Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema
ana imani na kikosi chake kuendelea kufanya vizuri ingawa kuna mambo kadhaa
hajaridhika sana.
“Katika soka kila unapocheza, linaibuka jambo
jipya. Mkirekebisha na kucheza mechi nyingine, linaibuka jambo ambalo
linahitaji marekebisho tena.
“Huo ndiyo mpira, tulitengeneza nafasi nyingi
dhidi ya Coastal. Tunachotakiwa ni kuzitumia zaidi,” alisema.
“Lakini kuna makosa kadhaa tulifanya, bado
tutayafanyia kazi zaidi.”
Yanga imeanza kutetea kombe lake kwa kuichapa Coastal
Union kwa mabao 2-0.
Mechi inayofuata Yanga itacheza na Prisons amnayo
ilianza ligi hiyo kwa kipigo cha mabao 2-1 ktoka kwa Azam FC.