Tuesday, May 6, 2014



Miss Dar City Center wakichezo show wakati wa onesho maalum la kuwatambulisha lililofanyika juzi jijini Dar es Salaam katika kiota cha Escape One.

Miss Dar City Center wakipozi jukwaani wakati wa kuwatambulisha lililofanyika juzi jijini Dar es Salaam katika kiota cha Escape One.

Miss Ubungo nao walikuwepo kuwasindikiza wenzao wa Dar City Center.

Miss Ukonga 2014 nao waliwasindikiza wenzao wa Dar City Center katika uzinduzi huo.

Miss Ukonga wakicheza show



Mambo ya zulia jekundu katika uzinduzi huo wa Miss Rad City Center


Mchezaji Chipukizi wa miaka 18 James Anthony Wilson aliifungia bao United katika dakika ya 31 baada ya Manchester United kupata frii kiki ambayo ilipigwa na Marouane Fellaini na hatimaye Dogo huyo Wilson kuachia shuti kali ambalo limezama hadi langoni mwa timu ya Hull City.New hero: James Wilson celebrates breaking the deadlock for Manchester United against HullBao!!!!!!James Anthony Wilson alivyoipachikia bao United na kufanya 1-0 kipindi cha kwanza1-0 bao la Wilson.
Bao pekee la Hull City lilifungwa na Fryatt katika Shuti lao pekee Golini.
Huenda Hull City, ambao wako Fainali ya FA CUP na watacheza na Arsenal Uwanjani Wembley hapo Mei 17, wakamkosa Mchezaji wao mzuri Meyler kwenye Fainali hiyo baada ya Mchezaji huyo kunaswa akimkanyaga Januzaj bila Refa kuona ikiwa FA, Chama cha Soka England, kitalipitia tukio hilo.
Jones akijiuguza chini baada ya kuumizwa bega JonesMapema Phil Jones aliumia baada ya kugongana na Figueroa na kuumia bega wakati wa kona.
Mpaka mapunziko United ndio wameenda kupumzika wakiwa mbele ya bao 1-0. 
James Anthony Wilson anaifungia bao dakika ya 61 kipindi cha pili na kufanya 2-0 baada ya Januzaj kukimbia na mpira mbele na kumpa pasi ili afunge Fellaini na kuchemka na mpira huo kutemwa na kipa na James Anthony Wilson kufunga bao hilo likiwa la pili kwake. Dakika chache tena United wamefanya makosa ya ukabaji na mchezaji wa Hull Matt Fryatt kufunga bao katika dakika ya 63 baada ya kutengewa mpira na George Boyd. 

Daklika ya 70 Giggs anaingia na anachukua nafasi ya Thomas Lawrence. Dakika ya 86 Robin van Persie anaipachikia bao la tatu Man United baada ya kukosa kosa bao kadhaa sasa anapachika bao na kufanya 3-1 dhidi ya Hull Bowing out: Nemanja Vidic goes up for a trademark header in his final appearance at Old TraffordVidic akiendesha leo hiiWilson akifunga bao baada ya kupokea mpira kutoka kwa  Fellaini
Wilson akishangilia bao lake kwa aina yake kulia ni Nemanja Vidic akimkimbilia kumpongeza.

Wilson akipeta baada ya kuifungia bao Manchester United

Robin van Persie akiosha! Bao la 3

Robin van Persie akishangilia bao lake

Mchezaji na Meneja: Ryan Giggs wakati anachukua nafasi ya Tom Lawrence kipindi cha pili dakika ya 70

VIKOSI:
Man Utd:
De Gea, Valencia, Jones, Smalling, Buttner, Carrick, Fellaini, Januzaj, Lawrence, Kagawa, Wilson. 
Subs: Mata, Giggs, Vidic, Young, van Persie, Keane, Amos.
Hull City: Jakupovic, Bruce, Davies, Figueroa, Elmohamady, Quinn, Koren, Meyler, Rosenior, Long, Boyd.
Subs: Huddlestone, Fryatt, Livermore, Jelavic, Sagbo, Harper, Faye.
Referee: Craig Pawson
 Nemanja Vidic na Ryan Giggs wakipasha
 James Wilson  wa Man United akipasha kabla ya mechi
 Tom Lawrence


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeazimia kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu Tanzania (TFF Development Trust Fund).
Uamuzi wa kuanzisha mfuko huo umepitishwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Mei 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo madhumuni yake ni kutafuta vyanzo vya rasilimali za kuendeleza programu za mpira wa miguu Tanzania.
Mfuko huo utakaokuwa chini ya uenyekiti wa Rais aliyepita wa TFF, Leodegar Tenga utatafuta rasilimali za kuendeshea michuano ya Taifa na kimataifa ya wavulana na wasichana kwa vijana wenye umri chini ya miaka 13, 15, 17 na 19.
Pia kuendeleza maeneo ya ardhi kote Tanzania ambayo ni mali ya TFF kwa kujenga vituo vya michezo (sports centres), kutafuta rasilimali za kutoa mafunzo kwa makocha, marefa, madaktari wa tiba ya michezo na viongozi (administrators).

Majukumu mengine ya mfuko huo ni kuagiza na kusambaza vifaa vya michezo hasa kwa watoto wadogo (grassroots) na vijana.

Mfuko huo utazinduliwa Oktoba 8 mwaka huu ambayo ni siku ya kilele cha Tanzania kutimiza miaka 50 ya uanachama wake katika Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Mbali ya Tenga, wajumbe wengine wanaounda bodi ya mfuko huo ni Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ayoub Chamshama, Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Fredrick Mwakalebela, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Tarimba Abbas na Mbunge wa Viti Maalum, Zarina Madabida.

MWINYI KAZIMOTO ATUA TAIFA STARS
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Al Markhiya ya Qatar, Mwinyi Kazimoto amewasili nchini kujiunga na kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Zimbabwe.

Kazimoto ambaye amewasili nchini jana (Mei 5 mwaka huu) anatarajia kusafiri leo (Mei 6 mwaka huu) kwenda Tukuyu mkoani Mbeya ambapo Taifa Stars imeweka kambi yake chini ya Kocha Mart Nooij kujiandaa kwa mechi hiyo.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager juzi (Mei 4 mwaka huu) ilicheza mechi ya kirafiki na Malawi (Flames) ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kuikabili Zimbabwe (Mighty Warriors). Mechi hiyo dhidi ya Flames ilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine na kumalizika kwa suluhu.

WACONGO KUCHEZESHA MECHI YA NGORONGORO HEROES
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kuchezesha mechi kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Nigeria.

Mechi ya mchujo kusaka tiketi ya kucheza Fainali za 19 za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 zitakazofanyika mwakani nchini Senegal itachezwa wikiendi hii jijini Dar es Salaam.

Waamuzi hao wataongozwa na Jean-Jacques Ndala Ngambo atakayesaidiwa na Oliver Safari Kabene, Nabina Blaise Sebutu na Mupemba Ignace Nkongolo. Kamishna wa mechi hiyo namba 37 ni Poiret Antoine Ralph Danny kutoka Shelisheli.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)



Nemanja Vidic akipata picha ya pamoja na  Sir Bobby Charlton kwenye uwanja wa  Old Trafford leo wakati Man United walipoikaribisha timu ya Hull City

Kwaheri kijana!!! Nemanja anatimkia kucheza soka lake la mwisho huko Inter Milan
 Vidic na baadhi ya wachezaji wa United
Vidic alianzia benchi kwenye mtanange wao na  Hull City ambapo Vidic alichukua nafasi ya  Phil Jones baada ya kuumia bega akiwa kwenye patashika za hapa na pale wakati wa kona.

Pia, Meneja-Mchezaji, Ryan Giggs, ambae aliingia kucheza Kipindi cha Pili na ambae ndie alitoa Pasi yenye akili iliyompa mwanya Robin van Persie, huenda nae pia ikawa hii ndio Mechi yake ya mwisho Old Trafford kama Mchezaji kwa vile Mkataba wake nae kama Mchezaji unamalizika mwishoni mwa Msimu.

Man United wamebakiza Mechi moja ya Ligi hapo Jumapili ambako watacheza Ugenini kwa Mtakatifu Maria dhidi ya Southampton na ushindi kwao na kipigo kwa Tottenham kitawapa Nafasi ya 6 na hivyo kucheza EUROPA LIGI Msimu ujao.

Mtaalamu wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ian McClements amewasili Bukoba leo hii Asubuhi kwa Ndege ya kukodi. 
McClements akiwa hapa Bukoba amekagua Uwanja wa Kaitaba, na baadae amekwea tena ndege yake kuelekea  jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.




Viwanja hivi vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClements atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.

Dr. Ian McClements (kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba
Dr. Ian McClementsNje kidogo ya mipaka ya Uwanja Dr. Ian McClements analazimika kuchimba ili aweze kuona chini kuna nini? akitaka kupima maji yanafyonzwa vipi na ni udongo gani? na Je Maji yananyonywa vipi na udongo wa hapa Kaitaba ususani kwenye uwanja huu huu wanaotaka kuuwekea nyasi za Bandia.
Dr. Ian McClementsKumbe kuna mchanga chini, yes! safi
Dr. Ian McClements (kulia) akichukua kumbukumbu kushoto ni Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba.
Dr. Ian McClement akipima kina
Dr. Ian McClement alimwaga maji ndani ya shimo ili kuona kaji nini kitafata na je yatanyonywa na udongo kwa muda gani!

Ili chukua muda wa dakika 1 na sekunde 40 tu maji yalikuwa yameishatowekaAkipima maji aliyoweka
Dr. Ian McClements akichukua maelezo kutoka kwa Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba
Alichima na sehemu ya upande wa pili wa goli



Dr. Ian McClements akiteta jambo na Kiongozi Katibu wa KRFA Jumanne Chama

Hapa mchanga hakuna na Udongo wake ni Mweusi mchanga upo chini zaidi

 


Dr. Ian McClements baada ya kumaliza kazi yake alipaa kuelekea jijini Mwanza na hapa alikuwa anaagana na Jumanne Chama kwenye Uwanja wa Ndege
Mwewe yupo tayari!

waliotembelea blog