ambalo halina ukweli,”alisema.

Majeruhi huyo alisema ilimbidi kwenda kuamulia ugomvi huo na ukaisha lakini alishangaa tena juzi marehemu aliamua kuchukua uamuzi huo.

Naye Silau, aliyelazwa wodi namba 10, alisema  alikuwa akifanya biashara karibu na saluni hiyo ndipo moto ulipomrukia na kumuunguza mikononi.


“Mimi nilisikia harufu ya mafuta ya petroli na kuwaambia wenzangu kuwa nasikia harufu katika saluni hiyo lakini sikusogea karibu,”alisema Silau.
 
MASHUHUDA
Mashuhuda wa tukio hilo ambao hawakutaka majina yao kuandikwa gazetini walisema kuwa marehemu huyo alipelekwa hospitali akiwa ameungua vibaya kiasi cha ngozi yote kuchunika.

“Marehemu alikuwa akilalamika maumivu, akisema  anatamani kufa mapema maana maumivu ni makali sana,”alisema mmoja wa shuhuda wa tukio hilo.




















































IRENE UWOYA AMWAGIWA MATUSI YAA NGUONI NA MASHABIKI WA BONGO FLEVA BAADA YA KUMFANANISHA 'DIAMOND PLATINUMZ' NA 'MICHAEL JACKSON'...!!




MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya, amelowa mvua ya matusi baada ya kumfananisha mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na aliyekuwa mwanamuziki mkubwa duniani, marehemu Michael Jackson.
Wikiendi iliyopita, Uwoya aliandika kwenye ukurasa wake katika mtandao wa Instagram kuwa msanii huyo anayefanya vizuri katika Bongo Fleva ndiye staa atakayemrithi mkali huyo wa Pop, maandishi ambayo yalizua matusi hayo ya nguoni.
Baadhi ya mashabiki wa mastaa hao walitoa maoni kuwa jambo hilo ni sawa na kufananisha vitu ambavyo havina uwiano hasa ukizingatia Michael Jackson alishafariki dunia Juni 25, 2009.
“Sasa hiyo ni akili gani ya ki…(tusi) kumfananisha mtu aliyeko hai na marehemu?” alihoji Mishish, mmoja wa mashabiki wa Uwoya katika mtandao wa Facebook baada ya ishu hiyo kuwa gumzo mitandaoni.

“Kweli wewe Irene (Uwoya) ni …(tusi) au kwa sababu Diamond amesha…(tusi) ndiyo maana unamsifia kiasi hicho,” aliandika shabiki mwingine kwenye Twitter na kupisha wengine kuendelea kumporomoshea Uwoya matusi ya nguoni










waliotembelea blog