Friday, December 20, 2013


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki ametangaza kujiuzulu wadhifa wake leo Bungeni.




Suarez, 
 



, Suarez


 
Share
MASHABIKI wa Liverpool huenda wakachekelea kwa muda kukalia usukani endapo timu yao itaichapa Cardiff City mchana wa leo Jumamosi.
Arsenal inaongoza Ligi Kuu England ikiwa na pointi 35 lakini Liverpool na Chelsea itakayocheza keshokutwa Jumatatu na Arsenal wote wana pointi 33.
Potezea hiyo, ngoma ipo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam jioni hii. Kuna mechi matata ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga ambao ni mchezo wa kujifurahisha lakini uliobeba uzito wa aina yake kishabiki.
Simba inashuka uwanjani ikijivunia majembe yake mapya ambayo ni makipa, Yaw Berko, Ivo Mapunda, kiungo, Awadhi Juma, straika Ally Badru na beki Donald Musoti lakini kama haitoshi, Wekundu hao wana kocha mtaalamu na mwenye mbwembwe za aina yake Zdravko Logarusic kutoka Croatia.
Ndani ya kambi ya Simba mjini Zanzibar mambo yalikuwa shwari wiki nzima huku wakipigishwa tizi mara mbili kwenye Uwanja wa Fuoni.
Rudi kwa Yanga, ina vifaa vipya matata kama Juma Kaseja, Hassan Dilunga na straika aliyezua gumzo zaidi nchini baada ya kutua Jangwani, Emmanuel Okwi.
Timu hizo mbili zinakumbana zikiwa na wachezaji ambao wamewahi kuzichezea zote kwa nyakati tofauti jambo ambalo ni burudani nyingine.
Wachezaji hao kwa upande wa Yanga ni Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa, Ally Mustapha ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’, Athuman Idd na Okwi. Simba ina makipa Mapunda na Berko na Amri Kiemba.
KOCHA YANGA
Ernest Brandts ambaye ni kocha wa Yanga alisema; “Tumejiandaa vizuri na sasa tumebakiza dakika chache kabla ya mechi. Kiujumla timu ipo vizuri na majeruhi tuliyenaye ni Salum Telela pekee ambaye hayuko vizuri sana.”
“Ninachowaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuja kushabikia timu yao na naamini tutashinda mchezo huo bila shida,”alisema kocha huyo kwa kujiamini huku akikiri kwamba anaweza kumtumia Okwi dakika kadhaa.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema; “Tuna kila sababu ya kushinda mchezo huo, maandalizi yalikuwa mazuri na kila kitu kinakwenda sawa.”

Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
WABUNGE wamewataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha kujiuzulu kutokana na maovu yaliyofanywa wakati wa Operesheni Tokomeza wakati wakijadili ripoti iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.

Baadhi ya wabunge waliochangia kuhusu kujiuzulu kwa mawaziri hao ni Mbunge wa Mwibara (CCM) Kangi Lugola, Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Longido (CCM) Lekule Laizer.



Jeneza lenye mwili wa Clement Mabina likiwa mbele ya waombolezaji.
Waombolezaji wakiwa katika ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Mabina kwenye uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza.
Padre akiongoza ibada ya mazishi katika uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza.
Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja akifuatilia ibada ya kuuombea mwili wa Mabina.
Ndugu na jamaa wakishiriki ibada ya kumuombea Mabina.
 
 
 
 
 
Ndugu na jamaa wakiweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu Clement Mabina.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mazishi hayo eneo la Kanyamati, Kisesa mkoani Mwanza.
ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa (CCM), Clement Mabina (56), amezikwa mchana huu shambani kwake Kanyamati, Kisesa mkoani Mwanza. Mazishi hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, viongozi wa serikali, madhehebu ya dini, vyama vya siasa, wananchi na wakazi wa Kisesa ambao wameungana na ndugu, jamaa na marafiki kumsindikiza marehemu Mabina. Mazishi hayo yalitanguliwa na ibada iliyofanyika uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza



Emmanuel Okwi akilakiwa na shabiki maarufu wa Yanga, Steven (kulia) katika uwanja wa ndege wa Taifa wa Mwalimu Julius Kambalage Nyerere muda mfupi baada ya kufika.



Mshambuliaji wa Kimataifa wa timu ya Taifa ya Uganda aliyesajiliwa na Yanga SC, Emmanuel Okwi, ametua jijini Dar es Salaam akitokea nchini Uganda.
Mamia ya mashabiki wa Yanga walihudhuria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar kumpokea mwanasoka huyo mahiri aliyewahi kuichezea timu ya Simba SC.

Okwi ametua kwa ndege ya Shirika la Rwanda Air majira ya saa 10 jioni na kupokelewa na nyomi ya mashabiki wa Yanga pamoja na viongozi wa timu hiyo walioondoka naye.
Okwi anatarajiwa kuungana na kikosi cha Jangwani kitakachokwaana na mahasimu wao Simba SC katika mechi ya 'Nani Mtani Jembe' Jumamosi Desemba 21 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Mechi ya mwisho ya watani hao wa jadi ilimalizika kwa sare ya 3 - 3 ambapo Yanga walitangulia kufunga na Simba wakasawazisha.


Ulinzi ukiwa umeimarishwa wakati Okwi akiwasili jijini Dar akitokea Uganda kuungana na Yanga.



RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Desemba 21
15:45 Liverpool v Cardiff
18:00 Crystal Palace v Newcastle
18:00 Fulham v Man City
18:00 Man United v West Ham
18:00 Stoke v Aston Villa
18:00 Sunderland v Norwich
18:00 West Brom v Hull     
Jumapili Desemba 22
1630 Southampton v Tottenham
19:00 Swansea v Everton
Jumatatu Desemba 23
23:00 Arsenal v Chelsea

Alhamisi Desemba 26
15:45 Hull v Man United
18:00 Aston Villa v Crystal Palace
18:00 Cardiff v Southampton
18:00 Chelsea v Swansea
18:00 Everton v Sunderland
18:00 Newcastle v Stoke
18:00 Norwich v Fulham
18:00 Tottenham v West Brom
18:00 West Ham v Arsenal
20:30 Man City v Liverpool
Jumamosi Desemba 28
1545 West Ham v West Brom
1800 Aston Villa v Swansea
1800 Hull v Fulham
1800 Man City v Crystal Palace
1800 Norwich v Man United
2030 Cardiff v Sunderland
Jumapili Desemba 29
16:30 Everton v Southampton
16:30 Newcastle v Arsenal
19:00 Chelsea v Liverpool
19:00 Tottenham v Stoke
Jumatano Januari 1
15:45 Swansea v Man City
18:00 Arsenal v Cardiff
18:00 Crystal Palace v Norwich
18:00 Fulham v West Ham
18:00 Liverpool v Hull
18:00 Southampton v Chelsea
18:00 Stoke v Everton
18:00 Sunderland v Aston Villa
18:00 West Brom v Newcastle
20:30 Man United v Tottenham

waliotembelea blog