Monday, June 29, 2015


WENYEJI Chile wametinga fainali ya Copa America 2015 kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Peru usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Taifa mjini Santiago:
Kwa ushindi huo, fainali Chile sasa itakutana na mshindi kati ya Argentina na Paraguay zinazomenyana usiku wa kuamkia kesho.
Eduardo Vargas aliifungia bao la kwanza akimalizia krosi ya Alexis Sanchez dakika ya 42.
Carlos Zambrano alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Charles Aranguiz.
Bao la kujifunga la Gary Medel dakika ya 60 liliwapa matumaini wageni, kabla ya Vargas kuifungia la ushidi Chile dakika ya 64.
Kikosi cha Chile kilikuwa; Bravo, Isla, Medel, Rojas, Albornoz/Mena dk46, Vidal, Diaz/D Pizarro dk46, Aranguiz, Valdivia/Gutierrez dk86, E Vargas na Sanchez. 
Peru; Gallese, Advincula, Zambrano, Ascues, Vargas, Carrillo/C Pizarro dk73, Ballon, Lobaton/Yotun dk73, Cueva/Ramos dk27, Farfan na Guerrero.

The former QPR loanee struck a superb winner into the top corner from well outside the box at the National Stadium
The former QPR loanee struck a superb winner into the top corner from well outside the box at the National Stadium
Peru goalkeeper Pedro Gallese could do nothing about Vargas' strike but the 10-man visitors put up a fight in Santiago
Carlos Zambrano caught Chile midfielder Charles Aranguiz on the back with his studs in the first half in Santiago
Carlos Zambrano caught Chile midfielder Charles Aranguiz on the back with his studs in the first half in Santiago
The Peruvian defender was booked earlier on in the contest but was still shown a straight red card by referee Jose Argote
The Peruvian defender was booked earlier on in the contest but was still shown a straight red card by referee Jose Argote
The Chile players celebrate at the end of the game - they will play either Colombia or Argentina in the Copa America final 
Vargas wheels away in celebration after opening the scoring for hosts Chile in the Copa America semi-final
Vargas wheels away in celebration after opening the scoring for hosts Chile in the Copa America semi-final
Vargas rolled the ball over the line after Alexis Sanchez' cross hit the post with the goalkeeper beaten
Vargas rolled the ball over the line after Alexis Sanchez' cross hit the post with the goalkeeper beaten
Arturo Vidal and Charles Aranguiz rush to congratulate Vargas after his strike put Chile in front in the first half

Gary Medel (right) stretches to cut out a cross but only manages to turn the ball past Claudio Bravo and into his own net

The Peru players celebrate after Medel's own goal gave them a route back into the Copa America semi-final

Aranguiz had to receive medical attention after he was caught by Zambrano during the first half of the Copa America semi-final in Santiago
 


c1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea akizungumza na wanamichezo (hawapo pichani) kabla ya kuanza fainali ya Kombe la Chikawe katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya Marambo na Timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa zilipambana na Timu ya Black Fire iliibuka mshindi kwa magoli 3 kwa 1. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
c2
Kapteni wa Timu ya Black Fire, Ally Njaidi (kulia) akipokea fedha taslimu Shilingi 500,000 pamoja na Kikombe cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema, baada ya kumalizika fainali ya Kombe la Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Timu hiyo iliirarua timu ya Motisha mabao 3 kwa 1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salimu Mwalimu, naye alihudhuria fainali ya mashindano hayo ambayo yalianzishwa na Mbunge Chikawe jimboni humo kwa kushirikisha timu 178 katika jimbo hilo.
c3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea akimsalimia mchezaji wa Timu ya Black Fire, Faraji Mohamed wakati alipokuwa anaikagua timu hiyo kabla ya fainali ya Kombe la Chikawe ambayo yalifanyika katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya Marambo iliibuka kidedea baada ya kuinyuka Timu ya Motisha, Kata ya Kilimani magoli 3 kwa 1. Nyuma ya Waziri Chikawe ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
c4
Kapteni wa Timu ya Motisha,  Saidi Chakupewa (kulia) akipokea zawadi ya ushindi wa pili, kikombe na fedha taslimu Shilingi 200,000 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema, baada ya kumalizika fainali ya Kombe la Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Timu hiyo ilifungwa na Timu ya Black Fire mabao 3 kwa 1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salimu Mwalimu, naye alihudhuria fainali ya mashindano hayo ambayo yalianzishwa na Mbunge Chikawe jimboni humo kwa kushirikisha timu 178 katika jimbo hilo.
c5
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe  (aliyevaa kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Black Fire ambao ndio waliibuka washindi. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
c6
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe  (aliyevaa kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
c7
Msanii maarufu wa bongofleva, Seleman Jabir ‘Msaga Sumu’ akitumbuiza katika fainali ya Kombe la Chikawe lililofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Katika fainali hiyo, Timu ya Black Fire iliibuka kidedea baada ya kuifunga timu ya Motisha magoli 3 kwa 1.
c8
Mchezaji wa timu ya Black Fire (kulia) akisakata kabumbu katika fainali ya kombe la Mbunge Chikawe lililofanyika katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu hiyo ya Black Fire iliinyuka timu ya Motisha magoli 3 kwa 1. Picha zote na Felix Mwagara.


xxx 
Baadhi ya Wanamichezo wa Polisi walioshiriki Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika mwaka 2013 nchini Namibia wakiwa katika picha.

Timu za Jeshi la Polisi Tanzania zitakazoshiriki michezo ya Umoja wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO),  mwishoni mwa mwezi julai nchini Swaziland zinaendelea kujifua vyema katika  kambi yao inayoendelea katika chuo cha Taaluma ya  Polisi Dar es Salaam (DPA).
Akizungumza na blog  hii Mkuu wa kitengo cha  michezo cha Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Jonas Mahanga alizitaja timu zilizopo kambini kuwa ni  pamoja na Timu ya Mpira wa miguu, pete, riadha na vishale ambapo hivi sasa zinajifua kuhakikisha kuwa zinakuwa vizuri pindi michuano hiyo itakapoanza kutimua vumbi.
Amesema timu hizo zitaanza kucheza michezo ya kirafiki ili kujipima nguvu na kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kuwa michezo ya mwaka huu itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na nchi zilizothibitisha kushiriki kujipanga vizuri.
SSP Mahanga amesema mpaka sasa nchi kumi na nne zimeshathibitisha kushiriki michuano hiyo na wanaendelea kuwakaribisha wadhamini mbalimbali watakaoweza kusaidia safari hiyo ili kuliletea taifa sifa.
Aidha amesema wachezaji wengi wa riaha wanaendelea na mazoezi katika timu ya taifa ya riadha na wengine wapo nchini Kenya ambapo muda utakapowadia wataungana na wenzao katika kambi hiyo ya Dar es Salaam.
Kwa upande wake kocha  wa timu ya mpira wa miguu Corporal John Tamba amesema wachezaji wake wamekuwa wakionyesha kiwango kizuri katika mazoezi kwa kuwa wengi wao wametoka katika mashindano hivi karibuni.
Amesema wachezaji wengi waliopo kambini wanatoka katika timu za Polisi Morogoro, Dodoma, Dar es Salaam, Tabora na Mara ambapo alisema kupitia michezo ya kirafiki atahakikisha timu yake inakuja na ushindi.

waliotembelea blog