EPL RATIBA
Jumanne Aprili 4
2145 Burnley v Stoke City
2145 Leicester City v Sunderland
2145 Watford v West Bromwich Albion
2200 Manchester United v Everton
MANCHESTER UNITED Jumanne Usiku wako kwao Old Trafford kucheza na Everton kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, ambayo hiyo na ile inayufuatia Wikiendi inayokuja dhidi ya Sunderland ndiyo itatoa mwelekeo wa Timu hiyo kuwemo 4 Bora au la kwa mujibu wa Meneja wao Jose Mourinho.
Akiongelea kuelekea Mechi hii na Everton, Mourinho alisema atashusha Kikosi kikali dhidi ya Everton na Sunderland na matokeo ya Mechi hizo ndio yataamua nini hatima yao kwenye Ligi na kwani baada ya hapo watacheza Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI na mkazo utakuwa huko.
Kufuzu 4 Bora ya Ligi kutawawezesha Man United kucheza UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao lakini pia kutwaa EUROPA LIGI kutawapa nafasi hiyo pia.
Hivi sasa kwenye EPL Man United wapo Nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 53 kwa Mechi 28 wakati Man City wapo Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 58 kwa Mechi 29.
Uso kwa Uso
-Man United hawajafungwa katika Mechi 4 zilizopita na Everton.
-Katika Mechi 49 za EPL, Man United Ushindi 33 Sare 8 Everton Ushindi 8
Man United wataingia Mechi hii wakitoka Sare ya 0-0 na West Bromwich wakati Everton walichapwa 3-1 na Liverpool Mechi zote zikichezwa Juzi Jumamosi.
Sare hiyo kwa Man United imeendeleza wimbi lao la Mechi 19 kutofungwa kwenye Ligi.
Hali za Vikosi:
Man United inategemewa kuwa nao tena Mfungaji wao Bora Zlatan Ibrahimovic na Kiungo Ander Herrera baada ya kumaliza Vifungo vyao vya Mechi 3 na 2 lakini itawakosa Majeruhi Juan Mata, Chris Smalling na Phil Jones huku pia kukiwepo uwezekano wa Paul Pogba kucheza baada ya kupona maumivu yake na kuanza mazoezi.
Everton inakabiliwa na Majeruhi 6 wakiwemo Seamus Coleman, alievunjwa Mguu akiichezea Nchi yake Republic of Ireland dhidi ya Wales Wiki ilyopita na pia Sentahafu wao wa Argentina Ramiro Funes Mori alieumia vibaya Goti.
Pia Mchezaji wa zamani wa Man United Kiungo Morgan Schneiderlin na Winga Aaron Lennon watakosekana kwa kuwa na maumivu.
Mechi ya Kwanza Msimu huu
Mapema Mwezi Desemba Zlatan Ibrahimovic aliifungia Bao Man United na Everton kusawazisha Dakika za lala salama kwa Penalti tata iliyotolewa kwa Rafu iliyofanywa na Mchezaji wa zamani wa Everton Marouane Fellaini na Adhabu hiyo kufungwa na Leighton Baines na kuifanya Gemu iishe 1-1.

0 maoni:
Post a Comment