Mabingwa
Watetezi wa International Champions Cup, Manchester United, Mwezi Julai
huko USA watakuwa na kazi ya kutetea Taji lao walilotwaa Mwaka Jana
wakati Mashindano haya yatakapochezwa tena yakishirikisha Vigogo wa
Ulaya.
Zipo Timu 10, wakiwemo Mabingwa Man United, ambazo zitashiriki na nazo ni Barcelona, Chelsea, PSG, Porto na Fiorentina, kutoka Ulaya pamoja na Klabu ya Mexico, Club America, na Klabu za Marekani New York Red Bulls, LA Galaxy na San Jose Earthquakes.
Mashindano hayo ya ICC yanatarajiwa kuanza Julai 11 na kumalizika Agosti 5 kabla tu ya Misimu mipya ya 2015/16 kuanza huko Ulaya.
Mwaka Jana kwenye Mashindano haya, Mechi kati ya Man United na Real Madrid, ambayo Man United walishinda 3-1, iliweka Rekodi huko Michigan, USA kwa kuhudhuriwa na Washabiki wengi mno ambapo Watu zaidi ya 109,000 walisheheni Uwanjani.Mwaka Jana, chini ya Kocha mpya Louis van Gaal, Man United iliitwanga Liverpool 3-1 kwenye Fainali na kubeba Kombe.
Kwenye Fainali hiyo, Liverpool walitangulia kwa Penati ya Steven Gerrard lakini Man United wakajibu kwa Bao 3 za Wayne Rooney, Juan Mata na Jesse Lingard.
Kwa kuelekea Fainali, ManUnited walizibwaga Klabu za Italy, AS Roma na Inter Milan, na kisha kuitwanga Real Madrid.
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI:
Chelsea
Manchester United
Barcelona
Club America
Fiorentina
LA Galaxy
New York Red Bulls
Paris Saint-Germain
Porto
San Jose Earthquakes