Thursday, October 15, 2015


LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Oktoba 17

14:45 Tottenham v Liverpool
17:00 Chelsea v Aston Villa
17:00 Crystal Palace v West Ham
17:00 Everton v Man United
17:00 Man City v Bournemouth
17:00 Southampton v Leicester
17:00 West Brom v Sunderland
19:30 Watford v Arsenal

Jumapili Oktoba 18
18:00 Newcastle v Norwich
Jumatatu Oktoba 19
22:00 Swansea v Stoke


BAADA ya kupisha Mechi za Kimataifa kwa Wiki mbili, La Liga ipo dimbani Wikendi hii kwa Jumamosi kupigwa Mechi 5, Jumapili 4 na Jumatatu moja.
Vinara wa Ligi hii ya Spain ni Villareal ambao wako Pointi 1 mbele ya Timu 3 ambazo ni Real Madrid, Celta Vigo na Barcelona ambazo zote zimefungana zikiwa na Pointi 15 kila mmoja na kupishana tu kwa ubora wa Magoli.
Jumamosi Real Madrid wako kwao Santiago Bernabeu kucheza na Levante katika Mechi ya kwanza ya La Liga Wikiendi hii na Usiku Barcelona wataingia Uwanjani kwao Nou Camp kucheza na Rayo Vallecano.
Vinara Villareal wao wapo Nyumbani Jumapili kucheza na Timu ya 3 Celta Vigo.

LA LIGA
RATIBA
Jumamosi Oktoba 17

17:00 Real Madrid v Levante
19:15 Eibar v Sevilla
21:30 Barcelona v Rayo Vallecano
23:00 Valencia v Malaga
23:05 Real Betis v Espanyol

Jumapili Oktoba 18
13:00 Villarreal v Celta Vigo
17:00 Real Sociedad v Atletico Madrid
19:15 Getafe v Las Palmas
21:30 Deportivo v Athletic Bilbao

Jumatatu Oktoba 19
21:30 Sporting Gijon v Granada

Gari aina ya Toyota Probox lenye namba za usajili T336 CKH likiendelea kuwaka moto eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar.
 


 

 

Wananchi wakiendelea kuzima moto huo.


Moshi ukiwa umetanda.

Muonekano wa gari hiyo wakati ikiendelea kuwaka moto.
 


 
Kitengo cha zima moto kikiendelea na kazi yake.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Pemba jioni ya leo kwenye kutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Gombani ya Kale mjini Pemba.

Katika mkutano huo wa Kampeni,Dkt Magufuli ameahidi kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano,atadumisha na kuulinda Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ulioanzishwa na Waasisi wetu akiwemo Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere pamoja na Abeid Amani Karume.Dkt Magufuli kesho atahutubia kwenye mkutano mkubwa wa kampeni mjini Unguja.
Wananchi wa Kisiwani Pemba wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale ,wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kura kwa wananchi hao. 
Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akiwahutubia wakazi wa Pemba jioni ya leo kwenye kutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Gombani ya Kale mjini Pemba.Dkt Shein amewataka wakazi wa Kisiwani Pemba kuilinda amani iliyopo ndani ya kisiwa hicho na kuwa Wananchi wakajitokeze kwa wingi kupiga kura siku ya Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu Mwaka huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana Mama Shadia Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Gombani ya Kale kwa ajili ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein kabla ya mkutano wa kampeni kuanza jioni ya leo kisiwani Pemba.
Umati wa wakazi wa kisiwani Pemba kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wa kiswani Pemba wakifuatilia mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo,kwenye uwanja wa Gombani ya kale kisiwani humo.
Wananchi wa kiswani Pemba wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein walitumia jukwaa na mkutano huo kuwaomba kura za kutosha ili wakaiongoze Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano.
 
 Ma Dj walikuwa wakifanya mambo kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri.
 *************
Onyesho la muziki la Coke Studio ambalo linajumuisha Kolabo ya wanamuziki wa kitanzania kwa kushirikiana na wanamuziki wan je limeanza kurushwa nchini Jumamosi nchini kupitia luninga ya Clouds ikiwajumuisha wanamuziki Ally Kiba,Vanessa Mdee,Ben Pol na Fid Q ambao wanashirikiana na wanamuziki Wangechi,Maurice Kirya,Victoria Kimani na 2Face.
Baada ya uzinduzi huo zilifanyika party za kukata na shoka katika viwanja vya maraha sehemu mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya na Arusha zilzowajumuisha vijana kucheza muziki,kuimba na kufurahi na kujishindia zawadi mbalimbali za Coca Cola.
 Wadau mbalimbali ndani ya Coce Studio Party
 Baadhi ya mayanki waliohudhuria Coke Studio party wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye ukumbi wa Maisha Club jijini Dar es Salaam.
 Ilikuwa ni burudani kubwa vijana wakicheza muziki kwa furaha ndani ya Maisha Club.
 Vijana wakishiriki kuimba Coke Studio Party mkoani Mwanza
 zawadi mbalimbali zilitolewa katika party ya Mwanza kama anavyoonekana Masai akijichukulia zawadi katika party ya Mwanza
 Ma Dj walikuwa wakifanya mambo kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri
Watu wa rika mbalimbali walifika CokeStdi party kupata burudani kama wanavyoonekana baadhi yao pichani mjini mwanza


KEPTENI wa Manchester United Wayne Rooney anatarajiwa kuwa fiti kwa Mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu England huko Goodison Park dhidi ya Klabu yake ya zamani Everton.
Rooney aliumia Enka Wiki iliyopita akiwa Mazoezini na Timu ya England ambayo yeye pia ndio Nahodha na kuzikosa Mechi zake mbili za kumalizia Kundi E la EURO 2016 dhidi ya Estonia na Lithuania.
Baada ya Mechi hiii ya Jumamosi, Man United watapaa kwenda Moscow, Urusi kucheza na CSKA Moscow katika Mechi ya Kundi B la UEFA CHAMPIONS LIGI hapo Jumatano na kufuatia na mtanange wa Dabi ya Jiji la Manchester dhidi ya Man City Jumapili Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England
Wayne Rooney


Klopp akiwapa darasa wachezaji wake wakati wa mazoezi Melwood baada ya kukutana nao wakiwa wamerudi baada ya mechi za kimataifa kupigwa.Klopp akifurahia jambo wakati wa mazoeziKopp akiwa kwenye mazoezi Melwood


www.bukobasports.comFIFA imethibitisha kuwa inachunguza Uhamisho wa Eliaquim Mangala kutoka FC Porto kwenda Manchester City kutokana na kukiukwa kwa Sheria zinazokataza Mchezaji kumilikiwa na pande tatu.
Mangala, Mchezaji wa Kimataifa wa France, ameichezea Man City mara 31 kwenye Ligi Kuu England tangu ahamie hapo kutoka Porto Agosti 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 32.
Imedaiwa kuwa Kampuni iitwayo Doyen Sports, yenye Ofisi zake Nchini Malta na Jijini London, ililipa Pauni Milioni 2 Mwaka 2011 ili kununua Hisa za Umiliki wa Mchezaji huyo wakitegenea thamani yake itapanda.
Inasemekana baada ya City kumnunua Mangala kutoka Porto, Doyen Sports ililipwa Pauni Milioni 10.6 kama mgao wao wa mauzo ya Mchezaji huyo.
Ikiwa uchunguzi wa FIFA utabaini kuna ukiukwaji wa Sheria basi FC Porto, na si Man City, ndio watakaoadhibiwa kwa kupigwa Faini au kufungiwa Kuuza au Kununua Wachezaji.
Mangala alianza Soka lake kwenye Chuo cha Soka cha Klabu ya Belgium Namur na kisha kuchukuliwa na Standard Liege akiwa na Miaka 17 ambako alicheza Mechi Zaidi ya 100 kwa Timu ya kwanza na kisha kujiunga na Porto.


JANA Cristiano Ronaldo alitwaa Buti ya Dhahabu baada ya kuwa Mfungaji Bora wa Ulaya kwa Msimu uliopita alipombwaga Lionel Messi na Kocha wa Nchi yake Portugal ameonya juu ya kumtoa nje Staa huyo wakati wa Mechi.
Kocha wa Portugal, Fernando Santos, amemuonya Kocha wa Real Madrid, Rafa Benitez, juu ya madhara ya kumbadili Ronaldo wakati wa Mechi.
Jumanne Ronaldo alifanikiwa kuzoa Buti ya Dhahabu ya Ulaya kwa kufunga Bao 48 Msimu uliopita na kumpiku Lionel Messi wa Barcelona aliefunga Bao 43.
Hiyo ni mara ya 4 kwa Ronaldo kuzoa Tuzo hiyo na kuweka Rekodi kuwa Mtu wa kwanza kufanya hivyo.

Ronaldo ametwaa Buti ya Dhahabu ya Ulaya mara 3 akiwa na Real na mara moja akiwa na Man United katika Msimu wa 2007/08.
Akiongea Jana mara baada ya kumsindikiza Ronaldo kutwaa hiyo Buti ya Dhahabu, Kocha Fernando Santos alisema: "Haiwezekani kumtoa Ronaldo wakati wa Mechi. Kwanza mwenyewe hapendi!"
Ronaldo alitimiza Miaka 30 Mwezi Februari lakini Santos anaamini Ronaldo, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani, atawika zaidi na kutwaa Tuzo zaidi kwa sababu ana ari ya ushindi.


Meneja wa Chelsea Jose Mourinho ameadhibiwa na FA, Chama cha Soka England, kutokana na kauli yake na kupigwa Faini na kufungiwa Mechi 1 lakini Kifungo hicho kinasimamishwa kuangalia mwenendo wake.
Adhabu hiyo ya Faini ya Pauni 50,000 pamoja na Kifungo inatokana na kumshambulia Refa Robert Madley hapo Oktoba 3 mara baada ya Chelsea kukung’utwa 3-1 na Southampton.
Mourinho alikasirishwa na Refa Madley kutowapa Penati na kudai Waamuzi wanaogopa kutoa uamuzi kwa Timu yake.
Kauli hiyo iliwafanya FA wamfungulie Mashitaka ya Utovu wa Nidhamu wakidai kauli za Mourinho zinalenga kuonyesha Marefa wanapendelea.
Wakitoa Adhabu hiyo, FA wamesema Kifungo cha 1 kinasimamishwa kuangalia mwenendo wake hadi Tarehe 13 Oktoba 2016 ambapo anatakiwa asitoe kauli au tamko lolote kinyume na Sheria ya FA E3 na akivunja hilo basi Jopo Huru litachukua mkondo wake na Adhabu hiyo itarejeshwa.

waliotembelea blog