Tuesday, January 28, 2014

 




 


World's Biggest Ship Ever carrying 19,000 TEUs (bigger than Mc-Kinney Moller Maersk) ordered by CHINA Shipping Container Lines
 
 



 





 


 Another view of SAIL Amsterdam
 Secrets that Cruise Lines Would Never Tell About


 Inauma lakini ndio hivyo tena...mzee huyu ambaye ni mmoja kati ya wasanii walioanzisha kundi la Futuhi na kulifanya ling'are vilivyo kupitia kituo cha luninga cha Star TV, hatunaye tena duniani.
 Mzee Dude amefariki dunia Leo mida ya saa kumi na moja jionI.
Habari zinasema kuwa alizidiwa jana Jumapili na kukimbizwa katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Mzee Dude.


Lionel Messi(kulia) akikabiliana na mchezaji wa klabu ya Malaga Juanmi
Mshambulizi matata wa Barcelona Lionel Messi hauzwi na kilabu hiyo inapanga kujadili mkataba mpya na raia huyo wa Argentina, amesema rais wa kilabu hiyo Josep Maria Bartomeu.
Kuna uvumi kuwa Messi ambaye ni mshindi mara nne wa tuzo la Ballo d'Or, mwenye umri wa miaka 26, analengwa na kilabu ya Ufaransa ya Pris St-Germain.
Lionel Messi ameshiriki pakubwa katika kusaidia Barcelona kufunga zaidi ya mabao 36 katika msimu huu na amekuwa katika kikosi cha ushindi mara 16 ati ya michezo 20 iliyochezwa.
Katika mahojiano na kituo cha radio cha RAC1, yaliyonukuliwa katika mtandao wa Barcelona, Bartomeu anasema: "Kilabu kitaketi na kushauriana mkabala mpya. Tutafanya kila tunaloweza kuhakikisha kuwa yeye ndiye mchezaji anayelipwa mshahara bora zaidi."
Messi alipachika wavuni mabao 60 katika mechi 50 alimoshiriki katika msimu uliopita Messi lakini kwa sasa anajitahidi kufikisha mabao kama hayo msimu huu wa mwaka 2013-14.
Hadi kufikia sasa amefunga mabao 18 na manane kati ya hayo ndiyo aliyoyafunga katika Ligi, ingawa amesaidia kufunga mabao 36 katika mechi 20 alimoshiriki.


Marehemu Ann Waithera
Shirika la habari la BBC limempoteza mwandishi wa habari Ann Waithera.
Ann alikuwa anafanya kazi na BBC katika ofisi za Nairobi na amekuwa akiugua Saratani ya Ubongo kwa karibu miaka miwili.
Ann aliwahi kuwa ripota wa BBC mjini Addis Ababa Ethiopia.
Kabla ya kujiunga na BBC Ann alifanya kazi na shirika la habari la Nation Media Group nchini Kenya na Citizen TV. Ann alikuwa na umri wa miaka 39.
Waandishi wenza wa Ann BBC wameelezea watakavyomkumbuka Ann katika enzi zake alipokuwa anafanya kazi nao.
Razvan Scortea mmoja wa wakuu wa BBC amesema : "Nimeshtushwa sana na kifo cha Ann. Alikuwa mtu mzuri , mwerevu mpenda watu na mwenye matumaini kwa kila jambo. Mungu ambariki.''
Mkuu wa BBC Afrika Solomon Mugera ameelezea kuwa ni jambo la kuhuzunisha sana kumpoteza Ann.
''Nimehuzinika sana. Anne alikuwa mwandishi mahiri . Kila nilipomtembelea nilivutiwa sana na matumaini ya Ann kupona. Hata katika mkesha wa krismasi, nilipozungumza na Ann alikuwa mcheshi sana. Nakumbuka Ann ndiye alikuwa mwandishi wetu wa kwanza mwenye uwezo wa kuripoti katika lugha zaidi ya moja mjini Addis Ababa Ethiopia,'' alisema Solomon
Mkuu wa idhaa ya kiswahili ya BBC Ali Saleh naye pia ameelezea kushtushwa kwake na kifo cha Ann akimkumbuka kama mwandishi mahiri na mwenye kujitolea kwa kazi zake.
'Nakumbuka kufanya naye kazi kabla ya yeye kwenda Addis Ababa, na kufanya mipango ya kila alichotarajiwa kufanya. Matumaini mengi ila yamekatizwa mapema mno.'' alisema Elizabeth Blunt aliyekuwa mwandishi wa BBC mjini Addis Ababa kabla ya Ann kuchukua usukani kutoka kwake.
"Anne alikuwa mmoja wa waandishi mahiri wa BBC nchini Kenya . Kifo kimetupokonya mmoja wa waandishi wenye talanta kuu Afrika Mashariki.'' Kauli ya David Okwemba mhariri mkuu wa ofisi ya BBC Nairobi Kenya.
Mhariri mkuu wa idhaa ya Hausa mjini London Mansur Liman, ametuma rambi rambi kwa familia ya Ann, akiwaombea utulivu wakati huu mgumu.


waliotembelea blog