Mshindi wa Shindano la Bongo Star Search 2015 (BSS), Kayumba Juma
(katika), akiwa ameshikilia fedha zake muda mfupi baada ya kuibuka
kidedea kwenye fainali hizo zilizokuwa zikifanyika usiku wa kuamkia leo
katika Ukumbi wa King Solomoni uliopo Namanga jijini Dar es Salaa.
Jaji Mkuu wa mashindano hayo, Madam Rita (wa pili kutoka kushoto), akimtangaza mshindi huyo.
Washiriki waliongia kwenye 6 bora ya mashindano hayo wakiwa jukwaani kabla ya mchujo huo kuanza
Mmoja wa Majaji wa shindano hilo (kulia), Master Jay akiingia ukumbini
hapo huku akiwa ameongozana na mpenzi wake ambaye ni msanii wa Bongo
fleva Shaa.
Majaji wakiwa kwenye meza yao ya kuratibia mashindano hayo.
Peter Msechu akiwa katika pozi kwenye Red Carpet.
Wasnii wanaounga kundi la Navy Kenzo wakipagawisha jukwaani hapo.
Msanii kutoka nchini Nigeria, Run Town anayetamba na kibao chake cha Gallardo, akipagawisha jukwaani hapo.
Mmoja wa washiriki waliokuwa wakichuana jukwaani hapo, Angel Marykato akisaka milioni 50.
Vijana wanaounda kundi la Yamoto Bendi wakitoa burudani kwenye fainali hizo.
Msanii wa Dansi Christiani Bella akitunza na mashabiki wake wakati akitumbuiza kwenye fainali hizo.
Bosi anayesimamia lebo ya Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akishuhudia kwa makini fainali hizo.
Mshiriki wa Shindano hilo kutoka Arusha, Frida Amani akipagawisha jukwaani hapo kuwania kitita cha shilingi milioni 50.
Kala Jeremiah akikumbushia enzi zake katika mashindano hayo.
Msanii wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ akiwa katika pozi kwenye red Carpet ya mashindano hayo.
Ben Poul akiwa katika pozi na mmoja wa mashabiki zake.
Baadhi ya washiriki waliyotolewa mapema kwenye kinyang’anyiro hicho wakihojiwa muda mfupi baada ya kuwasili ukumbini hapo.
Msanii wa Filamu, Muna Alphonce akiwa katika ubora wake kwenye tamasha hilo.
Kayumba akitunzwa na mashabiki wake kabla ya kutangazwa kuwa mshindi.
Madam Rita akifuta machozi muda mfupi baada ya kumkabidhi mshindi kitita cha shilingi milioni 50.
Madam Rita akiwa kwenye pozi.
Mmoja ya kikundi cha kudansi kikitumbuiza jukwaani hapo.
Mpiga picha Musa Mateja (kushoto), akihojiwa mara baada ya kuingia ukumbini hapo.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria ukumbini hapo wakifuatilia burudani hizo kwa makini.
Kayumba
Juma wa jijini Dar es Salaam juzi usiku aliibuka mshindi wa shindano la
kusaka vipaji vya muziki la Bongo Star Search (BSS) kwa mwaka 2015
baada ya kuwabwaga washiriki wengine watano waliofika hatua ya fainali,
hivyo kutwaa kitita cha Sh50 milioni. Mbali na kuondoka na fedha hizo,
kijana huyo amepewa bima ya afya ya mwaka mzima kutoka kwa kampuni ya
Jubilee Insurance.
Juma aliibuka kidedea katika fainali hizo
zilizofanyika katika Ukumbi wa King Solomon Hall, Kinondoni jijini Dar
es Salaam zilizopambwa na wasanii mbalimbali wa muziki.
Mshindi huyo aliwabwaga washiriki wengine watano ambao walifika hatua ya
fainali; Frida Amani, Nassib Fonabo, Jacqueline Kayengi, Angel Mary
Kato na Kevin Gerson. Licha ya kushindwa kutwaa taji hilo washiriki hao
watano walitoa ushindani mkubwa na kuwapa burudani mashabiki
waliohudhuria kwenye ukumbi huo.
Sambamba na burudani kutoka kwa
washiriki hao, pia wapo baadhi ya wasanii waliolipamba jukwaa la fainali
hizo ikiwa ni pamoja na Kala Jeremiah, Peter Msechu, Christian bella,
Yamato Band pamoja na msanii kutoka Nigeria, Runtown.
Jaji
kiongozi wa mashindano hayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya
Benchmark, Rita Poulsen alimtangaza mshindi huyo baada ya washiriki wote
sita kuchuana jukwaani na kubaki wawili.
Baada ya wawili hao,
Kayumba Juma akiwakilisha Dar es salam na Nassib Fonabo kutoka Arusha
ambao waliingia katika hatua ya mbili bora na kutupa karata yao ya
mwisho kwa kuimba muziki wa mwisho, mashabiki walipiga kura na muda
mfupi baadae Jaji huyo maarufu kwa jina la Madam Rita alipanda jukwaani
na kumtangaza mshindi.
“Mnamjua mshindi…? Sina maneno mengi maana
kazi yangu ni kumtangaza mshindi wa mashindano ya BSS msimu wa 8 (season
eight), mshindi ni.. ni.. Kayumba Juma’’ alitangaza Madam Ritah huku
mashabiki wakishangilia kutokana na burudani aliyotoa mshindi huyo.
Mashindano hayo yanayoandaliwa na Kampuni ya Benchmark Production 360
yalianza mwaka 2006 kwa kusaka vipaji vya vijana wa Kitanzania kila
mwaka lakini mwaka jana mashindano hayo hayakufanyika tofauti na
ilivyozoeleka.
Baadhi ya washindi wa BSS kwa miaka tofauti toka
shindano lianzishwe ni pamoja na; Jumanne Iddi, Kala Jeremiah, Peter
Msechu, Walter Chilambo na Emmanuel Msuya.