Kulia ni kocha mkuu wa West Ham akipongezana na kocha wa Man U Van Gaaal baada ya mechi yao ya Jumamosi iliyopita, Sep 28, 2014 |
Allardyce alisema enzi za kibabu Fergie mambo yalikuwa burudani Old
Trafford kwani kibabu alikuwa akitenga muda mfupi wa kuteta na kocha wa
timu pinzani baada ya mechi huku wa wakipata kinywaji.
"Baada ya mechi kama nilivyozoea nilielekea katika chumba ambacho
Ferguson zamani alikuwa akipenda kukutana na makocha wa timu pinzani
kupata kinywaji baada ya mechi kwa siku husika huku wakibadilishana
mawazo, lakini nilishangaa sana kuambiwa ule utaratibu haupo tena,
kiukweli nilitoka na aibu kubwa ukizingatia nimefungwa magoli 2-1 siku
hiyo!" Allardyce alisema.
Baada ya kupoteza mchezo huo dhidi ya Man U wikiendi iliyopita, West Ham
sasa wako katika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi kuu Uingereza huku
Mashetani Wekundu wakiendelea kuienzi mtaa wa saba (nafasai ya saba)
ambayo ndiyo ilikuwa nafasi yao mpaka ligi ya msimu wa 2013/2014
inamalizika