Thursday, December 31, 2015


 Msanii Tekno Miles (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla iliyomtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea kuanzishwa kwake.
Dj rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young Guru” akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ya kumtambulisha rasmi Msanii Tekno Miles (Katikati) ambaye anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya. Dj huyo atasimamia vilivyo kazi yake katika shughuli nzima ya Tamasha hilo. 
Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija (Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Msanii Tekno Miles (wa kwanza kushoto) na Dj rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young Guru” wakati wa hafla iliyomtambulisha Msanii Tekno Miles kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea kuanzishwa kwake. 


Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini mkutano wa kumtambulisha Msanii maarufu Tekno Miles kutoka Nigeria uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambaye anatarajiwa kutumbuiza katika mkesha wa Tamasha la Grown and Sexy the Gold finale litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite jijini Dar es salaam.



Maandalizi ya Tamasha maarufu la Johnnie Walker “Grown and Sexy The Gold finale” kwa ajili ya kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya yanaendelea vizuri ambapo kwa mujibu wa waandaaji wa Tamasha hilo, “Capital events” kupitia wadhamini wao “Johnnie Walker” chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti wamemleta Msanii Tekno Miles kutoka Nigeria kutumbuiza laivu katika Tamasha hilo ambalo litakua la mwisho kabisa katika historia ya matamasha ya Grown and Sexy nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam,Meneja chapa wa pombe kali SBL Shomari Shija alisema, “Tumeamua kulidhamini Tamasha hili kama njia mojawapo ya kujumuika na kufurahi kwa pamoja na wateja wetu wa chapa za Johnnie Walker katika kuuaga rasmi mwaka huu wa 2015.
Bw. Shija aliongeza kuwa katika Tamasha la mwaka huu ambalo ni la mwisho katika historia ya mfululizo wa matamasha ya Grown and Sexy waliona ni vema kumleta msanii maarufu toka Nigeria “Tekno Miles” ambaye aliwasili jana usiku mida ya saa nane akitokea Nigeria tayari kwa kulipamba Tamasha hilo. Msanii huyo ambaye anatamba na vibao mbalimbali kwenye anga ya muziki hivi sasa kama Shoki, Duro na Wash atatumbuiza laivu kwenye Tamasha hilo ambalo litafanyika siku ya mkesha wa mwaka mpya katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga, Msasani karibu na Best Bite.
Sambamba na uwepo wa msanii huyo wengine wataopamba Tamasha hilo ni Dj Maarufu “Young Guru” ambaye ni Dj rasmi wa msanii Jay Z toka Marekani ambaye ataisimamia shoo hiyo vilivyo pamoja na malkia wa uswazi mwanadada “Shaa” kisura wa Tamasha hilo ambaye atasherehesha shughuli nzima katika usiku wa tukio.
Kwa upande wake Msanii Tekno alisema anafurahia kusherekea mkesha wa mwaka mpya akiwa Tanzania na kuahidi kuporomosha burudani ya nguvu kwa mashabiki wake watakaojitokeza kushuhudia Tamasha hilo la kufunga mwaka.



Naye Mwakilishi wa Capital events waandaaji wa Tamasha hilo Bw. Justin Massawe alisema “Tunawakaribisha wapenzi wote wa burudani na chapa ya Johnnie Walker kujitokeza kwa wingi kushuhudia Tamasha letu la mwisho la Grown & Sexy na kuahidi kuwa litakuwa la kufana zaidi kwani wamejipanga kutoa burudani ya nguvu na kuwafurahisha mashabiki mbalimbali.

“Ningependa kuwashukuru wadhamini wetu mbalimbali katika kipindi chote cha mfululizo wa matamasha haya tokea yalipoanzishwa rasmi kwa ushirikiano mzuri ambao wametupatia hadi hii leo tunapofunga rasmi tamasha hili la mwisho la Grown and Sexy the Gold finale.”
Bw. Justin hakusita pia kuwashukuru Johnnie Walker kwa kuhakikisha wanakamilisha mikataba yote ya kumleta msanii Tekno Miles pamoja na Dj Young Guru hapa nchini na kwa kuhakikisha kwamba tamasha la mwisho linakamilika kwa mafanikio” makubwa zaidi.
JANA Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ilibidi atulizwe munkari na Polisi ya kumpandishia Meneja mwenzake wa Sunderland Sam Allardyce wakati wa Mechi ya Ligi Kuu England Uwanjani Stadium of Light.
Klopp alipandwa na jazba wakati Jeremiah Lens wa Sunderland alipomchezea rafu mbaya Beki wa Liverpool Mamadou Sakho.
Wakati huo Liverpool walikuwa tayari washafunga Bao lao pekee na la ushindi kupitia Christian Benteke aliefunga Dakika ya 53.
Klopp aliamini Sakho ameumia vibaya na Lens alipaswa kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu lakini Refa alimpa Kadi ya Njano.
Hapo ndipo Klopp alipoanza kumbatukia Sam Allardyce, maarufu kama Big Sam, na munkari ulipopanda Polisi waliingia kati kumtuliza Klopp.
Baadae, Allardyce alisema Klopp alitumia maneno mabovu na ya matusi na kumweleza Meneja huyo wa Liverpool kama 'Mjerumani laini'.
Hata hivyo, bifu halikuendelea kwani mwishoni Mameneja hao walipeana mikono kama ilivyo desturi Mechi ikimalizika.

Wednesday, December 30, 2015

LA LIGA: ..FC BARCELONA 4 v 0 REAL BETIS

Barcelona wamerejea tena kileleni mwa La Liga baada ya Timu za Jiji la Madrid, Real Madrid na Atletico Madrid, mapema kupokezana kukaa juu,
Barcelona, wakicheza kwao Nou Camp, waliitwanga Real Bertis 4-0 na kuongoza La Liga wakiwa na Pointi 38 kwa Mechi 16 wakifuata Atletico wenye Pointi 38 kwa Mechi 17 na Real wakiwa wa 3 na Pointi zao 36 kwa Mechi 17.
Bao za Barca zilifungwa na Westerman, aliejifunga mwenyewe katika Dakika ya 29, Lionel Messi, dakika ya 33 na Luis Suarez, Dakika za 46 na 83.
Mapema Leo, Real Madrid iliichapa Real Sociedad 3-1 na kutwaa uongozi.

Nao Atletico Madrid walibanwa na Rayo Vallecano hadi mwishoni ambapo Bao za Angel Correa, Dakika ya 88 na Antoine Griezmann, Dakika ya 90, ziliwapa ushindi wa 2-0.



ENGLAND imeanika Listi ya Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Nchi yao ambapo pia ipo Tuzo kwa Chipukizi Vijana wa chini wa Miaka 21, U-21.
Kepteni wa England, Wayne Rooney, ambae alishinda Tuzo hiyo Mwaka Jana, ni miongoni mwa Wachezaji Watano wanaogombea.
Rooney Mwaka huu aliiongoza England kufuzu kuingia Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, ambazo zitachezwa huko France Mwezi Juni huku akihakikisha England inashinda Mechi zao zote 10 za Kundi lao.

Pia, Mwaka huu, Rooney aliivunja Rekodi ya Sir Bobby Charlton ya Ufungaji Bora katika Historia ya England kwa kufunga Bao 50 Rekodi ambayo iliwekwa na Charlton Mwaka 1968 alipofunga Bao lake la 49. 

Wagombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka:

Joe Hart (Manchester City)
Gary Cahill (Chelsea)
Raheem Sterling (Manchester City)
Wayne Rooney (Manchester United)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)

Kwa Vijana wa U-21, Straika wa Man United, Jesse Lingard, yumo kwenye Listi ya Wagombea Watano na huenda akashinda baada ya kung’’aa alipoichezea England U-21 Mwezi Juni Mwaka huu huko Czech Republic kwenye Fainali za Ulaya za U-21.

Wagombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa U-21:

Jack Butland (Stoke City)
Carl Jenkinson (West Ham United)
James Ward-Prowse (Southampton)
Jesse Lingard (Manchester United)
Nathan Redmond (Norwich City)

Kura kwa Wagombea hawa zitapigwa Mtandaoni na Masapota wa England na upigaji utafungwa Jumapili Januari 3.


Ronaldo akishangilia moja ya  bao lakeLeo La Liga imerejea tena na ndani ya Santiago Bernabeu, Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo aliiongoza Real Madrid kuichapa Real Sociedad Bao 3-1 na kuongoza Ligi hii ya Spain pengine kwa muda tu hadi baadae Usiku huu.
Ronaldo alikosa kuipa Real Bao wakati walipopewa Penati na yeye kuipaisha juu lakini Dakika ya 42 wakapata Penati nyingine na yeye kupiga tena na kufunga.
Hadi Mapumziko, Real 1 Sociedad 0.
Dakika 4 tu baada ya Kipindi cha Pili kuanza Real Sociedad wakasawazisha kwa Bao la Armindo Bruma lakini Ronaldo akaipa Real Bao la Pili alipounganisha Kona ya Marcelo.

Bao la 3 kwa Real lilifungwa na Lucas Vazquez, alieingizwa Kipindi cha Pili kumbadili Karim Benzema, na hilo kuwa Bao lake la kwanza kabisa kwa Real.

Wednesday, December 30, 2015


www.bukobasports.comLA LIGA
RATIBA
Jumatano Desemba 30

18:00 Real Madrid CF v Real Sociedad
18:00 Levante v Malaga CF
20:15 Rayo Vallecano v Atletico de Madrid
20:15 Sevilla FC v RCD Espanyol
20:30 SD Eibar v Sporting Gijon
22:30 FC Barcelona v Real Betis
22:30 Celta de Vigo v Athletic de Bilbao
22:30 Getafe CF v Deportivo La Coruna
23:00 Las Palmas v Granada CF
Alhamisi Desemba 31
18:00 Villarreal CF v Valencia C.F


Barclays Premier League
PosLogo &TeamPWDLGDPts
1ArsenalArsenal1912341539
2Leicester CityLeicester City1911621239
3Manchester CityManchester City1911351736
4Tottenham HotspurTottenham Hotspur199821835
5Crystal PalaceCrystal Palace19946731
6Manchester UnitedManchester United19865630
7West Ham UnitedWest Ham United19784529
8WatfordWatford19856429
9Stoke CityStoke City19856129
10LiverpoolLiverpool18765-127
11EvertonEverton19685726
12SouthamptonSouthampton19667324
13West Bromwich AlbionWest Bromwich Albion19658-623
14ChelseaChelsea19559-620
15Norwich CityNorwich City19559-1020
16BournemouthBournemouth19559-1220
17Swansea CitySwansea City19478-819
18Newcastle UnitedNewcastle United194510-1517
19SunderlandSunderland183312-1812
20Aston VillaAston Villa191513-198


MARA baada ya Jumatatu Usiku kutoka Sare 0-0 na Mabingwa Watetezi Chelsea Uwanjani Old Trafford na kusitisha wimbi la kufungwa Mechi 4 mfululizo, Meneja wa Manchester United Louis van Gaal aliibuka na kutamba hana mipango ya kujiuzulu.
Baada ya kuchapwa 2-0 na Stoke City Siku ya Boksing Dei, Man United waliibuka na kusakata Soka safi na kustahili kuifunga Chelsea lakini, kama kawaida, umaliziaji uliwaangusha.
Hali hiyo ilimfanya Louis van Gaal apige ‘abauti tani’ na kudai Wachezaji wake wamempa sababu ya kutojiuzulu tofauti na alivyodokeza huko Britannia Stadium mara baada ya kufungwa na Stoke. Jana Van Gaal alisema: “Wachezaji wakicheza namna ile hasa wakati huu wa presha kubwa, hamna sababu ya mimi kujiuzulu. Labda Vyombo vya Habari wanataka hivyo, ila sitafanya.”
Wakati huo huo, Mchambuzi wa Soka anaeaminika huko England, Andy Gray, Mchezaji wa zamani wa Scotland aliechezea Klabu kadhaa huko England, amedai Man United hawana uchu wa kumwajiri Jose Mourinho kama Meneja.
Mourinho, ambae alitimuliwa na Chelsea Wiki iliyokwisha, amekuwa akitajwa na wengi kuwa atachukua wadhifa wa Van Gaal.

Jumatatu, nje ya Old Trafford, kwenye Mechi na Chelsea, Wachuuzi walikuwa wakitembeza bidhaa kadhaa zikiwa na Nembo ya Man United na Jina la Jose Mourinho wakimpigia debe kuwa Meneja wa Man United.
Lakini Andy Gray anaamini Bodi ya Man United bado inamsapoti Van Gaal na haimtaki Mourinho ambae wanaona hulka yake haiendani na utamaduni wa Man United.
Patashika za Ligi Kuu England kuendelea tena leo, Kuna Mechi moja pekee ambayo itaamua nani anamaliza 2015 akiwa anaongoza Ligi.
Jana, Arsenal iliichapa Bournemouth 2-0 na kutwaa uongozi wa Ligi wakiwa na Pointi 39 kwa Mechi 19 wakifuata Leicester wenye Pointi 38 kwa Mechi 18, Tottenham ni wa 3 na wana Pointi 35 kwa Mechi 19 na wa 4 ni Man City wenye Pointi 35 kwa Mechi 18.
Leo huko King Power Stadium, Leicester wanacheza na Man City na wakishinda watarudi kileleni na wakitoka Sare watabaki Nafasi ya Pili.
Ikiwa City itashinda basi watapanda hadi Nafasi ya Pili.
Leicester wanatinga kwenye Mechi hii wakitoka kufungwa 1-0 na Liverpool na kupoteza wimbi lao la kutofungwa katika Mechi 10 wakati City ikiichapa Sunderland 4-1.
Wakati Leicester wana Kikosi kamili bila Majeruhi ingawa mapema walipatwa na wasiwasi wa Staa wao Jamie Vardy, ambae ndie Mfungaji Bora wa Ligi, kutocheza kutokana na kuugua, City watamkosa Nahodha wao Vincent Kompany ambae ni Majeruhi pamoja na majeruhi wengine Pablo Zabaleta, Fernando na Samir Nasri.
Yaya Toure kendeleza tena wimbi la magoli!



Tukiwa tunaelekea kuumaliza mwaka 2015 na kuingia mwaka mpya 2016 moja kati ya mitandao inayoandika stori za michezo duniani imeandika TOP ya wachezaji bora wakali wa Ligi Kuu Uingereza. Mtandao wa bleacherreport.com umeandika list ya wachezaji 20 wakali wa Ligi Kuu Uingereza kwa mwaka 2015.
Hii ndio list ya majina yote 20 mtu wangu.
  1. David De Gea (Man United/Hispania)
  2. Mesut Ozil (Arsenal/Ujerumani)
  3. Alexis Sanchez ( Arsenal/Chile)
  4. David Silva (Man City/Hispania)
  5. Sergio Aguero (Man City/Argentina)
  6. Chris Smalling (Man United/Uingereza)
  7. Santi Cazorla (Arsenal/Hispania)
  8. Harry Kane (Tottenham/Uingereza)
  9. Toby Alderweireld (Tottenham/Ubelgiji)
  10. Francis Coquelin (Arsenal/Ufaransa)
  11. Willian (Chelsea/Brazil)
  12. Riyad Mahrez (Leicester City/Algeria)
  13. Jamie Vardy (Leicester City/Uingereza)
  14. Philippe Coutinho (Liverpool/Brazil)
  15. Hector Bellerin (Arsenal/Hispania)
  16. Hugo Lloris (Tottenham/Ufaransa)
  17. Morgan Schneiderlin (Man United/Ufaransa)
  18. Scott Dann (Crystal Palace/ Uingereza)
  19. Sadio Mane (Southampton/Senegal)
  20. John Stones (Everton/Uingereza)


Monday, December 28, 2015

 
Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (mbele kulia) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Selestine Gesimba wakati wa mapokezi yake leo tarehe 28 Desemba 2015 katika ofisi yake mpya Mpingo House mara baada ya kuapishwa Ikulu mapema asubuhi ya leo. Nyuma yake kulia ni naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na anaeongoza utambulisho katikati yao ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru.
 Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akisaini kitabu cha wageni mara tu baada ya kuingia katika ofisi yake mpya iliyopo Mpingo House mapema leo tarehe 28 Desemba 2015 baada ya kuapishwa Ikulu na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Wanaoshuhudia kulia ni Naibu Wazari wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na Katibu Mkuu Dkt. Adelhelm Meru (kushoto).
Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) na Naibu Waziri Mhe. Eng. Ramo Makani (kulia) mara baada ya kusaini kitabu cha wageni ofisini kwake mapema leo tarehe 28 Desemba 2015.
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) na Naibu Waziri wake Mhe. Eng. Ramo Makani (wa pili kushoto), Katibu Mkuu wa Wziara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (wa kwanza kulia) na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Selestine Gesimba(kushoto). 
Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa tayari kwa mapokezi ya Waziri wao mpya Mhe. Prof. Jumanne Maghembe aliyeapishwa Ikulu leo na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania Mhe. John Pombe Magufuli.(Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii)

waliotembelea blog