Thursday, May 7, 2015


Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid, ndio Klabu yenye thamani kubwa Duniani kwa Mwaka wa Tatu mfululizo kwa mujibu wa utafiti wa Forbes, Magwiji wa Mahesabu Duniani.
Licha ya Thamani ya Real kuporomoka kwa Asilimia 5 na kufikia Dola Bilioni 3.26, Mapato yao ya Dola Milioni 746 yamewaweka Nambari Wani.
Kwenye 20 Bora, Klabu 8 zinatoka Ligi Kuu England wakati Serie A ina Timu 4 ingawa ya juu kabisa ipo Nafasi ya 9.

Forbes wamesema Klabu za Italy zimeathirika Kibiashara Duniani kutokana na Skandali za Upangaji Matokeo Mechi, Viwanja vibovu na vya kizamani, Madeni na kuporomoka kwa Vipaji vya Wachezaji wao.
 

TIMU 10 ZENYE THAMANI ($ NI MABILIONI)
1. Real Madrid $3.26
2. Barcelona $3.16
3. Manchester United $3.10
4. Bayern Munich $2.35
5. Manchester City $1.38
6. Chelsea $1.37
7. Arsenal $1.31
8. Liverpool $982
9. Juventus $837
10. AC Milan $775

BARCELONA 3 vs 0 BAYERN MUNICH,

Dakika ya 77 na dakika ya 80 Messi alitikisa nyavu!Lionel Messi aliifungia bao safi kwa shuti kali baada ya kupewa pasi na Daniel Alves na dakika chache baadae dakika ya 80 Lionel Messi aliwachoma bao la pili na kufanya 2-0 dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani baada ya kupewa mpira na Ivan Rakitic. Kimya kimya!!Messi pia alifanya kutoa pasi safi kwa Neymar aliyejaza bao la tatu na mtanange kumalizika kwa bao 3-0Hakuna majibu!!Umechelewa tangu asubuhi!!Hadi nyavuni mwako!!Messi akishangilia bao lake la kwanzaPisha njia!ZIKIWA zimebaki dakika za nyongeza Neymar alitanguliziwa pasi na Messi na kisha kuwachomoka mabeki na kwenda kufunga bao la tatu na kumwancha kipa wa Bayern akiduwaa bila majibu.Neymar akifanya 3-0Neymar akishangilia bao lakeBarca wakipongezana mbele ya mashabiki wao Juan akimchomoka Iniesta wa Barca!
Neymar akiwania mpira wa KichwaSuarez dhidi ya Kipa ManuelSuarez!!Rafinha akipiga tiktaka!Chupuchupu Suarez achomeke bao!!Kipa Manuel akiokoa!Mpaka dakika 45 zinakatika hakuna mbabe, Timu zote mbili zilikuwa 0-0Kikosi cha Barcelona kilichoanza Wamekutana Mameneja timu zote mbili!Mchezaji wa zamani wa Arsenal na Mchambuzi wa soka kwa sasa Thierry Henry akiingia
VIKOSI:
Barcelona wanaoanza:
Ter Stegen, Dani Alves, Pique, Mascherano, Alba, Rakitic, Busquets, Iniesta, Suárez, Messi, Neymar
Akiba: Bravo, Xavi, Pedro, Rafinha, Bartra, Adriano, Vermaelen

Bayern Munich wanaoanza:
Neuer, Rafinha, Benatia, Boateng, Lahm, Alonso, Thiago, Bernat, Schweinsteiger, Müller, Lewandowski
Akiba: Reina, Dante, Martinez, Pizarro, Gaudino, Götze, Weiser
Mwali wa Klabu Bingwa huyoo!
Karibu!

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani - FIFA, Joseph Blatter ametuma salamau za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi kufuatia klabu ya Young Africans kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.
Katika salamu hizo za Blatter, amemuomba Rais wa TFF kufikisha salamu zake za pongezi kwa klabu ya Young Africans, wanachama, wapenzi wa mpira wa miguu kwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi mwakani katika michuano ya kimataifa barani Afrika.

 
 
Blatter amesema anatambua mafanikio hayo ya kutwaa Ubingwa, yametokana na na jitihada za 
uongozi, wachezaji, bechi la ufundi, madaktari, wanachama , washabiki na kila mmoja aliyeshiriki katika kufanikisha kutwaa Ubingwa huo.
Mpira wa miguu unapata mafanikio makubwa kwa kuvuka mipaka hadi kuwa kichochezi halisi cha maendeleo, unawasaidia wachezaji wa ngazi zote kuinua vipaji vyao na mbinu katika kuelekezwa na kubadilika wakati huo huo wakiwa wakiwa na nyoyo za ushirikiano.
Aidha Blatter amesema mpira wa miguu kwa sasa ni shule kwa maisha, vijana wa leo wanaweza kufaidika kupitia kucheza mpira wa miguu kwa ngazi ya kijamii na mtu mwneyewe binafsi, ndio maana amewapa salamu za pongezi Young Africans na kuendeleza kazi yao na kuongoza njia ya mafanikio.

Kujituma kwa klabu ya Young Africans kumewasaidia kushinda Ubingwa huu ikiwa ni ni mara ya 25, huu ni ushindi mkubwa katika mpira wa miguu.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)




Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2014- 2015, Yanga wakishangilia ubingwa wao huo mara baada ya kumalizika kwa mtanange wao dhidi ya Azam FC, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo. Mtanange huo ulimalizika kwa Azam FC kushinda Bao 2-1. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, MMG.
Mgeni Rasmi katika Mchezo huo, Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Yanga, Nadir Haroub cheti cha pongezi kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, Sepp Blatter kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara 2014 - 2015.Kushoto ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji.

Mgeni Rasmi katika Mchezo huo, Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangara akimpongeza Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa baada ya kuchaguliwa kuwa Mchezaji bora wa mwezi wa nne.

Wachezaji wa Timu ya Yanga wakiingia uwanjani tayari kwa kukipiga na timu ya Azam FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.

Mwali kabla ya kukabidhiwa kwa wenyewe.

Watu wa huduma ya kwanza wakifatilia mchezo huku wakiangalia yule atakaeumia na kwenda kumsaidia, hii ni kutokana na Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hapa jijini Dar leo.

Nyanda wa Timu ya Azam, Mwadini Ali akiwa makini kulinda wakati mashambulizi yakiandama upande huo.

Msambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa (kulia) akimkimbiza Kiungo wa Kati wa Azam, Mudathir Yahya wakati wa mtanange wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Azam imeshinda bao 2-1.














waliotembelea blog