Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platinumz ambaye ni balozi wa
Mziiki ambayo ni program ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom
Tanzania akiimba jukwaani Zari White Party iliyofanyika Mlimani City
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. App hiyo inawaletea
wateja burudani ya muziki kiganjani. Picha zote na BAZIRA.COM
Mchumba wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platinum... Bibie
Zari the bossylady akiwashukuru Watanzania waliofika katika Zari White
Party lililofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Umati wa Watanzania waliohudhuria katika Zari White Party
lililofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Mmoja ya vingozi wa Mziiki ambayo ni program ya simu za mkononi (mobile
app) ya Vodacom Tanzania akitoa maelezo machache kwa wateja waliofika
katika Zari White Party iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki iliyopita. App hiyo inawaletea wateja burudani ya
muziki kiganjani.
Msanii wa Kizazi Kipya, Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi akipozi katika zuria jekundu.
Msanii Shetta nae hakuwa nyuma kushow love mbele ya zuria jekundu.
Wafanyakazi wa Vodacom wakiwa amepozi katika zuria jekundu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platinumz ambaye ni balozi wa
Mziiki ambayo ni program ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom
Tanzania akiwa amepozi na mkewe mtarajiwa Zari katika Zari White Party
iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
iliyopita. Waliopo pembeni ni Madame Ritha, Msanii Ney Wa Mitego.
Wengine ni Msanii A.K.A (kushoto) toka nchini Afrika Kusini.
---
Mziiki
ni huduma ya muziki ya Afrika ambayo inatoa huduma hiyo kwa muziki wa
kitaifa na kimataifa, inajivunia kwa kiasi kikubwa kuwa sehemu ya
wadhamini wa pati ya Zari All-White party iliyofanyika ukumbi wa Mlimani
City jijini Dar es Salaam.
Mziiki ni sehemu ya
kuendeleza wasanii wa ndani na nje ya Afrika ambapo watumiaji wa simu za
smartphones za Android, iOS na BlackBerry wanapata nafasi ya kusikiliza
nyimbo mbalimbali kwa kupitia simu zao za mkononi.Wateja wa Kampuni ya
simu za mkononi ya Vodacom kwa kutumia intaneti ya wi-fi wanaweza
kuperuzi na kupata nyimbo ambazo wanaweza pia kuziweka katika miito yao
ya simu pia kuzisambaza kwa rafiki zao bure kwa kipindi cha mwezi mzima
ambao ni ofa.
Huduma hii inapatikana katika vifurushi vyote vya
Lite na Premium, na huduma ya Lite inapatikana pia kwa watumiaji wote
wa mtandao wa wi-fi ambao wanaweza pia kuperuzi moja kwa moja bila
malipo yoyote kila mahali mtandao wa Vodacom unapopatikana. Tangu Mziiki
izinduliwe mwezi Mei mwaka jana, imefanikiwa kuingiza zaidi ya wasanii
1000 wa Afrika ambao wanafanya vizuri mpaka sasa.
Huduma hii
imechaguliwa sana kwa ajili ya kuhakikisha Waafrika wanafurahia muziki
wao ambapo inaendelezwa na Spice Africa, na ilianzia Tanzania lakini kwa
sasa inazidi kukua katika nchi mbalimbali.
Afisa Mtendaji Mkuu
wa Spice Africa, Arun Nagar, alisema ‘Huduma ya hii ya kidijitali
inalenga zaidi kuibua vipaji katika nchi za ukanda wa Jangwa la Sahara
Afrika ambapo pia ni nafasi nzuri kwa wasanii mbalimbali kutangaza kazi
zao’.
‘Tunajivunia kuwa sehemu ya wadhamini wa sherehe za
Zari-White Party ambapo pia tuna imani kuwa Watanzania wengi watazidi
kufurahia huduma zetu’ Nagar aliongeza kuwa Mziiki ni huduma ambayo
inapatikana kirahisi mno kwa kutumia simu za mkononi kwa kupata huduma
ya muziki wa wasanii wa ndani na nje ya Afrika.
Diamond
Platnumz, ambaye ni balozi wa Mziiki Tanzania, alisema ‘Mziiki imekuwa
katika nafasi ya kutoa kipaumbele kwa wasanii mbalimbali kwa ajili ya
kupata changamoto kwa wasanii wakubwa kitaifa na kimataifa’ “Muziki wetu
umezidi kufanya vizuri katika nchi mbalimbali, na Mziiki inatoa ofa kwa
wadau mbalimbali wa muziki kusikiliza nyimbo wanazozipenda kwa kupitia
katika viganja vyao,” alisema Diamond Platnumz.
Burudani
mbalimbali zilizotolewa katika sherehe hizo za Zari White Party ikiwa ni
pamoja na muziki kutoka kwa DJ, muziki wa live kutoka kwa wasanii kama
vile Diamond Platnumz na Shetta wakati msanii mwalikwa atakua AKA,
kutoka Afrika Kusini.
Zari All-White Party 2015 imedhaminiwa na
Vodacom na Mziiki kwa kushirikiana na SK Entertainment, Clouds
Entertainment, Prime Time Promotions, Johnny Walker Gold label (
Serengeti Breweries) ambapo ilianza The All-White Parties mwaka 2009
nchini Uganda na Tanzania inafanyika mwaka huu kwa mara ya kwanza.