Sunday, December 27, 2015


MENEJA  wa Manchester United Louis van Gaal amesema anaweza kuamua kwa hiari yake kuachia ngazi baada ya Jana kupokea kipigo cha 4 mfululizo huko Britannia Stadium walipochapwa 2-0 na Stoke City.
Huku kukiwa na uvumi mkubwa kwa Mdachi huyo ambae Kikosi chake hakijashinda katika Mechi 7 kuwa atafukuzwa, Jana akihojiwa na Wanahabari baada ya Mechi hiyo ambayo walishushwa hadi Nafasi ya 6 kwenye Ligi Kuu England, aliulizwa ikiwa anahofia kufukuzwa.

Van Gaal alijibu: "Hilo ni jambo nitajadiliana na Ed Woodward (Mtendaji Mkuu wa Man United) na si wewe!"
Van Gaal aliongeza: "Si lazima Siku zote Klabu ikufukuze. Wakati mwingine unaweza kuamua mwenyewe. Lakini mimi nataka kwanza kuongea na Bodi ya Man United, Wafanyakazi na Wachezaji lakini si nyinyi!"
Mechi inayofuata kwa Man United ni Uwanjani Old Trafford Jumatatu Usiku dhidi ya Mabingwa Watetezi Chelsea ambao nao Msimu huu wako taabani kiasi cha Wiki iliyopita kumfukuza Meneja wao Jose Mourinho na kumteua Guus Hiddink kama Meneja wa muda hadi mwishoni mwa Msimu.



Mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke akichuana na beki wa Mbeya City, John Kabanda katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 3-0. (Picha na Francis Dande).

Mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke akiwatoka mabeki wa Mbeya City.

Wachezaji wa Mbeya City wakimzonga mwamuzi Jeonesia Rukyaa kutoka Kagera baada ya Yanga kupata bao la kwanza.

Sio goli.............

Kocha wa Yanga, Hans Pluijm akitoka wakati wa mapumziko.

Mashabiki wa Mbeya City.
Polisi wakituliza fujo zilizotokea katika jukwaa la Mbeya City.
Donald Ngoma wa Yanga akichuana na Haruna Shamte.
Amis Tambwe wa Yanga akishangilia bao la pili aliloifungia timu yake.
Thaban Kamusoko (katikati) akishangilia na Deus Kaseke na Simon Msuva.
Wakishangilia kwa staili ya aina yake.
Deus Kaseke wa Yanga akiwania mpira na mchezaji wa Mbeya City.
Hatari....

Mashabiki wa Mbeya Cuty wakiwa wameduwaa wakishuhudia timu yao ikipata kipigo kutoka kwa Yanga.



Leo, Chelsea, wakiwa kwao Stamford Bridge, walianza himaya ya Meneja mpya Guus Hiddink kwa Sare.
Chelsea walitangulia kufunga katika Dakika ya 32 kwa Bao la Diego Costa na Watford kusawazisha kwa Penati iliyotolewa baada ya Nemanja Matic kuushika Mpira na Penati hiyo kufungwa na Troy Deeney katika Dakika ya 42.
Watford walikwenda mbele 2-1 kwa Bao la Odion Ighalo la Dakika ya 56 na Diego Costa kufunga Bao lake la Pili Dakika ya 65 na kuipa Chelsea Sare ya 2-2.
Mwishoni Oscar alikosa Penati ambayo ingeweza kuwapa ushindi Chelsea katika Mechi ya kwanza ya Meneja wao mpya Guus Hiddink.



YoungWayne RooneyMeneja wa Stoke CityMan United hii leo imeshushiwa kipigo chake cha 4 mfululuzo na Stoke City walioshinda 2-0 katika Mechi ya Ligi Kuu England na kumfanya kila Shabiki wa Timu hiyo kumchukia Meneja Louis van Gaal na kutaka atimuluwe haraka.
Katika Mechi hii ambayo Kepteni wa Man United Wayne Rooney alianza Benchi, Stoke walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 19 baada ya Pasi ya Geoff Camerok kwa Johnson kunaswa na Mchezaji wa Man United Memphis Depay lakini Kichwa chake hafifu cha kumrudishia Kipa wake De Gea kilitua kwa Johnson ambae haraka alimpasia Bojan Krkic na kufunga Bao laini.
Stoke City walipiga Bao lao la Pili Dakika ya 26 kupitia Marko Arnautovic baada ya Frikiki ya Bojan Krkic kuzuiwa na Ukuta wa Man United na kutua kwake na kuachia Shuti toka Mita 20.
Hadi Mapumziko Stoke 2 Man United Kipindi cha Pili Man United walimtoa Depay na kumuingiza Rooney na kidogo juu na kukosa Bao kadhaa na Mechi kwisha kwa 2-0.
Jumatatu Usiku Man United wako Kwao Old Trafford kucheza na Chelsea katika Mechi nyingine ya Ligi.

Kipindi cha kwanza kimemalizika 2-0 Stoke wanaongoza mpaka sasa.2-0Bojan Krkic dakika ya 19 anaipatia bao la kwanza Stoke City, Bao la pili lilifungwa na Marko Arnautovic dakika ya 26.
VIKOSI:
Manchester United XI (4-2-3-1):
De Gea; Young, Smalling, Jones, Blind; Carrick, Herrera; Mata, Fellaini, Depay; Martial.
Subs: Romero, Varela, McNair, Borthwick-Jackson, Schneiderlin, Pereira, Rooney.

Stoke XI (4-2-3-1): Butland; Johnson, Shawcross, Wollscheid, Pieters; Cameron, Whelan; Shaqiri, Afellay, Arnautovic; Bojan.
Subs: Haugaard, Joselu, Wilson, Van Ginkel, Adam, Diouf, Walters.


Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney amewashauri wachezaji wenzake kukaza buti ili kuokoa kibarua cha meneja wao Louis van Gaal.
Kufuatia kutoshinda katika Mechi 6 zilizopita na kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kibarua cha Van Gaal kimekuwa kwenye hatari kubwa.
Klabu hiyo imeporomoka hadi nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England na kujikuta wakiwa na Pointi 9 nyuma ya vinara Leicester City,

Rooney amenukuliwa akisema: "Hatujashinda katika wiki chache zilizopita na ni kawaida kupoteza kujiamini. Inabidi turejeshe imani kwani tuna michezo migumu na tunahitaji tuwe bora zaidi. Si kitu chema kufungwa kila mchezo. Ni ngumu kwa wachezaji. Tunaumia kwani sisi ni watu wa fahari na tunajionea fahari kuichezea Manchester United."Leo tutakazana mkuu!

waliotembelea blog