Tuesday, September 15, 2015


Wakati Staa wa Barcelona Lionel Messi akijitayarisha kucheza Mechi yake ya 100 kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, Kocha wake, Luis Enrique, Jumatano anapambana na Klabu yake ya zamani AS Roma katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi E.
Luis Enrique, Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Spain, aliwahi kuwa Kocha wa AS Roma katika Msimu wa 2011/12 na kuondoka Klabuni hapo baada ya kushindwa kuiingiza Mashindano ya Klabu Ulaya.
Lakini Enrique, ambae Timu yake Barca Jumatano ipo Stadio Olimpico kucheza na AS Roma, amesema kuwa uzoefu aliopata huko Italy na Klabu ya AS Roma ndio unampa mafanikio.
Msimu uliopita, Enrique aliiongoza Barca kutwaa Trebo ikiwa ni Ubingwa wa La Liga, Copa del Reay na UCL.
Gemu hii ya Barca na AS Roma pia itamfanya Lionel Messi apige hatua nyingine katika maisha yake ya Soka kwa kufikisha Mechi 100 za UCL.
Messi ndie anaeshika Rekodi ya Ufungaji Bao nyingi kwenye Mashindano hayo.
Mwezi Agosti, Barca, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Ulaya, waliichapa AS Roma 3-0 katika Mechi ya Kirafiki ya Joan Gamper.
Mara ya mwisho kwa Barca kuivaa AS Roma kwenye UCL ni Februari 2002 Mechi ambayo walitoka 1-1 na Luis Enrique aliichezea Barca kama Kiungo.
Wakati Messi akitaka kupiga hatua, nae Gwiji wa AS Roma,Francesco Totti, anawania kuifungia Timu yake Bao lake la 300.

RATIBA
kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumatano 16 Septemba 2015

KUNDI E
Bayer Leverkusen v BATE Borislov
AS Roma v Barcelona

KUNDI F
Dinamo Zagreb v Arsenal
Olympiakos v Bayern Munich

KUNDI G
Chelsea v Maccabi Tel Aviv
Dynamo Kiev v FC Porto

KUNDI H
KAA Gent v Lyon
Valencia v Zenit St Petersburg

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog