Kipindi cha pili dakika ya 45 walifanya mabadili kwa makini kwa
Sammy Ameobi kumbadili Yoan Gouffran na Gabriel Obertan kumbadili Mehdi Abeid na kupata bao dakika ya mapema bao la kusawazisha katika dakika ya 46 kwa kufanya 1-1 bao lililofungwa na Jack Colback.
Dakika ya 53 Spurs walipiga mpira wa adhabu frii kiki na kuzama moja kwa moja ndani ya lango la Newcastle United na kujipatia bao la kuongoza la pili, Frii kiki iliyopigwa na Christian Eriksen na kufanya 2-1.
Bao la mwisho la tatu kwa Spurs lilifungwa na Staa wao wa mabao Harry Kane katika dakika ya majeruhi na mtanange kumalizika kwa 3-1 dhidi ya Newcastle United. Harry Kane akifikisha jumla ya mabao 20 msimu huu.Ushindi huu wa Tottenham umewapandisha hadi Nafasi ya 6 wakifungana Pointi na Liverpool walio Nafasi ya 5 wote wakiwa Pointi 7 nyuma ya Timu ya 4 Man City.Maelfu ya Mashabiki wao wakigomea kuhudhuria Mechi ya Timu yao Newcastle ilipocheza Uwanjani kwao Saint James Park dhidi ya Tottenham wakionyesha mshikamano wa kumpinga Mmiliki wa Klabu yao, Mike Ashley, Tottenham haikuwa na huruma ilipowashindilia Bao 3-1 katika Mechi ya Ligi Kuu