Thursday, October 15, 2015


JANA Cristiano Ronaldo alitwaa Buti ya Dhahabu baada ya kuwa Mfungaji Bora wa Ulaya kwa Msimu uliopita alipombwaga Lionel Messi na Kocha wa Nchi yake Portugal ameonya juu ya kumtoa nje Staa huyo wakati wa Mechi.
Kocha wa Portugal, Fernando Santos, amemuonya Kocha wa Real Madrid, Rafa Benitez, juu ya madhara ya kumbadili Ronaldo wakati wa Mechi.
Jumanne Ronaldo alifanikiwa kuzoa Buti ya Dhahabu ya Ulaya kwa kufunga Bao 48 Msimu uliopita na kumpiku Lionel Messi wa Barcelona aliefunga Bao 43.
Hiyo ni mara ya 4 kwa Ronaldo kuzoa Tuzo hiyo na kuweka Rekodi kuwa Mtu wa kwanza kufanya hivyo.

Ronaldo ametwaa Buti ya Dhahabu ya Ulaya mara 3 akiwa na Real na mara moja akiwa na Man United katika Msimu wa 2007/08.
Akiongea Jana mara baada ya kumsindikiza Ronaldo kutwaa hiyo Buti ya Dhahabu, Kocha Fernando Santos alisema: "Haiwezekani kumtoa Ronaldo wakati wa Mechi. Kwanza mwenyewe hapendi!"
Ronaldo alitimiza Miaka 30 Mwezi Februari lakini Santos anaamini Ronaldo, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani, atawika zaidi na kutwaa Tuzo zaidi kwa sababu ana ari ya ushindi.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog