Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson ambaye alistaafu kuifundisha Man United baada ya kuitumikia kwa miaka 27. Ferguson alistaafu 2013 kukinoa kikosi hicho na kuendelea kusimamia miradi yake binafsi, Ferguson ameeleza sababu za Paul Pogba kuondoka Man United na kutokubali kusaini mkataba mpya.
Ferguson aliwahi kulaumiwa kwa kushindwa kumshawishi Paul Pogba abaki Man United na wengi walifikiri hakuwa katika mipango yake hivyo ndio maana alimuacha kama mchezaji huru ajiunge na Juventus 2012. Stori hii inakuja baada ya Ferguson kueleza kwa kina nini kilipelekea hadi Paul Pogba akaondoka klabu hiyo.
Stori ni kuwa Ferguson licha ya kutozijibu lawama zake za mwanzo kuhusu Pogba wakati ule, katika kitabu chake ameeleza kuwa moja kati ya watu waliyosababisha Paul Pogba aondoke Man United ni Mino Raiola ambaye ni wakala wa Paul Pogba.