Wachezaji
wawili wa klabu ya soka ya TP Mazembe nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo wakiongozwa na mlinda mlango Robert Muteba Kidiaba, wamewasilisha
maombi ya kuwania ubunge katika jimbo la Katanga.
Pamoja na Kidiaba ambaye anafahamika sana kwa mtindo wa kusherehekea bao kwa kuruka kwa makalio, Pamphile Mihayo Kazembe pia ni mchezaji mwingine wa TP Mazembe anayewania ubunge kupitia chama cha upinzani cha PND.
Nahodha huyo wa Leopards mwenye umri wa miaka 39 amesema anaamini kuwa wachezaji wanaweza kuwa viongozi bora na kuleta mabadiliko ya maendeleo katika maeneo yao.
Uchaguzi wa wabunge na urais utafanyika mwaka ujao nchini humo na ikiwa Kidiaba atachaguliwa kuwa mbunge, bila shaka itakuwa ni historia katika mchezo wa soka nchini humo.
Kidiaba alianza kuichezea timu ya taifa mwaka 2002 na ameshiriki katika michuano 11 ya kufuzu katika michuano ya kombe la duniani na kwa ujumla kuichezea timu ya taifa mara 59. Mwezi Desemba, mwaka 2014 alitangaza kuwa alikuwa anajiuzulu baada ya michuano ya mwaka huu ya mataifa bingwa barani Afrika lakini baadaye akabadilisha mawazo ya kuendelea kucheza soka.

0 maoni:
Post a Comment