Wednesday, May 27, 2015


Kocha wa Bournemouth ya England Eddie Howe
Kocha wa timu ya soka Bournemouth ya England Eddie Howe ametajwa kuwa meneja bora wa mwaka wa shirikisho la mameneja wa soka nchini Uingereza LMA.
Kutajwa kwa meneja huyo kunakuja kufuatia kuiongoza kwa mafanikio klabu yake ambayo imeingia ligi kuu ya England kwa mara ya kwanza tokea ianzishwe zaidi ya miaka 100 iliyopita. Howe anakuwa kocha wa pili kutoka nje ya ligi kuu kushinda tuzo hiyo tangia mwaka 1992. "siamini kabisa, ni jambao nisilotarajia" alisema kocha huyo.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika -CAF leo hii limeipa Tanzania uenyeji wa fainali za michuano ya Afrika ya vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.
Uenyeji huu ni hatua muhimu sana kwa Tanzania katika kukuza soka la vijana na kwa hatua hii Tanzania itacheza moja kwa moja fainali hizi.
Katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki fainali hizi Tanzania, mwezi Juni mwaka huu TFF itaandaa mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 na wachezaji bora wa mashindano haya wataunda kikosi cha mwanzo cha Taifa kuelekea fainali za mwaka 2019.

TFF inamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete na Mh. Fennela Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kufanikisha maamuzi haya, na inaamini ushirikiano huu wa Serikali na wadau wengine utafanikisha mashindano haya mwaka 2019.


Klabu ya Spain, Sevilla, Jumatano wanawania kuweka Historia ya kuwa Klabu ya kwanza kutwaa Kombe la EUROPA LIGI kwa mara ya 4 watakapokuwa ndani ya National Stadium Mjini Warsaw, Poland, kucheza Fainali na Klabu ya Ukraine, FC Dnipro Dnipropetrovsk.
Sevilla wametwaa Kombe hili mara 3 katika Miaka ya 2006, 2007 na 2014.
Mbali ya kuwania kuwa Klabu ya kwanza kulibeba Kombe mara 4, Sevilla pia wanawania kulitwaa ili kuweza kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao kwani, kwa mara ya kwanza, Bingwa wa EUROPA LIGI anaingizwa UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao.
Hii ni nafasi pekee kwa Sevilla ambao hivi Juzi walimaliza La Liga wakiwa Nafasi ya 5 na hivyo kukosa kuingizwa UEFA CHAMPIONS LIGI.


Hii ni mara ya kwanza kwa Dnipro kucheza Fainali ya Klabu Barani Ulaya.
Sevilla, chini ya Kocha Unai Emery, wamefika Fainali hii kwa kuzitoa Borussia Monchengladbach, Villarreal, Zenit St Petersburg na Nusu Fainali Fiorentina ambayo waliinyuka Jumla ya Mabao 5-0 na hiyo yote ni kutokana na kazi njema ya Wachezaji wao kina Carlos Bacca, Aleix Vidal, Kevin Gameiro na Jose Antonio Reyes.
Dnipro, chini ya Kocha Myron Markevych na kwa mshangao wa wengi, wametinga Fainali kwa kuzibwaga Olympiakos, Ajax, Club Brugge na kisha Napoli kwenye Nusu Fainali baada ya kutoka 1-1 katika Mechi ya Kwanza huko Italy na kushinda 1-0 katika Marudiano kwa Bao la Yevhen Seleznyov.


Dutchman Mart Nooij, kocha wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
Kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, imeamua kuwa kocha Mkuu wa timu ya taifa Mart Nooij apewe changamoto ya kufaulu kucheza fainali za michuano ya CHAN mwakani, akishindwa aondoke.
Nooij raia wa Uholanzi ambaye kikosi chake hakikufanya vizuri katika michuano ya kusaka taji la COSAFA baina ya mataifa ya Kusini mwa Afrika na kuondoka bila ya kupata ushindi wowote.

Michuano ya CHAN huwahusisha wachezaji wanaocheza soka katika vlabu vya nyumbani barani Afrika, na michuano ya mwaka 2016 itachezwa nchini Rwanda kuanzia mwezi Januari.
Tanzania kwa mara ya tatu imejumuishwa katika kundi moja na Uganda kufuzu katika michuano hiyo na mchuano wa kwanza itapigwa katikati ya mwezi ujao huku ule wa marudiano ukiwa mwezi Julai.
Mwaka 2009 wakati michuano hii ilipofanyika nchini Sudan, Tanzania ilifuzu katika michuano hiyo baada ya kuifunga Uganda mabao 3 kwa 2 lakini mwaka 2014, Uganda waliibuka washindi baada ya kuwachabanga Tanzania kwa jumla ya mabao 3 kwa 1 na kufuzu katika fainali hizo nchini Afrika Kusini.


Wachezaji wawili wa klabu ya soka ya TP Mazembe nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiongozwa na mlinda mlango Robert Muteba Kidiaba, wamewasilisha maombi ya kuwania ubunge katika jimbo la Katanga.
Pamoja na Kidiaba ambaye anafahamika sana kwa mtindo wa kusherehekea bao kwa kuruka kwa makalio, Pamphile Mihayo Kazembe pia ni mchezaji mwingine wa TP Mazembe anayewania ubunge kupitia chama cha upinzani cha PND.
Nahodha huyo wa Leopards mwenye umri wa miaka 39 amesema anaamini kuwa wachezaji wanaweza kuwa viongozi bora na kuleta mabadiliko ya maendeleo katika maeneo yao.

Uchaguzi wa wabunge na urais utafanyika mwaka ujao nchini humo na ikiwa Kidiaba atachaguliwa kuwa mbunge, bila shaka itakuwa ni historia katika mchezo wa soka nchini humo.
Kidiaba alianza kuichezea timu ya taifa mwaka 2002 na ameshiriki katika michuano 11 ya kufuzu katika michuano ya kombe la duniani na kwa ujumla kuichezea timu ya taifa mara 59.
Mwezi Desemba, mwaka 2014 alitangaza kuwa alikuwa anajiuzulu baada ya michuano ya mwaka huu ya mataifa bingwa barani Afrika lakini baadaye akabadilisha mawazo ya kuendelea kucheza soka.


Kocha wa Spain Vicente del Bosque amewaita Vijana wapya wawili wa Sevilla, Sergio Rico na Aleix Vidal, kwa ajili ya Mechi zao za Juni dhidi ya Costa Rica na Belarus na kumwacha Straika wa Chelsea Diego Costa.Kipa Rico, Miaka 21, na Winga Vidal, Miaka 25, wamekuwa waking'ara Msimu huu na Sevilla ambayo imemaliza La Liga ikiwa Nafasi ya 5 na Jumatano Mei 27 huko Stadion Narodowy Mjini Warsaw, Poland, watacheza na Klabu ya Ukraine Dnipro Dnipropetrovsk kwenye Fainali ya Europa Ligi.
Wachezaji hao wawili wanaungana na mwenzao wa Sevilla, Vitolo, kwenye Kikosi cha Wachezaji 24 wa Spain.

Spain watacheza Mechi ya Kirafiki na Costa Rica huko Jijini Leon, Spain hapo Juni 11 na Juni 14 kucheza Ugenini huko Borisov na Belarus kwenye Mechi ya Kundi lao la EURO 2016.
 
Kocha wa Spain Vicente del Bosque amewaita Vijana wapya wawili wa Sevilla, Sergio Rico na Aleix Vidal, kwa ajili ya Mechi zao za Juni dhidi ya Costa Rica na Belarus na kumwacha Straika wa Chelsea Diego Costa.

KIKOSI KAMILI CHA SPAIN:

Goalkeepers: Iker Casillas (Real Madrid), David De Gea (Manchester United), Sergio Rico (Sevilla).

Defenders: Juanfran (Atletico Madrid), Dani Carvajal (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Marc Bartra (Barcelona), Jordi Alba (Barcelona), Juan Bernat (Bayern Munich), Mikel San Jose (Athletic Bilbao)

Midfielders: Koke (Atletico), Sergio Busquets (Barcelona), David Silva (Manchester City), Isco (Real Madrid), Santi Cazorla (Arsenal), Cesc Fabregas (Chelsea), Andres Iniesta (Barcelona), Pedro Rodriguez (Barcelona), Vitolo (Sevilla), Aleix Vidal (Sevilla)

Forwards: Paco Alcacer (Valencia), Alvaro Morata (Juventus), Nolito (Celta).

waliotembelea blog