Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara na Nahodha wa Ivory Coast Yaya Toure jana Jumatatu
Maelfu ya mashabiki wa soka nchini Ivory
Coast wamefika kuwapokea mabingwa wa mataifa ya Afika Ivory Coast baada
ya kuifunga Ghana kwa njia ya penati na kunyakua kombe hilo.
Maelfu ya mashabiki walitanda mitaani ili kuwalaki wachezaji na viongozi
kwa ushindi huo,Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara amewapongeza
wachezaji na kusema ushindi wa Ivory Coast utaleta umoja na amani kwa
nchi.
Polisi ilibidi kuamuru watu kubaki majumbani kwao sababu ya
usalama baada ya uwanja uliokuwa umeandaliwa kwa ajili ya kuwalaki
wachezaji na viongozi baada ya ushindi wa kihistoria wa kushinda kombe
la mataifa ya Afrika huko Guinea ya Ikweta.
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara akiwa na Nahodha Yaya Toure wakati wakilitembeza Kombe kwa Mashabiki
Wachezaji wa Ivory Coast wakishangilia ushindi huku wakilindwa na Wanajeshi
Yaya Toure akionesha Kombe Juu wakati wanashuka kwenye Ndege Mjini Abidjan
Karibu karibu..Ongera!!
Ushindi huo ulifanya Nchi ya Ivory Coast jana siku ya Jumatatu kuwa ni
siku ya Mapumziko Nhini humo na kuweza kuhudhuria kwa Wingi mapokezi
hayo na kuweza kuliona Kombe hilo waliloshinda Nchini Guinea wlipoifunga
kwa Mikwaju ya Penati 9-8 Ghana.
Wakitembeza Kombe kwa Mashabiki
Mchezaji wa Ivory Coast Nahodha na ambaye pia anacheza Ligi Kuu England
kwenye Klabu ya Manchester City Yaya Toure aliiongoza Timu hiyo na
kupigana Mpaka mwisho na Kuibuka Na Ubingwa wa AFCON 2015 dhidi ya
Ghana.
Yaya Toure na wenzake wakishangilia baada ya kuibuka Kidedea dhidi ya Ghana.