Sunday, September 22, 2013

 Pamoja na kuzipata hizi picha kuna maswali
 unaweza kuwa nayo ikiwemo Idadi ya ndege
 zitakazoweza kuhudumiwa kwenye uwanja 
huu mpya? utamalizika lini? gharama yake na mengine…



 
  
Baadhi ya majeruhi katika shambulio la kigaidi jijini Nairobi.
-Wadai Kenya ilipuuza onyo lao
-Wasema ni kulipiza kisasi kwa Kenya kijihusisha katika vita ya Somalia

-Watu zaidi ya 30 wadaiwa kupoteza maisha wengine wakijeruhiwa

KUNDI la Alshabaab, limethibitisha kuhusika na shambulio la kigaidi lililotokea jana kwenye jengo la ghorofa nne lenye maduka la Westgate jijini Nairobi, nchini Kenya.
Alshabaab kupitia kwa afisa wake mmoja, imethibisha hilo na kueleza kuwa shabulio lilikuwa na kulipiza kisasi baada ya Kenya kujihusisha na vita ya Somalia.

 
Hali ilivyokuwa ndani ya jengo lililovamiwa na magaidi.
Walioshuhudia tukio hilo wanadai watu waliovalia magwanda yalioonekana kama ya kijeshi huku wengine wakiwa wamefunika nyuso zao walivamia jengo hilo huku wakifyatua risasi.
Maduka hayo ya Westgate hutendelewa sana na matajiri pamoja na wageni kutoka nchi mbalimbali.
Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab imesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waislamu wasio na hatia nchini Somalia, na shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakumba wasomali nchini Somalia.
Taarifa kutoka Ikulu ya nchini Kenya, zinadai kuwa mmoja wa watuhumiwa aliyekamatwa katika tukio hilo  alifariki kutokana na majeraha yake.
Magaidi wapatao kumi walivamia jengo la kifahari la Westgate jana mchana la kuwapiga risasi kiholela Wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida.




              WATU waliokuwa na silaha wamefyatua risasi mjini 
Nairobi, Kenya, kwenye eneo la maduka katika mtaa wa Westlands.
Walioshuhudia tukio hilo, wanasema kuwa maguruneti piya yalitumika.
Inaarifiwa watu watano wamekufa.(P.T)

Mwandishi wetu mjini Nairobi anaeleza kuwa washambuliaji
 inaarifiwa walivaa vilemba kama vya al-Shabaab, lakini
 haikuthibitishwa kama wapiganaji hao wamehusika.
Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira jengo la maduka
 liitwalo Westgate, katika mtaa wa Westlands, na kuna taarifa
 ya watu waliojeruhiwa wakitolewa hapo kwa machera.















 
Mtangazaji wa habari katika kituo cha redio cha 
Kiss FM kwa jina la ''Ruhila Aditya''
 ni miongoni mwa waliopoteza maisha yao katika shambulizi hilo.
Warembo waliobahatika kuingia kumi bora

 
Tano bora ya Redd's Miss Tanzania 2013




Hii ndio tano bora ya Redd's Miss Tanzania 2013
. Je nani hapa ataondoka na taji, gari na
 kitita cha Milio ni 8? Warembo hao
 kutoka kushoto ni Happiness Watimanywa (Miss Photogenic),
 Elizabeth Pretty, Clara Bayo (Miss Sports Women), Lucy Tomeka na Latifa Mohamed.
 
Fainali za Miss Tanzania 2013 ndio zinaendelea usiku huu ndani ya Mlimani City jijini Dar es Salaam. Gari ndo hilo hapo Je nani ataingia ndani na kuliendesha? Tusubiri Majaji. Hadi sasa Top 5 ndo ishatajwa.




Onyesho la Redd's Miss Tanzania 2013 
Live kutoka Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam usiku huu

Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 
wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa Onyesho
 la Taifa la Urembo linalofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.



Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013
 wakifungua shindano la mwaka huu kwa
 kuonyesha ufundi wao wa kucheza muziki. Shindano
 la mwaka huu ambalo
 limedhaminiwa na kampuni ya vinywaji Tanzania.Tanzania
 Breweries Limited kupitia kinywaji 
cha Redds limefanyikia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam. Jumla ya warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali,vyuo nk wameshiriki.







Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013




 
Mshindi wa Redd's Miss Tanzania 2013
 Happiness Watimanywa katikati akipungia
 mkono mara baada ya kutangazwa mshindi 
usiku huu kushoto ni pili Latifah Mohamed na kulia ni mshindi wa tatu Clara Bayo.
 
 wakipita jukwaani na mavazi ya aina mbali mbali 
wakati wa Onyesho la Taifa Redd's Miss Tanzania 2013
 linalofanyika usiku huu kwenye
 Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam usiku huu.

Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa Kizazi kipya
 hapa nchini,Lady Jay Dee akitoa burudani kwenye
 Onyesho la Redd's Miss Tanzania 2013,linalofanyika
 hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam

waliotembelea blog