KOCHA wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesisitiza kuwa Real Madrid Leo wana ari kubwa kucheza na Wapinzani wao wa Jadi Atletico Madrid kwenye Dabi ya Jiji la Madrid Uwanjani Vicente Calderon na Staa wao Cristiano Ronaldo, ambae alizikosa Mechi 2 baada ya kuwa Kifungoni, ana moto mkubwa kucheza Mechi hii.
Hivi sasa Real Madrid wanaongoza La Liga wakiwa Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili Barcelona na Pointi 7 mbele ya Timu ya 3 Atletico Madrid ambao ndio Mabingwa Watetezi wa La Liga.
Lakini Real wanatinga Mechi hii wakiwa na pengo kubwa kwa kuwakosa Pepe, James Rodriguez na Sergio Ramos, ambao ni Majeruhi, na pia Marcelo ambae amefungiwa Mechi 1 baada ya kuzoa Kadi za Njano 5.
Licha ya Real kushindwa kuifunga Atletico katika Mechi zao 5 zilizopita, wakitoka Sare 2 na Kufungwa 3, Ancelotti amesisitiza wao watacheza kwa kushambulia.
Ameeleza: “Hatuwaogopi Atletico. Hatufikirii Sare. Tunajitayarisha kushinda Gemu!”
Aliongeza: “Hatufikirii kuhusu Wachezaji tutakaowakosa! Tunao Fabio Coentrao na Alvaro Arbeloa wanaoweza kucheza Fulbeki ya Kushoto [badala ya Marcelo]. Tunawaamini Raphael Varane na Nacho Fernandez kucheza Sentahafu!”